Magonjwa madogo madogo kwa Mama wajawazito.

Posti hii inahusu zaidi magonjwa madogo madogo kwa akina Mama wajawazito, ni magonjwa ambayo hayawezi kupelekea kupoteza maisha kwa Mama mjamzito, magonjwa haya upotea ikiwa Mama atajifungua.

Magonjwa madogo madogo kwa Mama wajawazito.

1. Kizungu Zungu na kutapika.

Ni mojawapo ya magonjwa kwa mama wajawazito ambayo hayawezi kupoteza maisha ya mama kwa hiyo hali huu umpata Mama akiwa na wiki nne mpaka kumi na sita, hasa hasa hali hiii utokea wakati wa asubuhi kwa akina Mama wengi na kwa wengine utokea mda wote, hali hii usababishwa na homoni za mimba ambazo ni progesterone, oestrogen na chorionic gonadotropin .

 

2. Na kwa wakati mwingine harufu ya chakula usababisha mama kubwa na kichefuchefu na kutapika kwa hiyo  wauguzi na wataalam wa afya wanapaswa  kuongea na Mama ili kuona hali huu ni ya kawaida kabisa na akina Mama wanapaswa kuambiwa ukweli kabisa na kuepuka woga usio na Maana kuhusu hali hii ya kuhisi kichefuchefu na kutapika.

 

3. Kuhisi maumivu kwenye kiuno na kwenye mgongo, hali huu uwapata akina Mama wakati wa ujauzito kwa sababu ya uzito wa mtoto anapoongezeka na anapobadilika mkao kwa hiyo Mama uhisi maumivu na pengine miguu kufa ganzi  kwa hiyo Mama anapaswa kufanya mazoezi, kunyoosha miguu kwa sentimita ishilini na tano, pia anaweza kutumia dawa ya vitamini B complex na calcium na pia Mazoezi ni lazima kwa kina Mama wajawazito.

 

4. Pia Mama wajawazito huwa wanakojoa mara kwa mara kwa sababu kibofu cha mkojo na uterus vimekaribiana sana kwa hiyo mtoto anakandamiza kibofu cha mkojo na kila mkojo unaoingia kwenye kibofu utolewa mara moja kwa hiyo Mama uonekane anakojoa Mara kwa Mara, pia kwa sababu ya mabadiliko ya kimwili kwa Mama mjamzito pengine uhisi kiu na kunywa maji mengi na baadae kuokoa sana, kwa hiyo wajawazito wanapaswa kuelewa kubwa huu si ugonjwa ila ni hali inayotokea na baadae ulisha baada ya kujifungua.

 

5. Na pia wajawazito wana hali ya kusikia ganzi kwenye mikono na vidole na pia kusikia vitu vinachoma kama vile pini na sindano huu ni kwa sababu ya maji maji ambayo kwenye nevu kwa hiyo Mama anapaswa kuweka mikono yake kwenye mito na kuvaa nguo raini wakati wa usiku, hali huu kwa wajawazito ni kawaida na wasiogope na uisha tu baada ya kujifungua, na wakati mwingine wajawazito ushindwa kutulia kwa sababu ya kukua kila siku kwa mtoto aliyeko tumboni.

 

6.Kuongezeka kwa kiasi au spidi ya damu kwenye uterus usababisha mtoto kutembea sana  ambapo hali hii usababisha mama kulala sana na kuwahi kusinzia mapema wakati wa jioni, pia Mama  kwa wakati mwingine uhisi wasiwasi pindi anapofikilia kujifungua kwa wakati huu Mama uhitaji mda mwingi wa kupata ushauri na kufarijiwa kuona kubwa ni hali ya kawaida. Kubadilika kwa homoni pia usababisha Mama kuwa mzito na kupata mawazo mengi sana. Kwa hiyo wauguzi wanapaswa kumwambia Mama kubwa akijifungua hali utapotea tu.

 

7. Tunaona wazi kuwa akina Mama wakati wa ujauzito kuna mabadiliko mengi ambayo utokea kwa hiyo jamii inayowazunguka kuanzia kwa mme, watoto, ndugu na jamii kwa ujumla kuwavumilia wajawazito na kuwapa ushirikiano wa hali na mali kuna pengine wahisi kukwazika waone kuwa ni hali ya kawaida ambayo ujitokeza na kuanza kuwaonyesha upendo kuwadhamini na kuwaelewa kwa kipindi chote cha ujauzito kwa hiyo kwa wale wanaowatesa wahawazito na kuonyesha kuwa maudhi yanayotokea kwao ni kuwa wanajifanyisha wapigwe marufuku na wapewe elimu kuhusu wajawazito wakati wa ujauzito.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/12/Wednesday - 04:55:31 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1423


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Sababu za kuongezeka uzito wa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuongezeka uzito kwa wajawazito, Mara nyingi Mama akibeba mimba uongezeka uzito kutoka wiki ya Kwanza mpaka wiki ya mwisho ya kujifungua. Soma Zaidi...

Hatua Saba za kutibu au kuepuka uvimbe kwenye kizazi
Posti hii inahusu zaidi hatua ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kutibu uvimbe au kwa kitaalamu huitwa fibroids. Hizi hatua zikitumika uweza kusaidia kupunguza kiwango cha kupata au kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi. Soma Zaidi...

Namna ya kutibu ugumba kwa Mwanaume.
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutibu tatizo la ugumba kwa Mwanaume, ni njia ambazo utumiwa na wataalam mbalimbali Ili kuweza kutibu tatizo la ugumba kwa wanaume. Soma Zaidi...

Mimi naumwa na tumbo chini ya kitovu upande wa kulia, ninapotok kushiriki tendo la ndoa ndonapata maumivu zaid pia nawashwa sehemu za siri itakuwa shida ni nin?
Maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa yanaweza kuwa ni dalili ya maradhi fulani, ama shida kwenye mfumo w uzazi. PID na UTI hutuhumiwa kuwa ni katika sababu hizo. Ila zipo nyingine nyingi tu. Kama ina hali hii vyema ukafika kituo cha afya Soma Zaidi...

Dalili za mimba ya watoto mapacha
Makala hii itakwenda kukupa dalili ambazo zinaonyesha kuwa mimba ni ya mapacha. Dalili hizi zitahitajika kuthibitishwa na kipimo cha daktari ili kujuwa kuwa ni kweli. Soma Zaidi...

Samahani naomba kuhuliza je unaweza kutokwa na maji maji ambayoa ayana rangi Wala harufu Ni dalili gani kwa mimba ya mwezi mmoja
ukiwa na ujauzito unaweza kuona mabadiliko mengi katika mwili wako yakiwemo kutokwa na majimaji. je majimaji haya yana dalili gani kwenye ujauzito? Soma Zaidi...

Mbinu za kuwakinga watoto na saratani.
Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo tunaweza kuzitumia ili kuwakinga watoto dhidi ya saratani, kama tulivyotangulia kusema kwamba saratani ya watoto mara nyingi Usababishwa na akina Mama hasa kwa sababu ya mtindo wa maisha wakati wa ujauzito kwa hiyo tun Soma Zaidi...

Dalili za tezi dume na sababu za kutokea kwa tezi dume.
dalili za ugonjwa wa tezi dume, na sababu za kutokea kwa tezi dume, maana ya tezi dume na athari zake Soma Zaidi...

Ijue kazi ya homoni ya HCG wakati wa kupima mimba.
Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya HCG katika kupima mimba, HCG maana yake ni human chorionic gonadotropin ni homoni ambayo uonekanekana kwenye mkojo na damu kama mtu ana mimba. Soma Zaidi...

Mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo chini ya umri wa miaka mitano ili kuweza kuweka afya yake kwenye njia safi. Soma Zaidi...

Dalili za kujifungua
Makala hii itakwenda kukufundisha dalili za kujifunguwa, hatuwa za kujifunguwa na kuzalisha, pia utajifunza mabo muhimu kabla na wakatii wa kujifungua. Soma Zaidi...

Sabau za maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...