Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme (sehemu ya nne)


image


Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne ni pale bibi anawachanganya kwa maneno yake yaani mke wa kwanza anaambiwa aandae malkia na mke mdogo atafute njia za kufanya kijana wake kuwa mfalme.


Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne.

1. Basi siku ya maongezi ikafika kati ya bibi na mke wa mdogo wa mfalme,bibi akamsalimia vizuri akampa sifa zote ila akamwambia kwamba wafanye utaratibu wa kumshauri kijana wa kiume wa mfalme awe na mke wa pili ili aweze kupata ufalme wa nane kwanza na mke huyu ambaye ni ndugu yake na kadri ya sheria hataweza kupata ufalme.

 

2. Basi bibi na yule mke mdogo wa mfalme wakamwita yule kijana na kumpasha habari ya kila kitu kinachoendelea ila kijana akasema siwezi kumwacha mke wangu ili niwe mfalme bora nikakosa ufalme ila nikaishi na mpenzi wangu, mama yake baada ya kusikia hivyo akahisi kuchanganyikiwa na siku zinaenda kijana hana mda mpaka mama yake akajuta na kusema bora ningewazaa watoto wangu wakiwa wawili.

 

3. Basi bibi akamwambia Mama usihofu kila kitu kitakuwa sawa nihaidi utanipa nini ,Mama akamwambia nitakutunza mpaka utakapofariki, akasema iwapo yeye atafariki ataacha ujumbe wa bibi kutunzwa maisha yake yote, bibi akasema tuandikiane wakaandikiana bibi akaanza mbinu za kuhakikisha kuwa ufalme unabaki mikononi mwa uzao wa mke mdogo.

 

4. Baada ya bibi kutoka kwa yule mke mdogo akaenda kwa yule mke mkubwa ambaye alimwambia aandae binti mkubwa kwa ajili ya kupata umalkia, basi bibi akaenda kwa ndugu wa mfalme akamshawishi kijana wa ndugu wa mfalme akamwambia , mfalme ana mpango wa kugawa mali kwa watoto wake ila mali kubwa zitaenda kwa binti wa kwanza na kwa mme wake akamwambia kijana kwa nini usimtongoze yule binti na ukampa mapenzi ya kweli ili upate zawadi nyingi na kuishi na binti wa mfalme.

 

5. Kijana akafanya hivyo na akafanikiwa kumpa binti yule mimba na binti akaogopa kuishi kwa mfalme akiwa na mimba kwa sababu siku zile wasichana waliobobea mimba kwa waliuawa na yule kijana akamwoa mtoto wa mfalme . Kwa hiyo sifa za kuwa malkia zikaishia hapo . Bibi baada ya kufanikiwa mbinu hiyo akaenda kwa mke mdogo na kutoa taarifa mke mdogo alifurahi sana ila akaendelea kumwacha bibi akae kwa wake wenza ili kuleta habari zaidi, basi bibi akapanga kukutana na mke mdogo kwa maongezi zaidi, 

itaendelea baadae

 

 

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    2 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    3 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme (sehemu ya nne)
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne ni pale bibi anawachanganya kwa maneno yake yaani mke wa kwanza anaambiwa aandae malkia na mke mdogo atafute njia za kufanya kijana wake kuwa mfalme. Soma Zaidi...