Mda wa kufanya tendo la ndoa baada ya kujifungua

Posti hii inahusu zaidi mda ambao mama anapaswa kukaa bila kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua.

Mda wa kufanya tendo la ndoa baada ya kujifungua.

1. Hili ni tatizo ambalo linawapata wanawake wengi ambapo hawajui ni mda gani na wakati gani waanze kufanya tendo la ndoa baada ya kujifungua, wengine wanakaa mda mrefu wengine mfupi ila kadri ya wataalamu wanashuri kuwa Mama anaweza kuanza kufanya tendo la ndoa baada ya wiki sita au siku arobaini na mbili tangia siku aliyojifungua, tendo la ndoa linakatazwa lisifanyike kwa Mama ndani ya siku arobaini na mbili baada ya kujifungua kwa sababu zifuatazo.

 

 

2.wakati wa kujifungua mwili wa Mama unakuwa uko tofauti kwa hiyo viungo vya Mama vinapaswa kujirudisha katika hali ya kawaida kwa sababu wakati wa kubeba mimba na kukua Kuna mabadiliko mengi kwenye mwili wa Mama kwa hiyo Mama anapojifungua anapaswa kurudi kwenye hali ya kawaida kadri ya wataalamu hali ya kawaida walau ni siku arobaini na mbili, kwa sababu ya utofauti wetu wakati wa kujifungua ni vizuri kuwasikiliza wataalamu wa afya Ili kama pametokea tatizo wakati wa kujifungua siku zinaweza kuongezewa .

 

 

3. Pia Mama anapojifungua Kuna bado uchafu unakuwa unatokea taratibu, kwa hiyo ikitokea mwanamke akafanya tendo la ndoa kabla ya siku zilizopangwa kwa sababu ya uchafu unaotoka anaweza kupata maambukizi, wote wawili ambao ni baba na Mama kwa hiyo kusubiri ni muhimu.

 

 

4. Na pengine kwa sababu ya kuwepo kwa ujauzito Kuna kipindi homoni zina badirisha mwili wa Mama ambapo Mama anakuwa mkavu kabisa kwenye via vya uzazi hali inayosababisha kuchubuka wakati wa kujamiiana, kwa hiyo ni vizuri kusubiri mpaka Mama apone kabisa.

 

5. Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kujua hilo kwa sababu wakikosea kuwakumbusha waume zao wanaweza kupata matatizo mbalimbali na wanaume wanapaswa kuwa Linda na kuwasaidia wake zao Ili siku za kujamiiana zifike.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/21/Saturday - 10:25:17 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 7889


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-