picha

WAKATI WA KUFUMBUKA

Post hii ni mwendelezo wa hadithi inayohusu Kufumbuka ambapo , John anaonekana kama sio mtoto wa Mzee maganga kwa sababu na miungu imekili kwa sababu chakula chote kimeliwa na kuisha.

WAKATI WA KUFUMBUKA. 

Wakati ulipofika kutangazwa kwamba John sio mtoto wa Mzee maganga watu wote walishangilia sana na kupiga makofi kwa sababu walijisikia vibaya kuona John anamsaidia Mama yake maria ,kwa sababu John alimpenda sana mama yake ,alipewa nafasi ya kuongea kwamba anasemaje na wengi wakidhani kwamba anataka kujitetea Ili kuendelea kuishi kwenye ukoo.kwa hiyo aliisimama akiwa ana uchungu mkubwa ,wengi wakidhani labda ana uchungu wa kutopokelewa kwenye ukoo ila kwake ulikuwa ni uchungu wa kuona roho mbaya za watu ambao wanawatenga wenzao hasa upande wa mama zao waliona hawana haki.

 

 Basa baada ya kuona John amesimama mda mrefu bila kuongea Mzee mmoja mwenye busara akamtoa John pembeni akamwambia kwamba unapaswa kuongea na ukoo kufuata Mila na desturi Ili uweze kuhudumiwa kama mtoto wa nyumba hii na ukoo huu kwa sababu miungu imekukataa na pia baba zako wamekukataa, John akatikisa kichwa sawa,kwa hiyo Mzee mmoja  akasimama mbele ya umati akasema kwamba kwa niaba ya John anapenda kuongea Ili kuweza kurudi kwenye ukoo kama mwana ukoo kwa sababu tangia utoto wake ameshiriki mema yote ya hapa na kila kitu kwa hiyo anaomba ukoo wa kununua na jamii iendelee kumpokea, wakamuuliza John yeye hakusema chochote kwa sababu alikuwa na hasira, basi mkutano ukahailishwa na kila mtu akarudi kwao.

 

Basi na John akamshika mama yake mkono wakaelekea nyumbani, yule kijana aliyeona jinsi wazee walivyokula zile nyama ,siku Moja kwa kujiiba alipaswa kwenda kwa John usiku mmoja,kwa sababu hawakuruhusiwa kwenda mchana ,kwa sababu hawakupaswa kuongea na mama yao pamoja na mjomba wao kadri ya familia hii upande wa mama hawakuudhamini, basi yule kijana akamwambia  John kila kitu kikafahamika, kwa hiyo wakapanga jinsi ya kuwaibisha jamii ya wazee Ili waweze kujenga msimamo wa kujali familia kwa usawa hasa upande wa mama.

 

Kwa kawaida kama mtoto akionekana hafai kwenye familia Ili kuweza kurudi kwenye familia hiyo ni lazima kutoa matoleo maalumu kama vile ngombe kumi, pombe vidumu kumi, kuku kumi, mbuzi kumi, na vyakula,na mambo hayo yalichinjwa na watu walikuja kusheherekea na kula na mtoto aliingizwa ndani kadri ya utaratibu. Kwa kawaida mtoto aliongea neno na kuomba kuingia kwenye ukoo,na pia Kuna Mzee aliyesimama kama msimamizi wa kijana, kwa hiyo vitu vilikuwa vingi kwa Vijana walilokuwa na uwezo wa Chini hali iliyosababisha kushindwa kupata ruhusa ya kurudi kwenye ukoo tena au kwa wakati mwingine walipewa ruhusa baada ya miaka mingi, ila kwa John kwa sababu ya kuwa na kipato kikubwa hiyo ilikuwa ni kazi ndogo kwake.

 

Kwa hiyo siku ikafika,Sheria ya kwanza ilikuwa ni kwamba John anapaswa kumtoa mama yake na mjomba wake kwenye nyumba yake na kuwapeleka kwenye nyumba ya watumishi wa kawaida na akishapata ruhusa ya kuingia kwenye ukoo hapaswi kutoa msaada wowote kwa mama na mjomba,hali hii ilimfanya mama kuogopa sana na kuendelea kupoteza matumaini, kwa hiyo John aliongea na mama na mjomba kuhusu lengo lake ambalo ni kuifumbua macho jamii  kwamba watu wote ni sawa na kwamba katika maisha ya makuzi ya mtoto Kuna pande mbili ambazo ni mama na baba na pia wote wanapaswa kupendwa.

 

Hali hii ilimfanya mama na John kuwa na matumaini ila waliogopa sana kwamba uenda na John akauawa kwa sababu ya kuipindua jamii kwamba ni vigumu baba na Mama kuwa sawa na upande wa mama kuwa sawa na upande wa baba, ila John akasema yeye yupo tayari kwa lolote Ila hawezi kuuawa , kwa kaida Mzee maganga alikuwa na majeshi mbalimbali ya kumlinda  kwa yeyote yule aliyeenda kinyume na Mzee maganga aliuwa, kwa hiyo John aliogopa sana kuhusu Ilio kwa hiyo akaunda jeshi lake akaliaandaa akampa mzee maganga kama zawadi akihaidi kwamba ni jeshi ambali litamlinda siku ya kuomba kuingia kwenye ukoo na Mzee maganga alifurahi sana akiwaambia wanajeshi wake kwamba siku ya sherehe hiyo wanapaswa kwenda kulinda mifugo sehemu ya mbali Ili wasije kuibiwa.

 

Kwa hiyo John akawaambia jeshi lake kwamba akiwa anaongea kuhusu kuifumbua jamii kwa kudhamini sehemu ya upande wa mama na kuona kwamba baba na mama wote ni sawa, Mzee maganga akiwaamulu kwamba ua huyo hastahili kuishi mnapaswa kusogea kwangu na kunibeba kwamba Nina haki na kuamulisha kwamba watu wote wakubali na atakayekataa mnamkata kichwa, Basi John akapaswa kuunda na jeshi la ziadi Ili kuzuia habari zisienee mpaka kwenye jeshi la Mzee maganga ambalo liko mbali Ili kuzuia vita kati ya jeshi la Mzee maganga na jeshi jipya la John. Basi na habari ikapita kwa ndugu wa John Ili John akitoa tamko waje wamembeba mama yao wakisema nani kama mama na washangilie ikiwa baba yao atachukia wote wanapaswa kuhamia kwa John kwa maandamano makubwa na kuwashurutisha wazee wote na ndugu kuandamana wakiimba wimbo ufuatao.

 

baba na mama wote ni wazazi,kuwaheshimu na kuwatunza ni kitu cha muhimu kwa sababu wote walishirikiana katika kumtunza na kumlea mtoto na tabia ya kudharau upande wa mama ni dhambi kubwa kwa sababu watu wote ni sawa na wote wanahotaji msaada na kuishi maisha mazuri na ya kumpenda aliyewaumba,

 

Wimbo huu uliimbwa kwa watumishi na washabiki wa John na pia jeshi lote la John wakifahamu wimbo huu, basi siku yenyewe ikafika na nyama zikachinjwa kila kitu kikapikwa na pia miungu nayo waliipatia chakula chake Ili Ile na baada ya kula ndipo wengine wafuate, kwa sababu wale wazee ndio waliokula chakula kile ,waliachwa waendelee na kazi zao za kula chakula Chao, na wakala baada ya kula na sherehe ikaanza, basi ikafika wakati wa  mtoto kuanza kuomba utambulisho wa kuwa mwana ukoo, akaenda yule Mzee aliyehaguliwa kwa kazi hiyo akasema enyi familia na ukoo wa Mzee maganga kwa heshima na taathima kufuatia agizo la ukoo wetu maalufu tukiwa na Sheria kwamba atakayevunja Sheria ya kuthamini mama yake na kutunza upande wa mama yake ni lazima aangaliwe vizuri inawezekana huyo mtoto sio wa familia hii.kwa sababu tatizo hili limemkuta kijana wetu John na ameumia sana na kwa moyo wote amehiari kuwa hatahusika tena na kuwa karibu na mama yake Wala kumjali mjomba wake kwa hiyo kwa kutumia Mali zake atawajali upande wa baba tu.

 

Basi watu wote wakashangilia na pia Mzee maganga aliamka kwenye kiti chake na kumkumbatia John na John akamkumbatia baba yake ila machozi yalimtoka na yalikuwa machozi ya hasira kwa sababu ya unyanyasaji wa upande wa Mama kwa hiyo John alipewa nafasi ya kuongea.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2023/03/22/Wednesday - 10:07:05 am Topic: Jamvini Main: Burudani File: Download PDF Views 1197

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰5 web hosting    πŸ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi

Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi.

Soma Zaidi...
Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 3)

Posti hii inahusu zaidi hasara za kuwa na wivu na kutokuwa wazi, sehemu hii inahusu zaidi maendeleo ya Lisa shuleni yanakuwa mabaya zaidi na lina anaendelea kumtunzia siri lengo lake lina ni kuendelea kuwa wa kwanza darasani.

Soma Zaidi...
USALITI (sehemu ya kwanza)

Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili

Post hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mitihani inaisha na wanaanza kuhukumiwa mmoja baada ya mwingine.

Soma Zaidi...
Hadithi katika kijiji cha burugo

Β Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii .

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara.

Soma Zaidi...
Mahusiano ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake.

Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)

Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya.

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI (sehemu ya nne)

Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha.

Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)

Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini.

Soma Zaidi...