Namna ya kuangalia kama mtoto aliyezaliwa anapumua

Namna ya kuangalia kama mtoto aliyezaliwa anapumua

Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuangalia kama mtoto anapumua pindi anapozaliwa,tunajua kabisa ili kujua na kuelewa kama mtoto yuko hai ni lazima kuangalia upumuaji wa mtoto,ambapo tunaitambua pale anapolia tu.

Namna ya kuangalia kama mtoto aliyezaliwa anapumua.

1. Kwanza kabisa wakati tunapokuwa  tunapangusa mtoto tunapaswa kuangalia upumuaji wake kwa kuangalia Dalili zote za upumuaji.

 

2.Vile vile Tunapaswa kusikiliza sauti inayotoka wakati wa kupumua na kuangalia jinsi kifua kinavyocheza cheza kwa kutumia sauti tunaweza kugundua kuwa mtoto yuko hai na anaweza.

 

3.Vili vile tunapaswa kuangalia kama mtoto anapumua haraka haraka na kwa urahisi au kuangalia kama mtoto analia kwa sababu kulia ni Dalili mojawapo ya kupumua kwa mtoto.

 

4. Na pia mtoto anapaswa kuonekana anapitisha hewa kwenye pua kwa urahisi sio kwa shida, ukiona anapitisha hewa kwa shida hiyo ni Dalili kwamba kuna Tatizo ambalo halijaenda sawa na pia ni lazima kumshughulikia mtoto.

 

5. Kwa kawaida mtoto anayepumua vizuri ni yule ambaye analia tu baada ya kuzaliwa, anapumua vizuri na kwa haraka haraka na upumuaji wake ni wa kawaida hakoromi au hakuna kitu chochote kinacholeta shida wakati wa upumuaji.

 

6. Na mtoto ambaye hapumui vizuri ni yule ambaye  anahangaika wakati wa kupumua na anapumua kwa kutumia hewa nzito na pumzi haieleweki au kwa wakati mwingine hakuna kupumua kabisa, hali ya namna hii ikitokea huduma inapaswa kutolewa haraka.

 

7. Kwa wakati mwingine kuna watoto ambao wanazaliwa na hewa yao inakuwa ya shida na kwa wakati mwingine wanazaliwa wakiwa hawapumui kabisa kwa hiyo tunapaswa kuwasaidia kwa kufungua sahemu muhimu kama vile kwenye mdomo, kwenye pua au kifuani labda kuna baadhi ya vitu ambavyo vimefunga hewa isiweze kupita.

 

8. Pamoja na upumuaji wa shida kwa watoto kuna baadhi ya watoto wanaozaliwa wakiwa na uzito mkubwa na wanahitaji uangalizi wa karibu ili waweze kupata huduma kwa sababu walicheleweshwa wanaweza kupata matatizo mbalimbali.

 

9. Kwa hiyo baada ya kugundua kubwa mtoto anapumua vizuri na hana tatizo lolote ni lazima kumpeleka kifuani mwa Mama ili aendelee kuishi hapo kwa ajili ya kupata joto la Mama na kwa wale ambao hawapumui ni vizuri kabisa kuwahi kuwapeleka kwenye vituo vya afya kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 2440

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 ai web app     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Dalili za mimba ya siku 4

Unaweza kutaka kujuwa je naweza kupata dalili za mimba baada ya siku nne toka ujauzito kutungwa? ama baada ya siku nne toka kushiriki tendo la ndoa. Makala hii itakwenda kujibu maswali haya na mengineyo.

Soma Zaidi...
Kupima ujauzito kwa kutumia chumvi, sukari na sabuni

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni

Soma Zaidi...
Habar doctor mm nahc kuwa ni mjamzito tumbo la chin ya kitovu linaniuma muda mwingine linaacha chuchu zinawasha na cku niliyokutana na mume wangu ni cku 11

Kuna uwezekano una ujauzito ila hujajijuwa, huwenda hujapata dalili zozote. Unataka kujuwa kama una ujauzito baada ya tendo la ndoa.

Soma Zaidi...
DARASA LLA AFYA na afya ya uzazi na malezi bora kwa jamii

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo kabla ya kupata hedhi

Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba.

Soma Zaidi...
Dalili 10 za kukaribia kujifungua pamoja na uchungu wa kujifungua

Download Kitabu cha elimu ya Ujauzito na malezi ya mimba.

Soma Zaidi...