Posti hii inahusu zaidi uchungu usio wa kawaida kwa akina Mama, kwa kawaida uchungu unapaswa kuwa ndani ya masaa Kumi na mawili ila Kuna wakati mwingine uchungu unaweza kuwa zaidi ya masaa Kumi na mawili na kusababisha madhara yasiyo ya kawaida kwa Mama n
1. Kwanza kabisa uchungu usio wa kawaida ni uchungu ambao utokea zaidi ya massa kumi na mawili na uchungu unakuwa na nguvu kama kawaida na mtoto hatoki tumboni mwa Mama kwa hiyo Kuna sababu zinazosababisha uchungu kupita mda wake,
2. Uchungu kuwa kidogo.
Kwa kawaida uchungu unapaswa kuwa na nguvu Ili kuweza kumfanya mtoto apite na kuzaliwa mapema lakini tatizo utokea pale uchungu unapokuwa kidogo na kusababisha mtoto asitoke mapema na pia mtoto anakuwa Hana uwezo wa kusukuma viungo vya Mama na kusababisha uchungu, hali inayofanya mtoto kutozaliwa mapema kwa mda
3. Kiuno cha Mama kushindwa kupitisha mtoto, Kuna wakati mwingine muundo wa kiuno cha Mama ushindwa kupitisha mtoto na hivyo kusababisha uchungu kuwapo kwa mda mrefu, hali hii kwa kitaalamu huitwa cephalopelvic disproportion, kwa hiyo wauguzi na wote wanaozalisha wanapaswa kumtambua tatizo hili na kuhakikisha kuwa mtoto anapata sehemu Sahihi ya kupita na ikiwezekana upasuaji unapaswa kutolewa Ili kuruhusu mtoto apitishwe.
4. Ikitokea mtoto akakosa msaada wa haraka na kukaa tumbo bila kutoka hali hii usababisha mtoto kuchoka sana na Mama akilazimisha kusukuma akiwa kwenye hali hii anaweza kusababisha kumuua mtoto kwa kumbana na kusababisha ulemavu kwa Mama kwa hiyo ni vizuri kabisa Mama kuangaliwa njia mapema Ili kuweza kumtambua kama mtoto ataweza kuzaliwa kwa njia ya kawaida au upasuaji ufanyike, kwa hiyo Ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto ni vizuri kuwepo wahudumu wenye sifa za kuzalisha.
5. Mtoto kutanguliza USO.
Kuna wakati mwingine mtoto utanguliza uso badala ya kichwa hali hii usababisha mtoto kushindwa kutoka na kutumia mda mrefu wa mtoto kuzaliwa, kwa hiyo Mama anaweza kupata uchungu kwa mda mrefu kwa sababu ya kitangulizi cha mtoto, ni vizuri kabisa kuangalia mtoto katanguliza nini Ili kuweza kuepuka mtoto kuzaliwa amechoka na kusababisha matatizo kwa Mama na mtoto pia
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa mtoto pindi anapozaliwa,tunajua wazi kuwa mtoto anapoanza kutokeza kichwa tu ndio mwanzo wa kuanza kumtunza mtoto na kuhakikisha anafanyiwa huduma zote za muhimu na zinazohitajika.
Soma Zaidi...Ni kweli kuwa kutema mate mara kwa mara inaweza kuwa ni dlili za ujauzito. Lakini itambulije kuwa pekee sio kithibitishi cha ujauzito.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake
Soma Zaidi...Mwanaume na mwanamke wanapo kutana na kujamiina kama mwanamke yupo kwenye ferlile process ni rahisi kupata mbimba. Sparm Zaid ya million moja huingia kwenye mfuko wa lakin sparm moja ndio huweza kuingia kwenye ovum(yai)lakin nyingine hubaki kwenye follopi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo anyopaswa kujua akiwa mjamzito. Ni mambo muhimu ya kuzingatia kwa mama akiwa mjamzito.
Soma Zaidi...Kipimo cha mimba kwa mkojo kimekuwa kikitumika sana kuangalia ujauzito. Kipimo hiki kinapotumika vibaya kinaweza kukupa majibu ya uongo. Kuwa makini na ujue muda sahihi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya matumizi ya sindano za kuzuia mimba kwa vijana ambao hawajafikilia mpango wa kuanza kujifungua watoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili za Mama mwenye kifafa cha mimba, ili kifafa cha mimba kiweze kutokea lazima kuna dalili ambazo uweza kutokea kwa Mama kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...