VIPIMO VYA MINYOO

VIPIMO VYA MINYOO
Haitoshelezi kuwa na dalili pekee ukathibitisha kuwa una minyoo. Itahitajika uende hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi. Kuna aina tano za vipimo vya kupima minyoo kama vile:-

1.kupima kinyesi kama kina minyoo au mazalia ya minyoo (fecal test)

2.Kumulika utumbo mkubwa (colonoscopy) hiki ni kifaa chenye kamera ambacho kinaingizwa kwenye njia ya haja kubwa, ili kumulika utumbo mkubwa kama kuna minyoo

3.Kupima damu (blood test)

4.Kuchukuwa picha za mwili kwa kutumia vifaa kama X-ray, MRI na CT scan.
v5.Kupima kwa kutumia tep (tape test). unapewa kaji tep (kama kamkanda kadogo) kisha unakaweka kwenye tundu ya haja kubwa na mara nyingi wakati wa asubuhi unapoamka. Kisha katep haka kanawekwa kwenye hadubuni (microscpe) na kuchunguza uwepo wa minyoo aina ya pinworm au mayai yao.