Tufaha ni katika matunda adimu na matamu, je unazijuwa faida zake kkiafya?
5.Tufaha (apple) au epo.
Hili ni katika matunda yaliyokuwa na historia katika maisha ya binadamu toka zamani sana. Wataalamu wa afya wanazungumzia tunda hili kuwa limesheheni virutubisho vingi sana. Tunda hili lina kiasi kikubwa cha vitamin C, vitamin K na vitamini B, pia tunda hili lina kiasi kikubwa cha madini ya potassium pamoja na kambakamba yaani fiber.
Tafiti za kisayansi zinathibitisha kuwa antioxodant iliyopo kwenye tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya moyo na kupunguza hatari ya kupata maradhi ya kisukari hasa kile kinachoitwa type 2 diaberes. Pia antioxidant iliyopo kwenye tunda hili huzuia kupata maradhi ya saratani (cancer) na kusaidia katika kuongeza ujazo wa kwenye mifupa.
Tafiti nyingine za kisayansi zinathibitisha kuwa tunda hili lina pectin. Hii pia huitwa prebiotic fiber nayo husaidia katika kupambana na kuuwa bakteria waliopo tumboni na kusaidia mfumo wa mmengβenyo wa chakula kuwa katika hali salama na madhubuti. Pia husaidia afya katika metabolic activities nazo na shuhuli zote za kikemikali zinazofanyika ndani ya seli.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pilipili
Soma Zaidi...Somo hili linalenga kukujuza juu ya umuhimu wa tikiti kwenye afya ya mwili
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za tangawizi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za mchai chai, ni mmea ambao upandwa na watu kama maua, dawa au kikolezo cha chai na Kuna wengine kabisa wanatumia kama sehemu Mojawapo ya dawa kwa hiyo tutaona faida za mmea huu wa mchai chai.
Soma Zaidi...kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu.
Soma Zaidi...