Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu
Ni nini husababisha mdomo kuwa mchungu?
1.Mdomo kutokuwa msafi. Hii ni kawaida wakati umelala mdomo bakteria waliokuwa wapo mdomoni wanaendelea kufanya kazi yao, kula mabaki ya chakula na kuendelea kuzaliana. Kumbuka mate yana kazi ya kusafisha mdomo,lakini wakati umelala mate hayawezi kufanya kazi hii kwani huwezi kuyatoa. Hivyo uchafu huendelea kujizalisha bila ya kutolewa. Hali hii inaweza kusababisha mdomo kuwa mchungu unapoamka.
Vyema usile kitu muda huu, kabla ya kupiga msaki. Safisha kinywa vyema ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya muda mchache. Pia kama ulitoka kulala baada ya kutema mate kwa muda mchache yaani baada ya mdomo kujisafisha hali hii inaweza kuondoka bila ya wasi wala hakuna ulazima wa kupiga mswaki, kwani mdomo una sifa ya kujisafish awenyewe kwa kutumia mate.
2.Matumizi ya madawa ya antibiotics au antidepressants. Dawa hizi pindi mdu anapozitumia hufyonzwa ndani ya mwili na kutolewa kwa kupitia mate na kusababisha mate kuwa machungu. Mfano wa dawa hizi ni:-
A. Tetracycline
B.Gout medication kama allopurinol na lithium
C.Madawa yanayotumika kutibu maradhi ya moyo.
Baada ya kuacha kutumia dawa hizi ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya siku chache. Pia unaweza kunywa juisi ya vitu vichachu kama hali itaendelea kukusumbuwa.
3.Ujauzito, hali ya mdomo kuwa mchungu ama kuwa na ladha ya chuma kwa wajawazito ni kawaida na hali hii kutaalamu hufahamika kama dysgeusia ama metallic taste. Hutokea kwa uda wa siku kadhaa kisha huondoka. Baadhi ya wajawazito wanapata ladha ya pesa, yaani kama ulishawahi kuweka mdomon hela ya sarafu, ile ladha unayoipata ndio ambayo huwapata baadhi ya wajawazito.
4.Kama unatumia dawa za kuongeza vitamini, unaweza kupata ladha hii. Kuna baadhi ya dawa za vitamini zina madini mengi ya metali. Madini hayokama zinc, shaba, chuma na chromium. Kama dawa hiyo ina madini haya inaweza kubadili ladha ya mdomo na kuwa chungu
5.Ni dalili ya maradhi ya ini. Kama ini lako halifanyi kazi vyema ama lina matatzo, mwili utakuwa na kiasikikubwa cha ammonia ambayo ni sumu. Hatimaye kubadili ladha ya mdomo.
6.Mashambulizi ya kwenye mfumo wa upumuaji. Wakati mfumo wa upumuaji unapokuwa katika mashambulizi ya bakteria ama virusi au fangasi, inaweza kuathiri ladha ya mdomo.
7.Kama umecheuwa, hali hii inaweza kupelekea kubadilika kwa ladha ya mdomo
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo hutumika kuponyesha majeraha kwa haraka zaidi,tunajua majereha utokana na kupona kwa vile vidonda au kupona kwa sehemu ambayo imekuwa na majeraha kwa hiyo ili kuponyesha majeraha hayo tunapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za seli. Seli ni chembechembe hai za mwili ambazo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Swali languKwanini mtu alie ng'atwa na nyoka hairuhusiwi kumpa pombe?
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukufundisha kazi 5 za maafu mwilimi. Wengi tunajuwa tu kuwa mapafu yanafanya kazi ya kupumuwa. ila si hivyo tu yapo mengi zaidi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi athari za kutotibu vidonda, hizi ni athari mbalimbali ambazo zinaweza kutokea ingawa kama vidonge haujatibiwa au vimetibiwa kwa kuchelewa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Imani potofu juu ya chanjo kwa watoto na akina Mama, ni baadhi ya Imani waliyonayo watu juu ya chanjo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo maradhi huambukizwa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi imani potofu waliyonayo Watu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, hizi ni imani ambazo uwepo kwenye jamii na pengine uweza kuaminika lakini si za ukweli.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea endapo tatizo halijatibiwa.
Soma Zaidi...