Posti hii inahusu mambo yanayochangia katika kupona kwa kidonda, ni mambo ambayo yapo kwa mgonjwa mwenyewe kama ifuayavyo.
Mambo yanayosababisha kupona kwa vidonda.
1. Kiasi au kiwango Cha kidonda.
Kwa kawaida kidonda kikiwa kikubwa uponaji wake uchelewa ukiulinganisha kama kidonda ni kidogo na uponyaji wake uwahi hii ni kwa sababu kidonda kikiwa kikubwa labda na wadudu waliopo ni wengi kuliko kidonda kidogo uwa na wadudu wachache na utunzaji wa kidonda kikubwa ni shida kuliko utunzaji wa kidonda kidogo huwa ni afadhari kwa hiyo kiasi Cha kidonda usaidia kupona haraka kwa kidonda hicho.
2. Mlo wa mgonjwa wa kidonda usaidia kidonda kupona kwa sababu.
Mgonjwa wa kidonda kama anatumia mlo kamili kama vile kiasi kikubwa Cha vyakula vya protein, kiasi Cha kutosha kwa vitamini C kiwango Cha kupona kwa vidonda ni kwa urahisi ukiulinganisha na mtu ambaye mlo wake ni wa kubabaisha kwa hiyo tunajua kabisa kuwa chakula Bora ni dawa kwa hiyo tunapaswa kula vyakula mbalimbali ambavyo vinaongeza kinga mwilini Ili pale tunaposhambuliwa na vidonda tuweze kupona haraka na kurudia kwenye hali zetu za kawaida.
3.umri wa mgonjwa.
Umri wa mgonjwa nao pia uchangiwa katika uponyaji wa vidonda, kama ni mtoto atachukua mda mfupi tu kupona kwa sababu seli zake zinazalishwa kila mara na viungo vyake bado vinafanya kazi vizuri kuliko Mzee, lakini kama ni mzee kupona kwake kitakuwa ni shida kwa sababu kiasi Cha seli zinazokufa ni nyingi kuliko zile zinazozalishwa au pengine seli zinazozalishwa na kufa ni sawa kuliko kwa mtoto ambaye seli zinazaliana ni nyingi zile zinazoharibika.
4. Kuwepo kwa Magonjwa.
Kuwepo kwa magonjwa mengine kwa mtu Mwenye kidonda usababisha kidonda kupona kwa mda mrefu kuliko mtu yule ambaye Hana magonjwa, kwa mfano mgonjwa wa kisukari utumia mda mrefu kupona kwa sababu ya kuwepo kiwango Cha sukari nyingi kwenye damu.kuliko mtu ambaye Hana ugonjwa wa kisukari upona mapema zaidi kwa sababu ya kuwepo kwa sukari ya kawaida kwenye mwili.
5. Sehemu ambapo kidonda kipo.
Kidonda kama kipo sehemu za miguuni, kwenye kucha, na sehemu ambazo ni rahisi kuwepo kwa uchafu kupona kwa kidonda uchelewa kuliko kama kidonda kipo kwenye sehemu za usoni ambapo ni rahisi kusafisha.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Dalili za mimba zinaweza kuwa tata sana kuzijua mpaka upate vipimo. Kwa mfano unaweza kupatwa na maumivu yakibofu. Je unadhani nayo ni dalili ya mimba?
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuyatunza macho
Soma Zaidi...Maumivu ya shingo ni malalamiko ya kawaida. Misuli ya shingo inaweza kuchujwa kutokana na mkao mbaya - iwe inaegemea kwenye kompyuta yako kazini au kuwinda benchi yako ya kazi nyumbani.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu, madhara haya uwapata watu wengi kwa sababu hawajui taratibu za matumizi ya dawa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kizungu Zungu ni tatizo ambalo utokea kwa watu mbalimbali na kwa sababu tofauti tofauti na pengine mtu akipata kizungu sehemu mbaya anaweza kusababisha majeraha au pengine kupata ulemavu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sehemu ambazo zinapaswa kudungwa chanjo, hizi ni sehemu zile zilizopendekezwa kwa ajili ya kuchoma chanjo kwa kadiri ya kazi ya chanjo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki-ngono-na-mtu-aliye-na-vvu-na-ukimwi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kushuka
Soma Zaidi...