5.Tufaha (apple) au epo.
Hili ni katika matunda yaliyokuwa na historia katika maisha ya binadamu toka zamani sana. Wataalamu wa afya wanazungumzia tunda hili kuwa limesheheni virutubisho vingi sana. Tunda hili lina kiasi kikubwa cha vitamin C, vitamin K na vitamini B, pia tunda hili lina kiasi kikubwa cha madini ya potassium pamoja na kambakamba yaani fiber.

Tafiti za kisayansi zinathibitisha kuwa antioxodant iliyopo kwenye tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya moyo na kupunguza hatari ya kupata maradhi ya kisukari hasa kile kinachoitwa type 2 diaberes. Pia antioxidant iliyopo kwenye tunda hili huzuia kupata maradhi ya saratani (cancer) na kusaidia katika kuongeza ujazo wa kwenye mifupa.

Tafiti nyingine za kisayansi zinathibitisha kuwa tunda hili lina pectin. Hii pia huitwa prebiotic fiber nayo husaidia katika kupambana na kuuwa bakteria waliopo tumboni na kusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kuwa katika hali salama na madhubuti. Pia husaidia afya katika metabolic activities nazo na shuhuli zote za kikemikali zinazofanyika ndani ya seli.