4.Buluu beri (blueberry)
Ni katika matunda yanayotambulika kuwa na virutubisho vingi mwilini.. Tunda hili hutambulika kuwa na vitamini c kwa wingi, vitamini K na madini ya manganese. Pia tunda hili lina kambakamba yaani fiber. Itambulike kuwa vitamini C ni katika vitamini vinavyofanya kazi kubwa sana kulinda afya na kuupa mwili uwezo wa kupambana na maradhi kuliko aina nyinginezo za vitamini.

Pia tunda hili lina antoxidant kwa wingi. Hii husaidia katika kupambana na maradhi ndani ya mwili. Antoxidant huzuia mwili usipatwe na maradhi hatari shambulizi kama shambulizi la moyo, kisukari na mengineyo.

Tunda hili pia husaidia katika kufanya madhubuti mfumo wa kinga wa mwili yaani immune system. Wataalamu wamegundua kuwa tunda hili husaidia katika kuuwa seli yaani natural killer cell hali hii husaidia mwili katika kupambana na athari za stress yaani msongo wa mawazo pamoja na mashambulizi ya virusi yaani viral infections.

Pia tafiti za kisayansi zimeonesha kuwa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu. Husaidia tatizo la kupoteza kumbukumbu hasa kwa wazee. Tunda hili ni katika orodha ya matunda ambayo yanajulikana kwa uwezo wake wa kusaidia katika kutunza kumbukumbu na kuondoa tatizo la kusahausahau.