image

Hadithi katika kijiji cha burugo

 Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii .

 

          JIFUNZE KUHUSU UFAHAMU WA HADITHI HII KATIKA  KATIKA KIJIJI  KIMOJA  

 Kulingana na hapo juu jinsi nilivyokuelezea mwanzo kuwa hadithi inaelimisha jamii ,inaburudisha pia inakuwa inaonesha jinsi gani maisha yalivyo hivo hivo zutangalia hadithi hii kutokea sehemu moja uko kanda ya ziwa mkoani kagera wilaya ya bukoba  kijiji burugo .burugo ni kijiji kilichopo kando ya ziwa Victoria watu wa kijiji cha burugo waliishi kwa upendo tangu zamani kijiji hicho kiliongozwa na mzee mmoja aitwaye ndyamukama tangu kuanzishwa kwake . mzeee ndyamukama alitokea katika familia duni iliyotingwa na ufukara licha ya kwamba babu wa babu alikuwa chifu miaka ya uko nyuma .

 

Mzee ndyamukama aliishi karne moka .Enzi za utawala wake aliwafanya watu waishi kwa amani na raha tele.aliwafanya juu chini kuwaendeleza watu kimaisha ndani ya hicho kijiji .aliwainua wanyonge na waliokata tamaa,kwa kutumia lugha nzuri yenye ushawishi .Alichukia sana umasikini hivo alihamasisha watu kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na umasikini .Aliviona vitu vitatu kuwa ni madui wa maendeleo .ujinga ,maradhi na umasikini . Kwa kipondi hicho vijana na wazee wote walikuwa sawa kutokana na undugu alioujenga katika hicho kijiji  mzee ndyamukama alikuwa  mzalendo ,mpambanaji mashuhuri .mpenda watu na aliyediriki kujinyima mwenyewe kwa manufaa ya wengine kutokana na  upendo wa hicho kijiji Hakuishia apo tu .bali aliwatunza waliokuwa wanahitaji mahitaji mahalamu .kama wazee, walemavu,watu wasiona, wagonjwa. na wengine kibao wasio na mahitaji mahalamu .pia watu wa kijiji hicho walimuona kama nguzo ya maisha yao  .

 

Mzee ndyamukama alipenda sana maendeleo Alijiwekea malengo ya kazi zake kwa faida ya watu wote apo kijijini burugo .Ajabu iliyoje! Hakuanzia kwenye familia yake wakati wa kutoa huduma .alikuwa anawaahangaza watu katika hicho kijiji .chochote alichokipata kutokana na kujiahugulisha kwake kilikuwa kwa ajili ya kuwaendeleza watu wote katika kijijini pale burugo mzeee ndyamukama alijishusha sana ingawa alikuwa mtu maharufu sana katika hicho kijiji  .Alidiriki kuvaaa nguo za ufukara .pia alikuwa anakula chakula walichokua wanakula wanyonge na kula kwenye malazi A ya kawaida sana.licha ya kwamba ndiye alikuwa kiongozi wa kijiji  pia wanakijiji waliendelea kumueshimu na kusaidiana katika shughuli mbalimbali za kijamii 

 

Katika uongozi wake aliushangaza ulimwwngu kuona anatumia tochi kumulika mchana kweupe .Aliweka katika kichuguu kirefu kuliko vyote pale kijijini na watu wote walieshimu tochi ile kuna wakati aliwaita wasaidizi wake kuwakabidhi.tochi ile  ili wazunguke kijiji kizima kuwasaka wahalifu ilitumika pia kumulika sehemu zote uilizokuwa na giza la maendeleo licha ya bikini vingine kuwa na maendeleo kuliko kijiji cha burugo bado burugo ilitambulika sana hata kwa wageni waliotoka mbali kutokana na umaarufu wa mzeee ndyamukama.

 

Kijiji cha burugo kilikuwa na utajiri mkubwa wa mali nyingi na zenye thamani sana  kama wanyamapori ,ndege, vyanzo vya maji  dhahabu kama almasi na tanzanite .hata hivyo kijiji cha burugo kuwa na hizo mali zote wazawa hawakulitambua hilo kwani kama ujuavyo misemo ya wahenga penye miti hapana wajenzi.walikuwa wanakanyaga juu ya mali bila kutambua , sawa  na msemo usemao anacho lakini hakioni. Licha ya kuwa na kiongozi mwenye maono bahadhi ya wanaburugo hawakuwathamini wenzao .waliotoka msaada kwa watu wa vijiji vya mbali ,walidanganya kwa kujiona kuwa wanafanya mambo makubwa ,lakini jitihada zao zote zlishia kuwapigia wageni makofi waowakaribisha watu hawa wanaweza kufananisha na baluni liloishiwa upepo ukiwa bado angani 

 

Mzee ndyamukama alijitahidi sana kuendelea na juhudi zake .lakini ulifika wakati utawala wake ukakata kuangushwa na msaidizi wake .mzee ndyamukama alitafakari mala mbilimbili lakini hakujua cha kufanya hatimaye alijisemea moyoni hakuna marefu yasiokuwa na ncha ,wakati huo alionekana kama wa kuishiwa nguvu kutokana na kuzidiwa na kuvamiwa na vijiji vingine kwa eshima na busara alitisha mkutano wa hadhara .katika mkutano huo aliongea mambo mengi ya kuwaasa wanakijiji wake .maneno yake yaliwachoma moyoni bahadhi ya watu wake alikuwa anawaongoza bahada ya maneno yale alitangaza uamuzi wa kupumzika uongozi wa kijiji na kubaki kuwa raia wa kawaida .uamuzi huo ulipokelewa kwa hisia tofautitofauti .watu wengi walisitikika ila japo wengine walishangilia .

 

Walichaguliwa viongozi wengine kutoka katika familia nyingine kukiongoza kijiji kile cha burugo .viongozi wote walichaguliwa ila hawakuweza kufuata nyayo za mzee ndyamukama wakati huu, mzee ndyamukama alikuwa akipumzika nyumbani kwake lakini hakuacha kishirikiana na majirani zake katika shughuli mbalimbali za uzaliahaji mali.wakati mwingine walimuendea ili kupata ushauri .maybe,bila iyana aliwaahauri kulingana na mahitaji.

 

Utaratibu wakurishana uongozi wa kijiji kile uliendelea miaka kadhaa waliitwa watu mbalimbali na kukaeishwa sehemu moja kisha walianza kuwajadili kisha mpaka apatikane wankurisithishwa kwakuwa ulikuwa utaratibu wa hicho kijiji kupokezana kijiti .wakati wote ,walijaribu kumtafuta mwenye uelekeo ili apatikane wa kufuata nyayo za mzee ndyamukama.

 

Tangu mzeee ndyamukama achie uongozi waliokata viongozi kadhaa kadhaa .kuna kipindi mzee ndyamukama alitumika kama mtoa ushauri .kila . Kiongozi alikuja na mbinu zake za kiutawala .hali ya kijiji ilibadilika kila kila utawala ulipobadilika .msemo wa kwamba kila "mwanadamu mavumbini,"ulidhirika mda ule bahada ya mzee ndyamukama kukata roho bahadhi ya watu walikata tamaa bahada ya kuondokewa na mzee wao ndyamukama kubaki kuchanganyikiwa .waliweza kuongea bila kufahamu wanachongea .kwao aliekuwa akitaja namna kumi ,alikuwa sahii,tano sawa na hata yule wa sifuri alijikuta anapata .

 

Siku moja katika uchaguzi wa viongozi katika kijiji cha burugo walijitokeza watu wengi kugombea nafasi hio alioiacha mzee ndyamukama .majina kadhaa yalipendekezwa katika kinyang'anyiro hicho miongoni mwao .alikuwemo kijana mmoja kutoka katika familia duni jina lake aliitwa   peter .wengi hawakujua kama angeweza kushika atamu kama mzee ndyamukama waliemzoea uko kipindi cha nyuma.fikira hii ilitokana na kwamba watu wengi hawakumfahamu na yeye mwanzoni hakuonesha nia ya kugombea mapema ata hivo peter hakuwa mtu wa mchezo mchezo .hakuwa na mzaha katika kazi pia na yeye alikuwa na msimamo mkali kuhusu jambo hilo .Hakuwa na lugha ya kubembeleza hasa kuhusiana na kufanya kazi kwa juhudi .Alitamka waziwazi kuwa  ikiwa angepewa fursa kuwa meithi,angeweza kusimamia kijiji na kuhakikisha watu wanafanya kazi  kama ilivyokuwa mwanzo ususani kipindi cha utawala wa mzeee ndyamukama  ulikuwa ukweli usiopingika kuwa historia Aya mzee ndyamukama ikuwapo na bado itaendelea kuwepo  na kukumbuka daima kutoka kwa mababu adi kwa vitukuu .mzee ndyamukama aliendelea kuishi ,japokuwa alikuwa amekufa maneno yake yalizungumzwa kila mahali hapo kijijini ata nje ya kijiji .

 

Kama wasemavyo wahenga  ,Umdhaniaye ndiye kumbe. Siye "kijiji kilikaa kimiya bahada ya wazee wa kijiji kumtangaza peter kuwa kiongozi wa kijiji bahadhi ya watu walimuona kama mwendawazimu vile.wengine walimuona kama malaika kashushwa na muumba kunusuru kijiji kile .wengine wengine walisikika wakisema upele umempata mkunaji ,kila mmoja alikuwa na lake  la kusema .jasiri haachi asili .peter ,katika mkutano wake wa kwanza wa hadhara ,alitangaza vita dhidhi ya wavivu wote wasiopenda kufanya kazi .Alisema kuwa lazima arudishe eshima ya kijiji .Alisisitiza kupambana na madui watatu aliowatangaza mzee ndyamukama enzi za utawala wake .Hivyo alihamasisha wanakijiji wote kupata elimu bora  ili kufuta ujinga .Alijenga vituo vya kutolea huduma kama.shure,zahanati,na kuboresha bahadhi ya uduma za kijamii alifanya hayo yote ili kuondokana na umasikini kwa kuwa mgaaga na upwa hali wali mkavu .

 

Apo apo wanakijiji walianza kusema maji hufuata mkondo .wanafikika wakubwa kuwa wadogo ,wake kwa waume ,wafanyakazi na waaiofanyakazi walikuwa kama watu walioamshwa usingizini ,walifanya kazi kwa juhudi na ndani ya mda mfupi,hali ya kijijini ilibadilika sana watu wa vijiji vya jirani na vya mbali walianza kukieshimu kijiji cha burugo walianza kuingia kwa adabu kama enzi za mzee ndyamukama  jina la peter likavuma kama jina la mzee ndyamukama.hapo ndo tunaona maendeleo ya kijiji hicho moka sahivi kinaendelea vizuri maisha ya wananchi yamebadilika sana .

 

              Kwahiyo inatubidi viongozi wanaochaguliwa na wananchi inabidi watende kazi zao kwa ufasaha ili waweze kuijenga nchi yao vizuri kama tunavyoiona nchi yeti ya tanzania inaongozwa na mama samia inabidi tuwe tunaiga na pia tuwasikilize au zukachukuwe ushauri bahadhi ya maraisi wastahafu ili tuweze kuondokana na shida zote hizi 

                         aliekuandalia makala aya ni mimi machius kutoka Bongoclass. 

 

       





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jamvini Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1620


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

SAFARI YA MUUJIZA sehemu ya tatu
Post hii inahusu Zaidi hadithi ya safari ya muujiza ambapo ya Mungu mengi anaenda kwao na kuomba kufahamu history yake ili afahamu kuhusu wazazi weo walipo na ndugu zao walipo. Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya. Soma Zaidi...

Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu. Soma Zaidi...

Hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na Soma Zaidi...

USALITI (sehemu ya tatu)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi. Soma Zaidi...

USALITI (sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo Soma Zaidi...

Mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake. Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha Soma Zaidi...

Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini. Soma Zaidi...

Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 3)
Posti hii inahusu zaidi hasara za kuwa na wivu na kutokuwa wazi, sehemu hii inahusu zaidi maendeleo ya Lisa shuleni yanakuwa mabaya zaidi na lina anaendelea kumtunzia siri lengo lake lina ni kuendelea kuwa wa kwanza darasani. Soma Zaidi...

WAKATI WA KUFUMBUKA
Post hii ni mwendelezo wa hadithi inayohusu Kufumbuka ambapo , John anaonekana kama sio mtoto wa Mzee maganga kwa sababu na miungu imekili kwa sababu chakula chote kimeliwa na kuisha. Soma Zaidi...

Hadithi za alif lela u lela
Haya ni masimulizi ya Hadithi za alif lela u lela Soma Zaidi...