Dalili za PID
Posti hii inahusu zaidi dalili za PID maana yake ni maambukizi kwenye pelvic kwa kitaalamu huitwa pelvic infection disease, ni ugonjwa unaoshambulia sana wanawake na wasichana
Dalili za PID
1.UTI za mara kwa mara
Unapokuwa na Maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo ya mara kwa mara ni dalili kubwa ya kuwepo kwa maambukizi kwenye pelvis, kwa sababu maambukizi kwenye pelvis usambaa mpaka kwenye kibofu Cha mkojo na kusababisha madhara mbalimbali ambayo mtu akienda kupima atagundulika na UTI kumbe ni maambukizi kutika kwenye pelvis.
2.Maumivu chini ya kitovu
Maumivu makali chini ya kitovu ni dalili mojawapo ya kuwa na Maambukizi kwenye pelvis, hii utokea pale ambapo maambukizi kutoka kwenye pelvis I usambaa Hadi kwenye chini ya kitovu na kusababisha maumivu chini ya kitovu, kwa hiyo baada ya kusikia dalili kama hizo mgonjwa anapaswa kwenda hospitalini kwa matibabu zaidi.
3.Kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya na kuwasha sehemu za Siri.hii ni mojawapo ya dalili za maambukizi kwenye pelvic ambapo bacteria ushambulia sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kusababisha madhara ya kutokwa na harufu mbaya ukeni na pia kuwepo kwa miwasho sehemu za Siri hasa wakati wa kukojoa au kama Kuna majimaji yoyote yamegusa sehemu za Siri pale penye maambukizi.
4.Kuvurugika kwa hedhi na mfumo wa homoni.
Kwa sababu ya maambukizi kwenye pelvis I usababisha hedhi kuvurugika na homoni kubadilika hali hii usababishwa na Maambukizi ambayo uenea zaidi kwenye via vya uzazi na kuaribu sehemu mbalimbali ambazo zinahusikana na hedhi kwa hiyo mda mwingine damu utoka kwa mabonge mabonge au pengine kubadilika kabisa kwa sababu ya maambukizi.
5. Kutokwa na maji kwenye sehemu za Siri yenye rangi ya kijani na rangi ya njano, hali hii utokea kwa sababu ya maambukizi kusambaa kwenye sehemu za via vya uzazi na kusababisha maji ya rangi isiyo ya kawaida. Kwa hiyo tunapaswa kwenda hospitalini kupima na kutafuta dawa maana huu ugonjwa unatibika haspitalini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Tatizo la muingiliano wa majimaji ya Amniotic au seli za Mtoto kwenye Damu ya mama mjamzito.
posti hii inaelezea kuhusiana tatizo la muingiliano wa majimaji ya seli za Mtoto kwenye Damu ya mama mjamzito ambao hujulikana Kama Amniotic Fluid Embolism ni hali adimu lakini mbaya ambayo hutokea wakati Maji ya amniotiki Majimaji ambayo huzunguka mtot
Soma Zaidi...Ishara za Uchungu wa Kujifungua Zinapoanza
Kufika kwa wakati wa kujifungua ni hatua muhimu na yenye msisimko mkubwa kwa kila mama mjamzito. Ni kawaida kuhisi wasiwasi kuhusu jinsi utakavyotambua kuwa uchungu umeanza. Dalili za uchungu wa kweli zinatofautiana na maumivu ya kawaida ya ujauzito (Braxton Hicks). Makala hii inaelezea ishara kuu unazopaswa kuzizingatia ili kujua kuwa wakati wa kuonana na malaika wako umefika.
Soma Zaidi...Damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito
Soma Zaidi...Nimetoka kufanya tendo la ndoa ghafla tumbo likaanza kukaza upande wa kushoto na kutoka maji yenye uzito wa kawaida kama ute mengi je hii itakuwa ni nini
Maumivu yavtumbo huwenda yakachanganya sana, Keane yanahusianana sababu nyingi sana. Kina baadhi ya watu hupata na maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa ama punde tu baada ya kumaliza.
Soma Zaidi...Njia za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha.
Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini v
Soma Zaidi...Fahamu matatizo yanayowapata watoto waliozaliwa kabla ya wakati au mapema (premature)
Kuzaa kabla ya wakati ni kuzaliwa ambayo hufanyika zaidi ya wiki tatu kabla ya kuzaliwa kwa mtoto au kuzaliwa mapema ni moja ambayo hutokea kabla ya mwanzo wa wiki ya 37 ya ujauzito. Kawaida, ujauzito hudumu kama wiki 40.
Soma Zaidi...