NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO
Kwa kuwa tumekwisha kuona namna ambavyo minyoo huenezwa, hivyo basi ni rahisi sasa kutaja namna ya kubambana na minyoo. Njia hizo ni kama :-
1.usile chakula, nyama ana samaki ambaye hajapikwa vyema, ama kula nyama mbichi ama isiyoiva
2.Epuka kugusagusa nyama unapoandaa chakula chako, tenganisha nyama kivyake na vyakula vingine wakati unapoandaa kupika.
3.Safisha vyema vyembo ambavyo vimegusa nyama ambayo haikupikwa
4.Usile mimea ambayo inaishi ndani ya maji yabaridi
5.Usitembee miguu wazi kwenye maeneo machafu ambayo yana kinyesi
6.Safisha vyema kinyesi cha wanyama.
7.Hakikisha unapika vizuri nyama mpaka uhakikishe imewiva vyema,
8.Wanya kung’ata kucha ama kunyonya vidole
9.Hakikisha unaosha kila unachokila kwa maji yaliyo safi na salama.
10.Usafi wa mwili, mavazi na mazingira ni muhimu kwa ajili ya kupambana na minyoo.
11.Kuwacha kabisa kula udongo