Home Afya Shule ICT Burudani Dini Maktaba Maswali Madrasa Apps Blog Legacy Login

FAIDA ZA MATUNDA


image


Somo hili linakwenda kukuletea faida za MATUNDA mbalimbali na mboga, upatikanaji wake na faida zake kiafya. Pia utakwenda kuona MATUNDA na mboga ambayo Ni kinga dhidi ya maradhi hatari Kama kisukari, saratani, maradhi ya moyo na mfumo wa fahamu pamoja na afya ya ubongo


1. Faida za kula zabibu

1. Zabibu Lina virutubisho vingi Kama vile vitamin C, B6 na K pia fati na madini ya shaba na manganese

2. Ina antioxidants zinazohusika kuondoa sumu za kemikali za vyakula mwilini

3. Hupunguza athari na hatari za magonjwa Kama vile kisukari, saratani na maradhi ya moyo na mishipa ya damu

4. Huondoa stress na misongo ya mawazo

5. Hushusha shinikizo la damu

6. Hupunguza cholesterol mbaya

7. Hushusha kiwango cha sukari kwenye damu

8. Husaidia kuimarisha afya ya macho

9. Huimarisha afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu

10. Husaidia kuboresha afya ya mifupa

11. Husaidia kupunguza maambukizi ya baadhi ya bakteria, fangasi na virusi

12. Hupunguza kasi ya kuzeeka mapema

 

2. Faida za kula nanasi

1. Nanasi Lina virutubisho Kama vile fati, protini, vitamin C na B6, madini ya chuma, manganese na shaba

2. Hupunguza misongo ya mawazo (stress)

3. Nanasi ni rahisi kumeng'enywa tumboni

4. Hupunguza hatari ya ugonjwa wa saratani

5. Huboresha na kuimarisha mfumo wa kinga mwilini

6. Hupunguza maumivu ya viungio

7. Husaidia kupona haraka baada ya kufanyiwa upasuaji

8. Ni tunda tamu

 

3. Faida za kula parachichi

1. Parachichi Lina virutubisho Kama vile wanga, vitamin C, E,K pia lina madini ya magnesium na potassium

2. Husaidia kuboresha na kuimarisha afya ya moyo

3 husaidia kupunguza kupata kwa ugonjwa wa mifupa kuwa dhaifu

3. Huzuia na kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani

4. Huboresha afya ya watoto wadogo na ukuaji wao

5. Hupunguza misongo ya mawazo

6. Huondoa tatizo la kutopata choo kikubwa

7. Husaidia kuondoa sumu za vyakula na kemikali mwilini

8. Husaidia kupunguza maambukizi ya baadhi ya bakteria fangasi na virusi

9. Husaidia kutokupata maradhi ya kisukari

 

4. Faida za kula apple(tufaha)

1. Tufaha Lina virutubisho vingi Kama vile vitamin C, K, E, B1, B2 na B6 pia madini ya potassium

2. Husaidia kupunguza uzito wa ziada mwilini

3. Husaidia kuboresha na kuimarisha afya ya moyo

4. Hupunguza athari za ugonjwa wa kisukari

5 husaidia kupambana na pumu

6. Husaidia kuzuia saratani

7. Husaidia kuboresha na kuimarisha afya ya mifupa

8. Hulinda tumbo dhidi ya majeraha yanayotokana na matumizi ya madawa

9. Husaidia kuimarisha afya ya ubongo

 

5. Faida za kula Embe

1. Huzuia tatzo la kukosa choo kikubwa

2. Huboresha mfumo wa kinga

3. Huimarisha afya ya macho

4. Hupunguza cholesterol mbaya

5. Huboresha muonekano wa ngozi na kuufanya uwe na afya njema

6. Embe ni zuri hata kwa wenye kisukari

7. Husaidia katika kupunguza uzito

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    3 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    5 ICT       ðŸ‘‰    6 Madrasa kiganjani    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS

Imeandikwa na Bongoclass Tags Zaidi , Afya , ALL , Tarehe 2021-10-18     Share On facebook or WhatsApp Topic school Zaidi Dini AFYA ICT Burudani Tags Uzazi maswali Afya mengineyo dini HIV Sira vyakula Matunda HTML php Alif Lela 1 Alif Lela 2 FANGASI Dawa SQL Tips Quran Sunnah fiqh DARSA Magonjwa Tajwid tawhid simulizi Dua Academy Wahenga chemshabongo WAJUWA Michezo ICT Imesomwa mara 706



Post Nyingine


image FAIDA ZA MATUNDA
Somo hili linakwenda kukuletea faida za MATUNDA mbalimbali na mboga, upatikanaji wake na faida zake kiafya. Pia utakwenda kuona MATUNDA na mboga ambayo Ni kinga dhidi ya maradhi hatari Kama kisukari, saratani, maradhi ya moyo na mfumo wa fahamu pamoja na afya ya ubongo Soma Zaidi...