Hadithi ya Binti mfalme

Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na

Hadithi ya Binti mfalme.

1. Hapo zamani za kale palikuwepo na mfalme mmoja aliitwa Gwanta , mfalme alioa wanawake watano ila kati ya wanawake wote hakuna aliyefanikiwa kupata mtoto wa kiume, hali hii ilimuumiza sana mfalme na kufikilia mambo mengi hasa mtoto wa kuridhi Mali yake, katika kuongea na washauri wake jinsi anavyoumia kwa sababu ya kutopata mtoto wa kiume waliamua kumpatia mfalme Binti mzuri Sana wa miaka kumi na mbili Ili aweze kumfariji, kwa hiyo mfalme aliishi na Binti huyo kwa miaka mitano na hatimaye akabeba mimba.

 

2. Kitendo cha mfalme kuishi na yule mke mdogo kilifanya mfalme awasahau wanawake wengine na pia alikuwa anampenda sana yule mke mdogo na yule mke alikuwa anamtii mfalme na kufanya kila kitu alichokipenda na pia yule mke mdogo alikuwa na uso mzuri na WA kuvutia sana kwa macho. Kwa hiyo wale wanawake watano wa mfalme wakimchukia sana yule mke mdogo isipokuwa mke wa tatu aliyeitwa Janka alimpenda kisiri Siri na kumwambia yule mke mdogo kila kitu wanachopanga juu yake.

 

3. Siku Moja baada ya mimba kukua na kuonekana kwa kila mmoja wale wake wenza wakaenda kwa mganga na kwa mizimu yao Ili kujua kuhusu mimba iliyobebwa ni mtoto gani , kwanza mganga akawaambia kuwa ni mtoto wa kiume na WA kike pia na mizimu ikatoa jibu hilo hilo,kwa hiyo walipofahamu hayo wakatafuta mbinu za kumwangamiza, yule Janka mke wa tatu akamwambia kimbia Ili usiuawe na kweli yule Binti akakimbilia mbali kabisa mbugani na huku akakutana na bibi aliyekuwa na kilimo cha njugu mawe, yule mke akamwekeza kila kitu na yule bibi akaamua kumficha.

 

4. Baada ya mfalme kutomwona mke wake alilia sana na kuita mkutano kwamba atakayemwona yule mke mdogo atapewa nusu ya ufalme wake, watu wakaanza safari kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kumtafuta, basi Kuna waliofikia kwa yule bibi wakaeleza kila kitu na ahadi za mfalme,bibi akawajibu sijamwona lengo la bibi ni kusubiri yule mke mdogo wa mfalme ajifungue Ili aweze kupeleka mtoto na mke mdogo wa mfalme na alijua wazi kuwa atapata zawadi kubwa na maisha mazuri.

 

5. Basi siku za kujifungua zikafika yule bibi alikuwa mtaalamu na mkunga akamzalisha yule mke mdogo wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha wa kwanza wa kiume na WA pili wa kike , mke mdogo wa mfalme alifurahi sana ila kwa sababu bibi yule alipenda sana sifa alimwambia mke mdogo wa mfalme kwamba wapeleke mtoto wa kiume tu wa kike akae na bibi na wakafanikiwa kufanya hivyo, basi bibi akakimbia kwa mfalme akatoa habari kwamba mke mdogo wa mfalme amepatikana na amejifungua mtoto wa kiume. 

 

6. Mfalme baada ya kusikia habari hizo alifurahi sana mpaka akazimia baadae alizinduka akatuma viongozi wake wamfuate yule mke mdogo,walimleta na kuimba njia nzima wale wake wenza waliumia sana isipokuwa yule rafiki yake , basi bibi akapewa zawadi nyingi na pia akaamuliwa Aishi na mfalme alikataa kwa sababu ya kuwepo kwa yule mtoto wa kike aliyebaki kwake, kwa hiyo bibi akapewa zawadi nyingi sana na akajengewa kwake na wakaishi vizuri na yule mtoto wa kike aliyebaki kwake.

 

 

 

7. Baada ya miaka na miaka bibi aliendelea kutunza yule Binti akakuwa akawa dada mzima mzuri Sana kwa umbo na sura ila alimwuliza bibi kuhusu history yake ila bibi hakumwambia basi na yule kijana wa kiume wa mfalme akakua akafikia wakati wa kuoa ila alimwambia mfalme baba nioze msichana wa kwa bibi kwa sababu nampenda sana,basi mfalme akatuma ujumbe kwa bibi , yule bibi kusikia hivyo alizimia na kuwa mgonjwa sana kwa hiyo yule dada akamuuguuza bibi yake ila bibi alipoona hali ni mbaya akapaswa kumwambia mjukuu wake story yote,Binti akaumia sana kusikia hivyo.

 

8. Kadri siku zinavyoonda ndivyo yule kijana akaendelea kumpenda Binti Ila Binti anakataa kuolewa naye na Mama wa watoto alikuwa anapinga sana , ndipo yule mvulana akashauliwa kuoa Binti mwingine ila alikataa kabisa alisema anampenda sana Binti wa kwa bibi. Basi siku Moja mvulana alitunga wimbo i akaanza kumwimbia yule Binti alisema.

 

9. Dada nakupenda sana kushindwa kukupata Bora nife, kujiua ni kazi rahisi kusema ukweli usipokubali nitajiua, 

 

10, na msichana akajibu, mimi nakupenda sana na ningependa kuolewa na kijana wa mfalme ila mimi na wewe ni ndugu mama alituzaa wawili mimi na wewe kwa kuwa mfalme alihitaji sana mtoto wa kiume mimi nilibakizwa kwa bibi wewe ukapelekwa kwa mfalme.

 

11. Baada ya yule kijana wa kiume wa mfalme kusikia hivyo aliumia sana na kwenda kumwambia mama yake mama naye akapanic sana akafikilia kuwa inshu hii ikifika kwa mfalme na watu wote atapata aibu kwa hivyo yule mama akapanga mbinu za kumtorosha mbali mtoto wa kike na yule Bibi  mbali Ili yule kijana asiweze kuwaona tena na apoteze Ile kumbukumbu ya yule dada ila kijana alimpenda sana na pia kijana hakutoa Siri hiyo kwa mfalme au kwa mtu yeyote ila kijana alisema hata kama ni ndugu mpaka nimuone,basi yule mke wa mfalme akawatorosha akawapeleka mbali kweli ila kijana akaamua kuwatafuta kila sehemu. 

 

Itaendelea

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jamvini Main: Burudani File: Download PDF Views 2915

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tano)

Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya Nimlaumu nani ambapo juma anapanga na madaktari wanaopima DNA ili kuweza kutambua kwamba mtu mimba ni ya kwake na sio ya Frank kwa hiyo tuendelee kusikiliza mpaka tutakapoona mimba itakuwa ya Frank au juma.

Soma Zaidi...
USALITI (sehemu ya tatu)

Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi.

Soma Zaidi...
Hadithi katika kijiji cha burugo

Β Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii .

Soma Zaidi...
Chemsha bongo na bongoclass

Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi.

Soma Zaidi...
USALITI (sehemu ya kwanza)

Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI part 1

Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita

Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya.

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI (sehemu ya nne)

Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha.

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu, kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu alichukua ule mkate akawapstia watoto wa yule mama wakiwa wanatoka shule kwa hiyo tutaona kilichotokea kwa wale watoto.

Soma Zaidi...
USALITI (sehemu ya pili)

Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya Usaliti kati ya Rhoda na Moses ambapo Moses anampenda sana Rhoda na wakati wa kuoa umefika ila akagikilia kwamba akimuoa Rhoda inawezekana wasipate watoto kwa sababu ya mimba ambazo Rhoda alikuwa anatoa mara kwa mara.

Soma Zaidi...