hivi ndio vyakula vya protini kwa wingi, maziwa, mayai, samaki, dagaa, nyama, maini. Endelea na zaidi
Tunaweza kupata protini kwenye mimea jamii ya mikunde kama kunde na maharagwe. Pia kiasi kikubwa cha protini tunaweza kukipata kwa kula mayai, nyama, samaki, dagaa na maziwa. Pia tunaweza kupata protini kwa kula nafaka kama mchele na nafaka zingine. Ulaji wa mboga za majani unaweza pia kutupatia protini kwa kiasi kidogo. Wadudu kama kukbikukbi, senene na wengineo pia wanaweza kutupatia protini.
Kwa kifupi vyakula vinavyotupatia protini ni pamoja na :-
1.Samaki; samaki ni chanzo kizuri cha protini. Samaki wenye mafuta kama salmon ni vyanzo vyema zaidi vya protini. Ulaji wa samaki umekuwa ni chanzo kizuri cha protini hasa kwa wakazi wa maeneo ya baharini na maeneo ya pwani ama mitoni, mabwawa na maziwa. Tunaposema samaki hapa wanaingia mpaka dagaa, kaa, kaji, kamongo, perege, mikunga, papa na samaki wengine. Pia ulaji wa samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo, kukinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali, chanzo cha madini ya chumvi na fati
2.Mayai; mayai ni katika vyanzo vikubwa vya protini. Karibia watu wengi hujipatia protini kwa kula mayai. Unaweza kula yai likiwa limekaangwa, chemshwa ana la kuchoma. Pia unaweza kula yai bichi kama wafanyavyo baadhi ya watu. Ulaji wowote kati ya niliotaja unaweza kukupatia protini. Ila hakikisha kama umelikaanga ama kulichoma halikauki sana likawa kama chapati iliyokauka, upishi huu unaweza kuathiri virutubisho.
.3. Maziwa; maziwa ni katika vyanzo vikuu vya protini kwa binadamu na wanyama. Maziwa ya mama ni chanzo kipekee kilicho salama zaidi kwa mtoto mchanga kuliko hata ya ng’ombe. Tofauti na kutupatia protini maziwa pia ni chanzo cha vitamini na fati. Maziwa ni katika vyakula vilivyokusanya viinilishe vyote muhimu. Ni vyema kuyachemshha maziwa kabla ya kuyanywa ili kuepuka baaadhi ya matatizo ya kiafya.
4.Nyama; tunaweza kupata protini kwa kiasi kikubwa kwa kula nyama. Nyama ni katika vyanzo vizuri vya protini. Inaweza kuwa nyama nyekundu ama nyama nyeupe. Nyama nyeupe tunaweza kuzipata kwa kula kuku, baadhi ya samaki, kaa. Nyama nyekundu tunaweza kupata kwa kula mbuzi, kondoo na karibia wanyama wengi. Nyama pia ni chanzo kizuri cha fati mwilini. Ulaji wa nyama unaweza kuleta athari za protini kwa muda mchache sana.
5.Mimea aina ya kunde na nafaka; mimea jamii ya kunde hii ni mimea ambayo inatambaa kama kunnde na maharagwe na mimea jamii hii. Mimea hii inatambulika kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Watu wenye kipato cha chini mimea hii ni chanzo chao cha msingi cha kupata protini. Maharagwe yapo katika aina nyingi yapo ya soya na aina mbalimbali. Ulaji wa aina zote hizi unaweza kutupatia protini.
6.Mboga za majani. Kwa kiwango kilicho kidogo tunaweza kupata protini kwa kula mboga za majani. Mboga za majani oekee hazitoshelezi kutupatia kiwango cha protini kinachohitajika. Kwa wale ambao hawali chama (vegetarian) wapo ambao hawali nyama lakini wanakula mayai na maziwa hawa wanaweza kujipati protini kwenye mayai na maziwa. Lakini kwa wale ambao hawali nyama, maziwa wala mayai watahitajika kupata vyamzo vingine mbadala vya protini yaani watumie protini za kutengeneza japo miongoni mwazo zipia mbazo zinatengenezwa kwa wanyama.
7.Vyanzo vingune: tofauti na vyanzo vya protini nilivyotaja hapo juu lakini pia kuna vyanzo vingine kama ulaji wa senene na kumbikumbi na wanaofanana. Kuna baadhi ya jamii zinakula senene hasa jamii zinazopatikana maeneo ya kagera. Kwao senen ni chanzo kizuri sana cha protini. Kumbikumbi nao hupatikana maeneo mengi na jamii nyingi zinatumia chakula hiki.
Umeionaje Makala hii.. ?
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukuletea vyakula vyeny maji kwa wingi na umuhimu wake mwilini
Soma Zaidi...Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya
Soma Zaidi...Somo hili linalenga kukujuza juu ya umuhimu wa tikiti kwenye afya ya mwili
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya Piriton katika kutibu mzio au akeji ni dawa ambayo kwa lingine huitwa chlorpheniramine Maleate.
Soma Zaidi...Matunda yenye vitamni C kwa wingi ni machungwa, maembe, ndimu na limao, endelea kusoma
Soma Zaidi...Zijuwe sababu za upungufu wa damu, dalili za upungufu wa damu na kazi za damu mwilini,n avyakula vya kuongeza damu
Soma Zaidi...Matatizo ya macho yanaweza kuruthiwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto. hata hivyo shughuli zetu na vyakula tunavyokula vinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa matatizo haya. Hapa nitakuletea vyakula muhimu kwa afya ya macho yako.
Soma Zaidi...