Wanaopasawa kutumia PEP

PEP Ni dawa ambazo utumiwa na watu wanaojamiiana na watu wenye virus vya ukimwi ila wenyewe hawawezi kupata kwa sababu ya kutumia dawa hizo.

Wanaopasawa kutumia PEP.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua maana ya PEP kwa kitaalamu ni post exposure prophylaxis kama nilivyotangulia kusema kuwa ni dawa ambazo utumiwa na wale wanaojamiiana na watu wenye maambukizi ya ukimwi na hawawezi kupata ugonjwa wa ukimwi lakina dawa hizi zinatolewa hospital hasa kwenye vituo vya kuhudumiwa wagonjwa wenye maambukizi ya ukimwi, unaenda pale unaeleza Nia Yako na unapatiwa. Ili kupunguza ongezeko la virus vya ukimwi wafuatao wanapaswa kutumia dawa hizo.

 

1.wanaofanya biashara ya ngono.

Kwa wale wanaofanya kazi hizi ni vizuri kutumia dawa hizi kwa sababu ya kukutana na watu wengi mbalimbali na wenye magonjwa mbalimbali Ili kuweza kupunguza kuendelea kuwepo au kusambaa kwa ugonjwa huu na watu Hawa wanapaswa kuwasiliana na watoa huduma kwenye vituo hivi na watapata msaada.

 

2. Wanaume wanaojamiiana na wanaume wenzao.

Na Hawa ni watu walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu wa ukimwi kwa sababu Leo anejamiiana na mwanaume huyu kesho na mwingine kesho kutwa na mke wake na hao aliojamiiana nao pia na wenyewe Wana wapenzi wao hali hii usababisha kuendelea kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi, kwa hiyo Ili kuepuka kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa ukimwi ni lazima kufatilia dawa mapema Ili kuweza kuepuka kupata ugonjwa.

 

3. Watu wanaovuta madawa ya kulevya kwa kutumia sindano.

Kwa kawaida tunajua watu Hawa nao wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa ukimwi kwa sababu sindano Moja inaweza kutumiwa na watu zaidi ya kumi na huwezi kujua ni nani mwenye maambukizi kwa hiyo ni vizuri kabisa kutumia dawa Ili kuepuka hatari ya kuwaambukiza wengine.

 

4. Pia watoto ambao wameanza kubarehe na hawatulii na wenyewe kama tunaona wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa ukimwi wapatiwe Ili pale wakitulia waache, kwa kufanya hivyo ni kuwasaidia Ili katika umri mdogo wasipatwe na maambukizi na kukatisha ndoto zao.

 

5. Kwa hiyo hizi dawa zinapatikana hospital na unaenda unajieleza na unapatiwa hata ukijamiiana na mtu mwenye maambukizi huwezi kupata ila uliamua kuacha kazi ambayo inakuingiza kwenye hatari ya kupata maambukizi unaweza kuacha na kuendelea na maisha ya kawaida, kwa hiyo uaminifu wa kutumia dawa ni lazima pamoja na kufuata mashart.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/22/Sunday - 07:33:15 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1384


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-