Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano, baada ya bibi kuachana na mke mdogo wa mfalme alienda kwa kijana wa kiume wa mfalme na kuona udhaifu wake kwamba anapenda sana mali.

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme ( sehemu ya tano).

1. Baada ya bibi kuachana na mke mdogo wa mfalme alienda kwa kijana wa kiume wa mfalme na kugundua kwamba anapenda sana mali. Kwa hiyo bibi akagundua namna ya kumtega ili aweze kuona mke wa pili ili aje apate ufalme na bibi apate sehemu ya kuishi na kutunzwa.

 

2. Palikuwepo na mzee mmoja alikuwa na kiwanja kikubwa cha madini mbalimbali kwa hiyo bibi alisafiri akaenda huku na kuongea na mzee kwamba kuna mtoto wa kiume wa mfalme angependa kuchimba madini pamoja nawe, basi yule Mzee aliogopa sana na kusema yeye ni nani mpaka afanye kazi na mtoto wa pekee wa kiume wa mfalme? Bibi akasema usihofu yeye ameomba,

 

3. Basi yule mzee alikuwa na mabinti wanne wazuri sana . Bibi akamwambia sheria ni kwamba ukimpatia mtoto wa kiume wa mfalme sehemu ya kuchimba ni lazima umpatie na binti mmoja wa kumliwadha na mzee akafurahi sana kuona binti yake anaolewa na mtoto wa mfalme, kwa hiyo binti akaandaliwa vizuri na kupambwa kwa ajili ya mtoto wa kiume wa mfalme.

 

4. Basi bibi alienda kwa mtoto wa kiume wa mfalme na kumwambia yote kuhusu mali na madini kutoka kwa yule mzee, mtoto wa kiume wa mfalme alifurahi sana kusikia kitu kinachoitwa madini na kusikia mali kwa hiyo siku hiyo mtoto wa kiume wa mfalme akaandamana na umati mkubwa wa watu na farasi watu wa kijiji cha yule mzee waliogopa  sana ila bibi aliwahakikishia usalama na amani pia.

 

5. Basi mtoto wa mfalme akaonyeshwa sehemu kubwa ya kuchimba akaanza kuchimba, na akapiga hema uko, ila siku ya kwanza alichoka mno alipoingia chumbani kwake alikuta binti mzuri alifurahi sana kuona jinsi alivyoandaliwa na yule mzee binti mzuri mno akalala naye na ilikuwa siku ya kubeba mimba akabeba mimba ya mapacha wa kiume na baada ya siku chache aliambiwa habari ya ujauzito wa mke wake alifurahi sana kwa sababu yule mke wa kwanza hakuwahi kuwa na mimba.

 

6. Basi bibi baada ya kuchimba kila kitu akamwacha mtoto wa kiume wa mfalme na mke mpa akaenda kwa mke mdogo wa mfalme akamwambia kila kitu na yule mama alifurahi mno.

 

Itaendelea baadae

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jamvini Main: Post File: Download PDF Views: 3257

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 ai web app     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Chemsha bongo na bongoclass

Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi.

Soma Zaidi...
Mahusiano ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake.

Soma Zaidi...
Hasara za wivu na kutokuwa wazi ( sehemu ya 2)

Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani.

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo.

Soma Zaidi...
Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi

Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi.

Soma Zaidi...
SAFARI YA MUUJIZA

Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama.

Soma Zaidi...