25.
25. Kuwa na Upendo
Upendo ni matunda ya vipengele vingi vya tabia njema vikiunganishwa pamoja. Kwa mfano kuongea na watu vizuri, kuwahurumia wakati wanamatatizo au kuwafanyia wema wa aina yoyote kama kuwasaidia kazi, kuwakirimu kitu n.k. ni miongoni mwa maadili mema yanayoleta upendo na mahusiano mema kati ya wanaadamu. Kinyume chake, kauli mbaya, ukatili, usengenyi, fitina, uchochezi, husuda, na matendo mengine mabaya kama haya yakitendwa kwa wan adam hujenga chuki na uadui.
Uislamu unatutaka tudumishe upendo kati yetu kwa kuwafanyia wenzetu mema tunayoyapenda na ambayo tungeliwataka wengine watufanyie. Pamoja na kusisitizwa na Uislamu kuwafanyia wengine mema na kujiepusha na kuwaudhi, tunashauriwa pia tuwe na tabia ya kupeana zawadi ili kukaza imara zaidi kifungo cha uhusianao mwema na upendo. Muislamu anashuriwa ajitahidi kutoa zawadi kuwapa wengine kila anapopata fursa ya kufanya hivyo na pia anashauriwa kupokea zawadi kwa moyo mkunjufu kila anapo pewa hata kama yeye ni tajiri na huyo anayempa ni maskini. Hebu turejee Hadith zifuatazo tuone jinsi Mtume (saw) anavyotuelekeza katika kupeana na kupokea zawadi:
Aysha(ra) amesimulai kuwa Mtume w a Allah amesema: Peaneni zawadi, kwani zawadi inaondoa chuki. (Tirmidh)
Aysha (ra) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akipokea zawadi akirudisha kitu kin gine badala yake kama badilisho kumpa yule aliyetoa. (Bukh ari).
Jab ir ames imulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yeyote yule aliyepewa zawadi na akawa na uwezo, na airudishie kwa zawadi nyingine , na yule ambaye hana kitu cha ku rejesha , na atoe shukurani na yule asiyetoa ahsante, ni mkosefu wa shukurani, na yule anayejifanya amepewa kitu na huku hakupewa, anakuwa kama yule aliyevaa magwanda(nguo) maw ili ya uw ongo ( ni mw ongo mkubw a-mnafiki). (Tirmidh, Abu-Daud).
Hadith hizi mbili zinatufahamisha kuwa zawadi isielekee upande mmoja tu bali kila anayepokea zawadi naye ajitahidi, kutoa zawadi ya namna nyingine kwa yule aliyempa kama ana uwezo na kama hana cha kutoa atoe ahsante na kumuombea dua aliye mzawadia.
Si tabia ya kiislamu kukataa zawadi- ya aina yoyote iliyohalali. Tunajifunza hili kutokana na hadith zifuatazo:
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Ningalikaribishwa unyayo wa mguu wa mbuzi (uliopikwa) hakika ningalikaribia na ningalipewa zawadi ya mguu wa mbuzi, hakika ningali pokea. (Bukhari).
Anas amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa harudishi manukato yoyote (aliyopewa kama zawadi). (Bukhari)
Ibn Sayid amesimulia: βOmar aliniteua kukusanya Zakat. Nilipo maliza na kuwasilisha zakat yote kwake, aliamuru nipwe ujira wangu. Nilisema: Nilifanya kwa ajili ya Allah na ujira wangu uko kwa Allah. Alisema: chukua kile ulichopewa kwa sababu niliteuliwa kufanya kazi kama hiyo wakati wa Mtume wa Allah. Aliniteua nikasema namna unavyosema. Mtume wa Allah akaniambia: unapopewa kitu ambacho hukukiomba, basi kula na toa sadaqa. (Abu Daud).
Hadith zote hizi zinatufundisha kuwa Muislamu akipewa kitu chochote cha halali asikatae hata kikiwa kidogo namna gani. Na kama hakihitajii sana, basi akipokee kisha atoe sadaqa. Pia tunapata fundisho kuwa Muislamu akikaribishwa na mwenziwe kula kitu chochote kilicho halali asikatae. Alimradi madhumuni ya kutoa na kupokea zawadi siku zote yawe ni kuzidisha upendo, udugu na mahusiano mema kati ya Waislamu na wanaadamu wote kwa ujumla.
Pia kutoleana salamu ni miongoni mwa nyenzo za kujenga upendo baina ya watu kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Abu Hurairah (ra) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema; βHam taingia Pep oni mpaka mw amini na hamtaamini mpaka mpendane. Je, nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? Toleaneni salamu baina yenuβ (Muslim)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 784
Sponsored links
π1
Kitau cha Fiqh
π2
Kitabu cha Afya
π3
Madrasa kiganjani
π4
kitabu cha Simulizi
π5
Simulizi za Hadithi Audio
π6
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
ZOEZI
Zoezi laΒ 1 (a) Ainisha maana ya sunnah kilugha na kisheria. Soma Zaidi...
Fadhila za kujenga msikiti
Kuna malipo makubwa kwa ambaye amejenga msikiti kwa ajili ya kuoatavradhi za Allah. Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran
Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki. Soma Zaidi...
Majina ya vijana wa pangoni
Makala hii inakwenda kukutajia majina ya vijana saba wa pangoni Soma Zaidi...
jamii somo la 32
Soma Zaidi...
Ukarimu na Sifa za kuwa Mkarimu na faida zake
30. Soma Zaidi...
(viii)Wenye khushui katika swala
Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala. Soma Zaidi...
jamii zoezi
Zoezi 2:1 1. Soma Zaidi...