Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini .
1. Basi baada ya wale watoto wawili kukutana na mwalimu wa Ile shule, Hawa watoto hawakujua kwamba ni mwalimu Bali ni msamaria mwema tu, basi watoto Hawa walinunuliwa soda , mtoto wa maskini kwa sababu alikuwa na kiasi na wazazi wake walimwambia kwamba asitumie vitu vya kula njiani kwa mara nyingi alitunza Ile soda ila mtoto wa tajiri kwa sababu ya kula kula kila mara alibugia Ile soda na kwa sababu tumbo lilikuwa halijakaa vizuri alianza kuendesha tena.
2. Basi yule mtoto badala ya kukimbilia chooni alijichafua kwenye nguo zake na akasubilia kusafishwa kama kawaida yake , Bali yule mwalimu alimwambia mwanangu hauko nyumbani na pia wazazi wako hawapo hapa jikaze ujisafishe kwa sababu yule mtoto wa maskini aliona jinsi wale makonda walivyomsafisha na yeye akachukua maji akammwagia maji na mwalimu akamwambia ajisafishe na yeye akajisafisha na kwa sababu ilikuwa usiku kidogo baridi lilikuwa ni kama lote mwalimu akamwonea huruma akaamua kumuomba number ya wazazi wake na kuwapigia.
3. Basi baada ya kusikia sauti ya wazazi wake alilia kwa sauti kubwa na kuanza kusema kwa nini mmenitesa kwa nini hamkunifundisha maisha na mbona watoto wenzangu hawana shida hapa mimi mtaniua kama maisha ni hivi hamjanitendea haki mwenzangu aliambiwa kila kitu hata hajaaibika hata kidogo na wazazi wakalaumiana wao kwa wao, basi mtoto akasema sitapanda tena gari la jumla nataka gari la binafsi , kwa sababu baba Ela zilikuwepo aliongea na yule mwalimu Ili wakodi gari la binafsi na yule mtoto wa maskini pamoja na yule mwalimu walikodiwa gari na wakasafiri mpaka shuleni, yule mtoto wa tajiri alifurahi sana na yule mtoto wa maskini alikuwa akishangaa kila kitu.
4. Basi baada ya kufika pale shuleni mwalimu akajitambulisha wazi kwamba yeye ni mkuu wa shule pale yule mtoto wa tajiri aliumia sana kwa sababu alikuwa hataki kuhaibika na akikumbuka alichokifanya shuleni, kwa hiyo wanafunzi wakapelekwa bwenini, wakaweka vitu vyao mwalimu alishangaa kuona mtoto wa maskini akiwa na ki mzima kidogo na mtoto wa tajiri ana kila kitu na begi kubwa na ka thamani kubwa kwa hito mwalimu akaona tofauti kati ya wake watoto kati ya vitu walivyonavyo na kati ya tabia zao.
5. Basi wakapelekwa mezani kupata chakula wakakuta ni ugali wa Dona maharage na pia maji ya kunywa , yule mtoto wa maskini akamshukuru Mungu kwa kuona chakula cha aina Ile na mtoto wa tajiri aliangua kilio kuona chakula kile kwa sababu alikuwa hajawahi kuona na watu wote wakaamka na wafanyakazi wakashangaa yule mtoto.
Itaendelea
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 web hosting 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
USALITI (sehemu ya tatu)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi.
Soma Zaidi...Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme (sehemu ya nne)
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne ni pale bibi anawachanganya kwa maneno yake yaani mke wa kwanza anaambiwa aandae malkia na mke mdogo atafute njia za kufanya kijana wake kuwa mfalme.
Soma Zaidi...Mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake.
Soma Zaidi...Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini.
Soma Zaidi...SAFARI YA MUUJIZA sehemu ya tatu
Post hii inahusu Zaidi hadithi ya safari ya muujiza ambapo ya Mungu mengi anaenda kwao na kuomba kufahamu history yake ili afahamu kuhusu wazazi weo walipo na ndugu zao walipo.
Soma Zaidi...NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku
Soma Zaidi...