Vyanzo vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito
Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito, kwa sababu kuna sababu nyingi ambazo Usababisha mwanamke kushindwa kupata ujauzito kama tutakavyoona hapo mbeleni
Vyanzo vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito.
1. Mayai kushindwa kupevuka.
Hili ni tatizo ambalo uwakumba wanawake kwa kiwango cha asilimia arobaini kwa hiyo
mayai yakishindwa kupevuka usababisha kuwepo kwa ugumba.
2. Maambukizi sugu ya PID.
Kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi ya PID usababisha sehemu mbalimbali za via vya uzazi kuziba na kushindwa kuruhusu mayai kupita kwa ajili ya urutubishaji.
3. Mvurugiko wa homoni.
Na lenyewe hili ni tatizo kubwa ambapo homoni uweza kuongezeka au kupungua kwa hiyo kama ni homoni za uzazi zikapungua ni shida na ikiwa zikaongezeka na nalo ni tatizo jingine kwa hiyo homoni zinapaswa kulinga kabisa na kuwa sawia.
4. Kuwepo kwa uvimbe au maji maji kujaa kwenye sehemu ya kupitisha mayai.
Kuna wakati mwingine mirija ya kupitisha mayai inaweza kujaa maji maji au kwa wakati mwingine kuziba kabisa kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha maambukizi , kwa hiyo mayai hayawezi kupita kutoka kwenye ovaries na kuingia kwenye mirija kwa ajili ya urutubishaji.
5. Au wakati mwingine Kuna wakati panakuwepo na uvimbe , na pia uvimbe huo hauwezi kuruhusu mayai kupita kutoka kwenye ovaries mpaka kwenye mirija ya urutubishaji mpaka uvimbe huo kuondolewa ndipo mayai yanaweza kupita kwa ajili ya urutubishaji.
6. Mayai kuharibika kabla ya umri.
Kuna wakati mwingine mayai yanaweza kuwepo kabisa na ya kutosha na kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi mayai hayo uharibika kabla ya umri wake hali ambayo usababisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha ugumba kwa akina Mama kwa hiyo matibabu ni lazima Ili kuweza kuzuia maambukizi ya nayosababisha kutokomaa kwa mayai.
7. Kuwepo kwa matatizo au asidi nyingi kwenye mlango wa kizazi na uke .
Kwa sababu asidi ya kwenye uke uwa ni ya kawaida kwa ajili ya kuruhusu mbegu kupita na kurutubisha mayai Kuna wakati asidi inakuwa nyingi na kusababisha kuuua megu za kiume kabla hazijaendea kurutubisha mayai.
8. Kuwepo kwa makovu kwenye mji wa mimba.
Kuna wakati mwingine kunakuwepo na makovu kwenye mji wa mimba hali ambayo usababisha mimba kutoweza kutungwa kwa sababu ya kutokuwepo sehemu ya kutungwa.
9. Kulegea au kuziba kwa shingo ya kizazi.
Kuna wakati kunakuwepo kwa tatizo la kulegea na kuziba kwa shingo ya kizazi hali ambayo usababisha mimba bkushindwa kutungwa.
10. Uzito wa kupita kiasi.
Kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta mwilini usababisha kitendo cha urutubishaji kuleta shida na kusababisha ugumba, kwa hiyo akina Mama wenye uzito wa kupita kiasi ni vizuri kabisa kupunguza Uzito na kupata uja uzito.
11. Unywaji wa pombe kupita kiasi na uvutaji wa sigara kupita kiasi.
Kuna akina Mama wenye tatizo la kuvuta sigara kupita kiasi na kupiga pombe ya uhakika hali ambayo usababisha baadhi ya homoni kushindwa kufanya kazi vizuri na hatimaye kuwepo kwa ugumba.
12. Magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji.
Kwa kawaida Kuna tatizo la magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji nayo uharibu ubora wa mayai na mzunguko wa damu kwa hiyo ni vizuri kabisa kutibu magonjwa haya kabla hayajaleta matatizo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 ai web app 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Kiwango cha juu cha Androgen
Posti hii inahusu zaidi homoni ya androgen, ni homoni ambayo imo kwa wanaume na ikizidi kwa kiwango chake inaweza kuleta shida kwenye mwili wa binadamu kwa hiyo homoni hii inaweza kuleta shida iwapo ikiongezeka kwa kiasi kikubwa.
Soma Zaidi...Fahamu kuhusu fangasi za ukeni
Posti hii inahusu zaidi fangasi za ukeni, hili ni tatizo kubwa ambalo linawakumba watoto, akina dada na wanawake kwa hiyo na vizuri kujua Dalili zake na kuweza kuchukua hatua mapema.
Soma Zaidi...Imani potofu kuhusu uzazi wa mpango
Post hii inahusu zaidi imani potofu kuhusu uzazi wa mpango, ni imani walizonazo Watu kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango.
Soma Zaidi...Zijuwe Dalili za minyoo na dalili kuu 9 za minyoo
Utajifunza dalili za minyoo, sababu za minyoo na namna ya kujiepusha na minyoo. Dalili kuu 5 za minyoo mwilini
Soma Zaidi...Mama mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa?
Mama mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka siku ya kujifungua Kama mume wake pamoja na yeye akiwa Hana maambukizi ya zinaa na Kama akiona dalili zozote zile za hatari ndio hataruhusiwa kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...