Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa
Protini ni chembechembe zinazotokea kwa njia ya asili (bila ya kutengenezwa) na zimetokana na asidi za amono (amino acid) zilizounganishwa kwa kutupia bondi za peptide. Neno protini asili yake ni lugha ya Kigiriki ”proteios” likiwa na maana ya kuwa ni kitu kinachopewa nafasi ya kwanza. Yaani protini ni viinilishe “nutrients” ambazo ni muhimu sana mwilini kuliko viinilishe vingine. Neno hili limeanzaka kutumiwa karne ya 19 mwaka 1838 na Mkemia kutoka Swedih Jöns Jacob Berzelius.
Protini huweza kutofautiana namna zilivyo kutoka kiumbe kimoja na chingine, pia protini huweza kutofautiana kutoka kiungo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano protini za kwenye macho ni tofauti na zile za kwenye moyo, ini na figo. Kila kiumbe hai kina protini, na pia protini huhusika katika michakato tata kwenye miili ya viumbe hai, kwa mfano protini huhusika katika kutengeneza antibodies ambazo hutengeneza kinga na kupambana na maradhi na wadudu shambulizi kama bakteria na virusi. Protini hutengeneza enxymes ambazo ndizo hutumika katika kumeng’enya chakula. Pia protini hutengeneza homoni (hormones)
Baada ya kukila chakula chenye protini chakula kinaanza kumengenywa kinapofika kwenye tumbo na utumbo, kisha hufyonzwa kwenye utumbo mdogo na kuingia kwenye mirija ya damu. Pindi chembechembe za protini zinapoingia kwenye damu, damu huanza kusafirisha protini kwenda maeneo mbalimbali ya mwili yanayohitajia protini. Huko protini zitaingia kwenye seli za mwili. Ndani ya seli mchakato kwa kuvunjwa vunjwa protini ili kutumiwa zaidi hufanyika. Ndani ya seli mchakato huu jhufanyka kwenye sehemu inayotambulika kitaalamu kama ribosomes
Miili ya wanyama haina uwezo wa kuhifadhi protini kwa matumizi ya baadaye. Hivyo kama mtu atakula protini nyingi, mwili utaibadili protini kuwa fati na baadaye kutumika kutengeneza nishati ndani ya mwili. Na endapo mtu hataweza kupata protini za kutosha mwili utaanda kuangalia maeneo yenye protini ndingi kama misuli, kisha mwili utaanza kuvunja protini iliyomo mule na kuipeleka maeneo mengine na hapa mtua ataanza kukonda na kupoteza nyama na hatimaye kufariki kama hatapata chakula chenye protini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida kuhusu uyoga mwekundu ni uyoga unaopatikana katika sehemu mbalimbali na pia kuna waliofanikiwa kupandikiza na kuweza kuvuna ila uyoga huu una siri mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukutajia mahonjwa matano ambayo hutokana na utapia mlo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula njegere, kunde, mbaazi, njugu mawe na maharage
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa ajili ya matumizi mbalimbali, Ili kutumia mmea wa mchai chai zifuatazo ni mbinu za kuandaa mmea huu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za kahawa mwilini, ni faida ambazo ujitokeza hasa kwa watumiaji wa kahawa.
Soma Zaidi...Mlo kamili ni mkusanyiko kuu wa vyakula mbalimba kwa pamoja huimarisha na kuujenga  mwili wa binadamu na wanyama kwa sababu vinaleta virutubishi vyote vinavyohitajika.  Mkusanyiko wa vyakula vinavyotengeneza mlo kamili Kuna majina ya vyakula
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu lishe salama kwa mjamzito
Soma Zaidi...