Siku za kupata mimba
Nitakujulisha siku ya kupata mimba na sifa zake, na namna ya kuweza kuitafuta
SIKU ZA KUPATA MIMBA
Kwa wale wanaohangaika kutafuta ujauzito makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakwenda kukujuza siku yako mujarabu ambayo utatapa ujauzito. Pia nitakujuza sifa za siku za kupata mimba. Unajuwa wanawake wanatofautiana sana katika mifumo yao ya uzazi, simaanishi maumbile, namaanisha hali zao. Watu wengi wanaelewa kuwa mwanamke anaweza kupata mimba siku zote. Hapa hii sio sahihi kabisa. Ukweli ni kuwa kuna siku maalumu na ni chache. Kitaalamu siku hizi hufahamika kama faertile window.
Siku ya kupata ujauzito utaweza kuijuwa kwanza kuangalia mambo kadhaa nitakayoyatajahapo chini. Kabla ya kuyajuwa mabo hayo haklikisha kuwa unakula lishe bora na inayoshawishi kutafuta mtoto kweli kama unatafuta mtoto. Kwa wanaume wale vyakula vya kuongeza mbegu za kiume kama karangga, korosho, kunywa maji mengi na vyakula vingine, wasiliana nasi hapo chini nikueleze. Pia hakikisha wewe na mwenza mnakula vyakula vya kuongeza hamu ya tendo lando kwaingi. Hakikisha mwili ni msafi na kila mmoja amejiandaa vyema kumpokea mwenza. Sasa nakwenda kukufundisha siku za kupata mimba.
1.Kutambuwa siku za kupata mimba kwa mahesabu.
Kwanza hakikisha unaujuwa tarehe yako ukiwa ni mwanmke, na kama ni mwanaume itambuwe vyema tarehe ya mwenzio. Tambua byema mzunguruko wake wa hedhi unakwenda siku ngapi. Ukitambua vitu hivyo sasa twende pamoja. Wataalamu wanaeleza kuwa mwaname anaweza kubeba mimba siku 12 mpaka 14 kabla ya kuingia hedhi yake. Pia wataalamu wanatueleza kuwa yai la mbegu ya mwanaume inaweza kuwa hai ndani ya siku tatu mbaka 5 na yai la mwanamke linaweza kukaa masaa 12 mpaka 24 . ila sanasana ni siku 3, yaani mbegu iliyoingia leo inaweza kurutubisha yai siku tatu zijazo. Hivyo tyujaalie mwaname ana mrunguruko wa hedhi wa siku 28. tutafanya hivi:-
Mfano wa kwanza mwenye siku 28
A.28 - 12 = 16 (ongeza moja iwe 17, kufidia yai la mama)
B.16 - 02 = 14
C.14 - 3 = 11 (tunapunguza 3 nyuma kufidia mbegu ya maba)
Hivyo mwanamke huyu siku zake za kupata mimba ni kati ya siku ya 11 mpaka 17 toka siku ya kwanza aingie hedhi.
Mfano wa pili mwenye siku 35
A.35 - 12 = 23 (ongeza 1 iwe 24)
B.23 - 02 = 21
C.21 - 03 = 18
Hivyo mwenye mzunguruko wa siki 35 siku zake hatari kupata mimba ni kati ya siku ya 18 mpaka 24 toka siku ya kwanza kuona hedhi.
Mfano wa tatu mwenye siku 21
A.21 - 12 = 9 (ongeza 1 iwe 10)
B.9 - 2 = 7
C.7 - 3 = 4
Mwanamke huyu anaweza kubeba ujauzito punde tu baada ya kumaliza hedhi mpaka siku ya 10
Unaweza kutumia mifano hii kitafuta skuku yako ya kupata mimba. Wanawake wanatofautiana sana siku zao. Kuna ambao ni 21, kuna ambao ni 35. ila kwa hali ya kawaida siku za hedhi ni kati ya 21 mpaka 35. ikizidi hapo ama kuwa chini ya hapo kutakuwa na shida kwenye mfumo wa homoni. Kama upo katika kutafuta ujauzito hakikisha unashiriki ngono katika siku zote hizo ama unaweza kuruka ruka ila hakikisha unaanza na siku ya kwanza, kisha unaweza kuacha moja na kushiriki inayofata.
2.Sifa za siku za kupata mimba.
Baada ya kujuwa kuitafuta siku ya kupata mimba sasa napenda ujuwe ssifa za siku hiyo. Sasa hata kama unaijuwa kwa mahesabu ukweli ni kuwa unaweza pia kuikosa kwani sio maalumu. Sasa hapa nitakurahisishia kazi kwa kukutajia sifa za siku hizo za kupata mimba.
1.Siku ya kupata mimba ina sifa hii, kwanza joto la mwili linakuwa kubwa tofauti na siku zilizotangulia na siku zijazo. Tambuwa kuwa hapa mwili utakuwa na joto ila haliusiani na ugionjwa wowote ama mambo mengine. Kwa mfano kuchelewa kulala, misongo ya mawazo maradhi na homa kwa pamoja hupelekea joto la mwili kupata. Joto tunalolizungumzia hapa halisababishwi na sababu yeyeote katika hizi.
2.Uteute wa ukeni utakuwa mwingi kulinganisha na siku zilizopita. Uteute huu husaidia kati akuzisafirisha mbegu za kiume kwenda kutungisha mimba. Uteute kuu ni mlaini na unateleza sana. Mwanamke anaweza kuuiona baada ya kuingiza kidole ndani sana kwenye shingo ya uzazi.
3.Siku hii mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo la ndoa kuliko siku zilizopita. Hii ni kutokana na miamsho iliyosababishwa na homoni ambazo zinaandaa mwili kwa ajili ya ujauzito.
Sifa hizi huweza kupotea baada ya kupata ujauzito ama muda wa kubeba mimba ukiisha. Mabadiliko hayo pia huweza kuathiriwa na mabo mengine kama matumizi ya uzazi wa mpango hasa wa kutumia sindano. Je utakuwa na maoni, maswali ama mapendekezo?. wasiliana nasi kwa hapo chini
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 ai web app π2 Dua za Mitume na Manabii π3 Madrasa kiganjani π4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 web hosting
Post zinazofanana:
Ongezeko la homoni ya estrogen
Posti hii inahusu zaidi ongezeko la homoni ya estrogen, kwa kawaida homoni hii ya estrogen inapaswa kulingana ikitokea ikaongezeka uleta madhara mbalimbali kwenye mwili na Kuna dalili ambazo zzz inaweza kujionesha wazi mpaka tukafahamu kuwa ni tatizo la o
Soma Zaidi...je kutokwa na maji mengi wakati wa tendo la ndoa inaashilia nini?
Je kutokwa na maji ukeni ambayo hayana harufu na meupe Hadi kuroanisha chupi, na je kutokwa na maji mengi wakati wa tendo la ndoa inaashilia nini?
Soma Zaidi...Je ?kipimo kikionyesha misitar miwili mmoja hafifu mwingine umekolea ni mimba au sio
Kipimo chamimba cha mkojo, huonyesha nestory miwili kuwa una mimba, na mmoja kuwa huna mimba. Sasa je ukitokea mmoja umekoleana mwingine hafifu? Endelea na pasti Γ’ΕΒΓ―ΒΈΒ hadi mwisho
Soma Zaidi...Mama mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa?
Mama mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka siku ya kujifungua Kama mume wake pamoja na yeye akiwa Hana maambukizi ya zinaa na Kama akiona dalili zozote zile za hatari ndio hataruhusiwa kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...NAMNA YA KUITAMBUA SIKU HATARI YA KUPATA MIMBA (UJAUZITO)
SIKU YA KUPATA UJAUZITO Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote.
Soma Zaidi...