Hii posti inahusu zaidi sifa za mkojo usio wa kawaida,ukiona mkojo wa namna hii unapaswa kwenda hospitalini kwa matibabu au vipimo vya zaidi.
Kiasi Cha mkojo kisicho Cha kawaida
1.kiasi Cha mkojo ,
Kuna wakati mwingine kiasi Cha mkojo ubadilika na kuwa mwingi au kidogo, ikiwa kiasi Cha mkojo kinaongezeka kuliko kawaida inawezekana ikawa ni shida ya sukari mwilini hii hali ya mkojo kuwa mwingi huitwa polyuria na pengine kiasi Cha mkojo kuongezeka inawezekana mtu ametumia dawa kama vile frusemide,au lasix, potassium citrate na digitalis hizi ni dawa ambazo uongeza kiwango Cha mkojo.
2.Na Kuna wakati mwingine kiasi Cha mkojo kinapungua hii kwa kitaalamu huitwa Oliguria kiasi Cha mkojo kinapungua ndani ya maasaa ishilini na manne hili tatizo utokea zaidi kwa watu wenye matatizo kwenye nephroni, matatizo ya moyo, na watu wale wenye ugonjwa wa kuishiwa maji iwapo mtu anaona dalili hizi za kuona kiasi kidogo Cha mkojo anapaswa kwenda hospitalini kupima.
3. Kuna wakati mwingine mkojo ukosa kabisa na figo linakuwa halitoi kabisa mkojo,hii ni hatari kwa sababu kunakuwepo na matatizo kwenye nephroni au kwenye figo au pengine damu inashindwa kusafili mpaka kwenye figo na usababisha kutokuwepo kwa mkojo kwa mtu, hii hali ikitokea ndani ya maasaa ishilini na manne mgonjwa Inabidi apelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi.
4 Tunapaswa kujua kuwa kitendo Cha mkojo kukosa ndani ya maasaa ishilini na manne ni tofauti na Ile hali ya mtu kusikia mkojo lakini akawa anashindwa namna ya kupitisha kwa Sababu maalumu kwa hiyo tunapaswa kumhudumia mgonjwa ambaye anakosa mkojo na kunywa anakunywa kila kitu kama kawaida.
5. Kwa hiyo tukiona kitendo Cha mtu kukojoa mara kwa mara, au kukojoa kidogo,au kushindwa kukojoa kabisa tujue kuwa sio dalili nzuri kwa sababu mkojo unachujwa kutoka sehemu mbalimbali za mwili Ili kuondoa sumu mwilini, kwa hiyo sumu isipoondolewa shida nyingine zinaweza kutokea kwenye mwili wa binadamu na kusababisha madhara mengine makubwa,kwa hiyo tunapaswa kudhibiti hali hii mapema.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi athari za kutotibu maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo, nimatazito yanayoweza kutokea iwapo ugonjwa huu hautatibika.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kutumia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda, ni njia muhimu ambazo ni lazima kuzipitia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu Mambo yanayopunguza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.
Soma Zaidi...Katika vyakula tunaposema wanga tunamaanisha virutubisho ambavyo hupatikana kwenye vyakula. Hivi husaidia sana katika kuifanya miili yetu iwe na nguvu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...upungufu wa damu wa madini ya chuma ni aina ya kawaida ya upungufu wa damu hali ambayo damu haina chembe nyekundu za damu zenye afya. Seli nyekundu za damu hubeba oksijeni kwa tishu za mwili. Bila chuma cha kutosha, mwili wako hauwezi kutoa dutu ya k
Soma Zaidi...