TIBA YA MINYOO

TIBA YA MINYOO
Moja katika sifa za minyoo ni kuwa wanatibika kwa urahisi pindi mgonjwa akipewa dawa husika. Minyoo hawa wanauliwa kwa dawa, kisha wanatolewa nje ya mwili. Ni mara chache sana minyoo hawa wanavamia sehemu nyingine za mwili na hivyo tiba sahihi ni kufanyiwa upasuaji.

Tiba ya minyoo hawa pia inategemea ni aina gani ya minyoo ambao mgonjwa anao. Kwani kila aina ya minyoo hawa ina sifa zake na hivyo dawa zao zinaweza kutofautiana. Mgonjwa asikurupuke kwenda duka la madawa kununua dawa za minyoo bila ya kujua aina za minyoo alio nao.

Kwa mfano:-
1.minyoo aina ya tapeworm wanaweza kutibika kwa vidonge kama praziquantel (biltricide)
2.Minyoo aina ya roundworm wanaweza kutibika kwa mebendazole (vermox, emverm) na albendazole (albenza).

Ni vyema mgonjwa kwenda kituo cha afya akaonane na daktari ili aweze kumthibitishia tiba inayofanana na tatizo lake.