Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, baada ya kijana wa kiume wa binti mfalme kuoa yule ndugu yake baba anafanya sherehe kubwa na wake wenza wamepata habari kwamba kijana wa kiume wa mfalme ameoa ndugu yake wakaamuru kunyamaza il
1. Kama tulivyomalizia kwenye sehemu ya pili pale mama wa kijana wa kiume wa mfalme alitaka kumuua binti na bibi ili kupoteza ushahidi ila kijana huyo wa mfalme aliwahi akawaokoa na kumwona kipenzi cha moyo wake na kumchukua nyumbani kama mke wake ila mama hakukubaliana naye ila mfalme kwa kuwa alikuwa anampenda kijana wake akisikiliza kila kitu alichotaka na akaamua kufanya sherehe kubwa na ya kifahari.
2 . Na yule bibi kwa kuwa alipenda sana umaarufu na maisha mazuri alijisalimisha kwa wake wenza na akatoa siri zote za yule mke mdogo wa mfalme, wale wake wenza walifurahi sana kusikia habari hiyo na wakapata sehemu ya kumwaibisha adui yao kwa sababu yule mke mdogo wa mfalme alikuwa ni kama kizuizi kwao na mfalme, basi wakapanga njama na kutunza siri ili siku ya kumwapisha mfalme siri itobolewe na kujana wa kiume wa mfalme hasiweze kupata ufalme.
3. Katika wakati ule palikuwepo na sheria moja kwamba ili mtu aje kuwa mfalme ni lazima awe ameoa kwenye ukoo ambao hawana undugu hata kidogo ili kuepuka hali ya ufalme kugawanyika kwa hiyo walitaka ufalme ubaki ndani, au kama kwenye familia ya kifalme hakuna mtoto wa kiume wa kurithi ufalme au yupo ila hana sifa za kuwa mfalme mtoto wa kike anaweza kuwa malkia ila mme wake atoke sehemu tofauti na ile sehemu na hasiweze na undugu wowote na familia ya kifalme iwe kati ya ndugu wa wake wenza yaani pasiwepo na undugu hata chembe.
4. Katika maandalizi yote hayo mama wa kijana wa kiume wa mfalme aliona kwamba mwanae hawezi kupata ufalme kwa sababu aliona bibi yupo pale akiwa na ushahidi wote na yuko kati ya maadui zake akapata shida sana akawaza mpaka akakonda , kwa kuwa bibi alikuwa mnafiki na mpenda sifa aliamua kumwita yule mke wa mfalme kwa siri akamwambia kuwa kwamba kwa sasa mwanao hawezi kupata ufalme sasa cha kufanya ni kuhakikisha kuwa tunafanya mbinu ili kijana aweze kuachana na yule binti .
5. Kwa kuwa yule Mke wa mfalme alikuwa kwenye hali ngumu akamuuliza bibi tufanye je? Bibi akasema nitakwambia cha kufanya baada ya siku chache, kisha bibi akaenda kwa yule mke wa kwanza wa mfalme akasema andaa binti yako ili yule kijana wa kiume wa mfalme hasipopata ufalme huyu atakuwa malkia. Baadae siku mbili zinafika bibi akaenda kuonana na mke mdogo wa mfalme kwa ajili ya maongezi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mtihani unafika ila Jackie hakujiandaa alishutuliwa na marafiki zake baada ya kuona mwenendo wake haueleweki.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya.
Soma Zaidi...Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama.
Soma Zaidi...Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano, baada ya bibi kuachana na mke mdogo wa mfalme alienda kwa kijana wa kiume wa mfalme na kuona udhaifu wake kwamba anapenda sana mali.
Soma Zaidi...Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku
Soma Zaidi...