Mambo ya kuzingatia kwa mtoto mara tu anapozaliwa

Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa mtoto pindi anapozaliwa,tunajua wazi kuwa mtoto anapoanza kutokeza kichwa tu ndio mwanzo wa kuanza kumtunza mtoto na kuhakikisha anafanyiwa huduma zote za muhimu na zinazohitajika.

Huduma muhimu kwa mtoto pindi anapozaliwa.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa mtoto aliyekamilika na kufikia wakati wa kuzaliwa ni kuanzia miezi thelathini na saba mpaka arobaini na mbili chini yake mtoto akizaliwa anakuwa hajafikisha umri kwa hiyo mtoto akitoa kichwa tu, muuguzi anasafisha Uso wa mtoto, midomo na pua kwa hiyo hatua hii ufanyika kwa kutumia kitambaa safi au vifaa vilivyoandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo ambavyo kwa kitaalamu huitwa gauze, ila kama Mama amejifungulia kwenye sehemu isiyo ya hospitalini anapaswa kufanya hivyo kwa kitambaa kisafi.

 

2. Pia mtoto akitolewa akitoka mzima anapaswa kuwekwa kwenye tumbo la mama yake moja kwa moja ili aweze kupata ujoto wa Mama, pia kwa wakati huo muuguzi au mtoa huduma kwa Mama anapaswa kumpangia mtoto kwa kutumia kitambaa safi, na anapompangusa awe kama anamtekenya tekenya ili kuweza kusaidia upumuaji na pia mapigo ya moyo, kwa hiyo Mtoto akiwa anapanguswa inabidi iwe kwa haraka ili kuweza kuepuka kuwepo kwa baridi.

 

3. Kwa wakati huo mtoto anapaswa kufunikwa kwa nguo safi akiwa kwenye tumbo la Mama yake ili kuweza kuepuka kuwepo kwa baridi na pia Mama anaweza kumnyonyesha mtoto hapo hapo, pia tunapaswa kujua kuwa mtoto anapaswa kunyonyeshwa ndani ya saa moja kabla ya kuzaliwa na hasizidi mda huo 

 

4.Baada ya kumaliza hayo, muuguzi au msaidizi wa Mama anapaswa kunawa vizuri na kuweka gloves ambazo ni maalum kwa kitaalamu huitwa stelire gloves kwa aji ya kukata kitovu, kwa hiyo kitovu kinapaswa kukatwa kwa uangalifu zaidi ili kuweza kuzuia maambukizi,na pia  hatua zinapaswa kufuatwa ili kukata kitovu kadri inavyopaswa .

 

5.Baada ya kukata kitovu, muuguzi anaweza kuendelea na kazi nyingine za kuhakikisha kubwa Mama yuko vizuri na kumfanyia Mama usafi na kutoa kondo la nyuma na kuhakikisha kuwa hakuna madhara yoyote kati ya Mama na mtoto na baadae Mama anaweza kuwekwa kwenye sehemu ya uangalizi ndani ya masaa ishirini na manne kwa ajili ya uangalizi zaidi na kwa kipindi hicho Mtoto na Mama wanakuwa kwenye uangalizi wa muuguzi

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/07/Thursday - 10:22:32 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1880


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-