Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kutunza joto la mtoto mara tu anapozaliwa,tunajuwa wazi kuwa Mama anaweza kujifungulia sehemu yoyote ile kabla hajafika hospitalini kwa hiyo mtoto anapaswa kuwa na joto la mwili la kutosha i
1. Kwanza kabisa kwenye hospitali ni lazima chumba cha kujifungulia kiwe na joto la kutosha madirisha yawe yamefungwa pamoja na milango kwa ujumla ili kuweza kutunza joto la kutosha kwa mtoto, pia na feni hazipaswi kuwepo kwenye chumba cha kujifungulia, pia hata kama Mama amejifungulia nyumbani sehemu ile inapaswa kuwa na joto la kutosha kwa Mama na mtoto pia.
2. Pindi mtoto anapozaliwa tu anapaswa kupangunswa kwa kutumia kitambaa safi na kisicho na unyevunyevu wowote,kwa kutumia kitambaa hicho kikavu, macho yanapaswa kupangunswa, uso,kichwa, nyumba na mbele , miguu na mikono na pia kitendo cha kupangusa mtoto kinapaswa kutumia mda mfupi ili kuepuka kumletea mtoto baridi na kuleta matatizo kwa mtoto yatokanayo na baridi na baada ya kupangusa mtoto nguo nzuri zenye joto zinapaswa kuwepo.
3.Na kitu cha kuzingatia ni kuwa mtoto anapaswa kukaa amefunikwa kichwa kwa kofia bila kuvumiliwa mpaka masaa ishirini na manne,na pia sio vizuri kumwosha mtoto mdogo aliyezaliwa ndani ya masaa ishirini na manne mpaka ruhusa kutoka kwa muuguzi kwa sababu kwa kipindi hiki mtoto anakuwa bado yuko kwenye uangalizi mkubwa , kwa hiyo wazazi na walezi wote wanapaswa kujua kuwa mtoto ni lazima awe na joto la kutosha katika masaa ya mwanzo ya kuzaliwa.
4.Ni vizuri sana kama mtoto amezaliwa kwenye hospitali ambayo ina vifaa vyote hasa vya kutunza joto, mtoto akiwa anapanguswa anapaswa kupangunsiwa na katika sehemu ile ya joto ili kuendelea kuwa na joto la kutosha, kwa hiyo ni vema kumfanya mtoto awe na joto la kutosha kwa sababu mtoto akipata baridi kwenye siku za Mwanzo anaweza kupata matatizo mbalimbali kama vile vichomi, Nimonia na Magonjwa mengine yanayoweza kuletwa na baridi.
5.Kwa hiyo akina Mama na walezi wa watoto wanapaswa kuwa makini na kuzingatia joto la mtoto akiwa hospitalini au akiwa nyumbani ili tuweze kuepuka kuendelea kuwepo kwa magonjwa ya Nimonia na vichomi kwa watoto.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Je ungependa kuijuwa Njia ya kuzuia mimba wakati wa tendo la ndoa?. Posti hii itakwenda kukufundisha ujanja huu.
Soma Zaidi...Posti inahusu zaidi mazoezi ya kegel, ni mazoezi ambayo ufanywa na watu wengi na sehemu yoyote yanaweza kufanywa kama vile chumbani, sebuleni, uwanjani na sehemu yoyote ile na kwa watu tofauti.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango, sio kwa imani potofu ambazo Watu utumia kuelezea uzazi wa mpango.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukuletea orodha ya vyakla vinavyoaminika kuongeza nguvu za kiume.
Soma Zaidi...Habari DoktaNikuulize kituu?
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba katika mwezi was kwanza
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uzazi wa mpango kwa njia ya kumwaga shahawa nje, hii ni njia mojawapo kati ya njia za uzazi wa mpango ambapo mwanaume humwaga nje mbegu ili asimpatie Mama mimba.
Soma Zaidi...Post hii itakujulidha mambo ambayo hupunguza nguvu za kiume
Soma Zaidi...