Imani potofu kuhusu kifua kikuu

Posti hii inahusu zaidi imani potofu waliyonayo Watu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, hizi ni imani ambazo uwepo kwenye jamii na pengine uweza kuaminika lakini si za ukweli.

Imani potofu kuhusu kifua kikuu.

1.mwenye kifua kikuu ana Maambukizi ya virus vya ukimwi, hii ni mojawapo ya imani ambayo imo miongoni mwao Watu wengi wakiamini kuwa mwenye kifua kikuu ana Maambukizi ya virus vya ukimwi, hii siyo kweli kwa sababu kifua kikuu kinapona ila Ukimwi hauna dawa na kifua kikuu usababishwa na bakteria bali Ukimwi usababisha na virus.

 

2.Watu wanaweza kusema hivyo kwa sababu dalili za awali zinaweza kufanana ila sio kweli kuwa mwenye kifua kikuu ana ukimwi kwa hiyo vipimo ni vya la, lazima ili kuweza kutambua kuwa ni kifua kikuu au ni Maambukizi ya virus vya ukimwi.

 

3.Imani potofu nyingine ni kuwa mwenye kifua kikuu anapaswa kutengwa kwenye jamii.hii ni imani ambayo Watu wanayo kwamba mtu akiwa na kifua kikuu hapaswi kuishi na wengine anapaswa kutengwa na vyombo vyake visichanganywe na vya wengine ili kuepuka kuambukiza wengine.

 

4.Ni kweli kama mtu hajaanza kutumia dawa anaweza kuambukiza wengine kwa hiyo hatupaswi kuwatenga wagonjwa wa kifua kikuu bali tuwapeleke hospitalini wapime na wakianza kutumia dawa baada ya wiki mbili hawaambukiza Watu wengine kwa hiyo hatupaswi kuwatenga bali tuwahudumie kama wagonjwa wengine.

 

5. Kwa hiyo ambacho tunapaswa kujua ni kuwa kifua kikuu kinasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ila mtu akipata dawa hawezi kuambukiza wengine na pia ugonjwa huu unatibika vizuri sana na jamii isiwatenge wagonjwa hawa kwa sababu nao wanahitaji huduma kama wagonjwa wengine 

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/16/Wednesday - 10:08:41 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 937

Post zifazofanana:-

Chanzo cha VVU na UKIMWI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyanzo m ali mbali vinavyohisiwa kuwa chanzo cha UKIMWI Soma Zaidi...

Upungufu wa vyakula vya madini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula vya madini Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma
Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa ukoma ni Ugonjwa unaosababishwa na bacteria anayejulika kama mycobacterium leprae. Soma Zaidi...

Hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na Soma Zaidi...

Madhara ya kupungua kwa homoni ya projestron
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa homoni ya projestron ikipungua mwilini na pia kuweza kutambua dalili za kupungua kwa homoni hii ya progesterone. Soma Zaidi...

Vyakula vyenye maji kwa wingi
Somo Hili linakwenda kukuletea vyakula vyeny maji kwa wingi na umuhimu wake mwilini Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu vitamini K na kazi zake mwilini
vitamini k ni moja katika vitamini vinavyoitajika sana mwilini. Je unazijuwa athari za upungufu wa vitamini k mwilini? Soma Zaidi...

Dalili za gonorrhea
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya dalili za gonorrhea Soma Zaidi...

Namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo. Soma Zaidi...

Dalili za mtu aliyekula chakula chenye sumu
Post hii inahusu zaidi mtu aliyekula chakula chenye sumu, chakula chenye sumu ni chakula ambacho kikitumiwa na mtu yeyote kinaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu hata kifo. Soma Zaidi...

Aina za kifua kikuu.
Posti hii inahusu zaidi aina mbili za kifua kikuu, aina ya kwanza ni ile ya kawaida ambayo ushambulia mapafu na aina ya pili ni ile ambayo ushambulia sehemu mbalimbali za mwili kama vile kwenye limfu node, kwenye sehemu za moyo, kwenye uti wa mgongo, kwen Soma Zaidi...

Tango (cucumber)
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula tango Soma Zaidi...