Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu.
Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu. Ni vigumu kuwatofautisha wenye sumu na wasio na sumu kwani wakati mwengine wanafanana sifa. Wataalamu wameweka njia kadhaa za kuweza kuwajuwa weenye sumu. Nyoka mwenye sumu ana sifa zifuatazo
1.kichwa chake kipo katika pembe tatu
2.Rangi zake zinameremeta sana
3.Mboni ya Macho yao yamefanana na macho ya paka
4.Wanapoogelea kwenye maji miili yao inaelea juu
Tmbua kuwa sifa hizi hata nyoka wasio na sumu wamaweza kuwa nazo. Kuwa makini na kaa mbali na nyoka wa aina yeyote kama huna ujuzi na utambuzi huu. Mtu aliyengatwa na nyka mwenye sumu ataonyesha dalili zifuatazo:-
1.Uchovu
2.Kizunguzungu
3.Anaweza kuzimia
4.Kichefuchefu
5.Kuharisha
6.Kutapika
7.Mapigo ya moyo kuongezeka kwa kasi
8.Misuli kukosa uweze wa kutanuka na kusinyaa
9.Kuvimba eneo alipong’atwa.
Ukiona mtu ameng’atwa na nyoka na akaonyesha dalili hizi, wahi kuomba msaada ili awahishwe ituo cha afya kwa haraka. Hakikisha unampatia huduma ya kwanza ili kupunguza athari za kusambaa kwa sumu mwilini. Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka inaweza kuwa kwa nama zifuata zo:-
1.mtulize mgonjwa nafsi yake, mpe maneno matamu na ya kutuliza. Hii itasaidia moyo kupunguza kazi ya kusambaza damu mwilini, hivyo sumu haita sambaa kwa kasi.
2.Muweke mgonjwa chini, na katu usimtembeze, mlaze chini kwa namna ambayo sehemu alipong’atwa itakuwa chini. Kwa mfano kama ameng’atwa mguuni, unaweza kumuwekea kitu kichwani akaegemea kwa mto ili sehemu ya mguuni iwe chini.
3.Ondoa mengo ya nyoka kwa uangalifu na katu usimishe eneo alilongatwa na nyoka.
4.Kama mgonjwa ana kizunguzungu, ama baridi mfunike kwa nguo ili kumuongezea joto
5.Chukuwa maelezo kuhusu aina ya nyoka, hii itasaidia wataalamu wa afya kujuwa tiba sahihi.
6.Osha eneo kwa kupitishia maji kwa juu na katu usisugue ama kuminya jeraha.
Usifanye vitu hivi:
1.Usinyonye sumu kwa mdomo wako
2.Usimpe mgonjwa chakula wala maji
3.Usimtembeze mgojwa
4.Usitumie barafu sehemu yenye jeraha
5.Usifunge kwenye jeraha eti kuzuia mzunguo wa damu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu namna ya kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima, ni njia ambazo utumika kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima au kumwosha Mgonjwa hasa wale walio mahututi na hawawezi kuamka kitandani.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali ya maumivu ya mwili, Maumivu ya mwili utokea kwa aina mbalimbali kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula vya madini
Soma Zaidi...Ajali ya kichwa na ajali inayotolewa kwenye sehemu mbalimbali za kichwa, ambavyo husababishwa madhara kwa aliyepata ajali hiyo
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa vijana
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu.pua ni mlango wa fahamu ambao uhusika na kupumua.
Soma Zaidi...upungufu wa damu wa madini ya chuma ni aina ya kawaida ya upungufu wa damu hali ambayo damu haina chembe nyekundu za damu zenye afya. Seli nyekundu za damu hubeba oksijeni kwa tishu za mwili. Bila chuma cha kutosha, mwili wako hauwezi kutoa dutu ya k
Soma Zaidi...Posti huu inahusu zaidi visababishi mbalimbali vya magonjwa, tunajua wazi kuwa ugonjwa ni hali ya kutokuwa kawaida kwa ogani mbalimbali kwenye mwili na kusababisha mwili kushindwa kufanya kazi zake vizuri.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wajawazito na wanaonyonyesha
Soma Zaidi...