Namna ya kufunga kitovu cha mtoto.

Posti hii inahusu zaidi njia au namna ya kufunga kitovu cha mtoto mara tu anapozaliwa, kwa kawaida tunafahamu kwamba ili mtoto aweze kuishi akiwa tumboni anategemea sana kula na kufanya shughuli zake kwa kupitia kwenye plasenta kwa hiyo mtoto akizaliwa tu

Namna ya kufunga kitovu cha mtoto.

1. Tufahamu kuwa kitovu cha mtoto kinakuwa kimeunganika na Mama pindi mtoto anapozaliwa kwa hiyo mtoto anapolia tu pale wakati wa kuzaliwa anaanza kutegemea hewa ya nje na kuacha kutegemea hewa ya kupitisha kwenye plasenta kwa hiyo kitovu hicho kinaweza kutenganishwa na pia mtoto akaanza kutumia maziwa ya Mama kama chakula chake.na kitovu hiki kinahitaji sana umakini wakati wa kutenganishwa ili kuweza kuepuka matatizo ya Maambukizi na kuoza kwenye sehemu ya kitovu.

 

2. Kwa hiyo hatua ya kwanza tunapaswa kutenganisha mtoto kutoka kwenye plasenta kwa hiyo tunapima sentimita kuanzia nane mpaka kumi na tunabana, hizo sentimita zinaanzia kwenye kitovu cha mtoto tunafanya hivyo ili kuepuka kuchanganya damu ya Mama na mtoto.

 

3. Wakati wa kufanya hivyo tunazingatia usafi wa hali ya juu na kutumia glovesi nzuri na za kitaaluma zinazoitwa stelire gloves, kwa kufanya hivyo tunaepuka Maambukizi yanayoweza kujitokeza kwa wakati wowote.

 

4. Pa damu ukiacha kuzunguka tunapima sentimita mbili kutoka kwa mtoto na kufunga vizuri na pia tunapima sentimita tatu kutoka kwenye sentimita mbili na tunafunga, kwa hiyo tunakata kati kati ya sentimita mbili na tatu na tunazingatia usafi kwa kuweka kitambaa ili damu iweze kudondoka humo.

 

5.Baada ya kumaliza kuweka vizuri kitovu chukua vifaa vyote kwenye sehemu muhimu na inayohitajika na kuosha mikono vizuri kwa maji na sabuni hatimaye unaweza kuendelea na vitu vingine.na pia walezi na wazazi wote wanapaswa kuachana na mila potofu za kuweka vitu visivyofaa kwenye kitovu kwa hiyo niache kitovu kitakauka chenyewe.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/07/Thursday - 07:21:59 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2603


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-