Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako
3.Palachichi (avocado)
Hili ni katika matunda yenye fat (mafuta). Itambulike kuwa si kila mafuta ni hatari ndani ya miili yetu. Tunahitaji vyakula vya fat yaani mafuta kwa ajili ya kutupatia joto kwenye miili yetu. Pia fati husaidia kuipa miili yetu nguvu. Katika tunda hili palachichi mafuta yake ni aina ya oleic acid yaani yapo katika aina flani ya asidi ambayo husaidia katika kupunguza uvimbe mwilini na kusaidia kuboresha afya ya moyo.
Palachici pia hutambulika kitaalamu kuwa lina lina madini ya potassium na magnesium kwa wingi sana. Pia ni katika vyakula vyenye kambakamba yaani fiber. Vyakula hivi vyenye fiber husaidia katika kuweka usalama wa tumbo yaani kuhakikisha chakula kinatembea ipasavyo ndani ya tumbo kutoka sehemu moja mpaka sehemu nyingine mpaka kufika kwenye njia ya haja kubwa.
Pia tunda hili husaidia kupungusa hatari za kupata maradhi ya stroke yaani kupalalaizi kutokana na kiwango kikubwa cha madini ya magnessium ambayo husaidia katika kupunguza shinikizo kubwa la damu. Hivyo palachichi husaidia katika kudhibiti afya ya moyo. Palachichi moja linaweza kutoa 28% ya mahitaji ya mwili ya madini haya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za biringanya/ eggplant
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyanya
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kwa ufupi vyakula vya kuviepuka kama una presha ya kupanda.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu faida za kunywa maji kabla hujula kitu chochote,tunajua kabisa kabla ujala au kunywa chochote sumu nyingi mwilini zinakuwa hazijachanganyikana na chochote kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa kuna faida kubwa nyingi za kunywa maji kama ifuatavy
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...