Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 11: Kisa cha Kalid na Jalid

Tuendelee kusikiliza na kusoma visa, hadithi, na simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza tuwe pamoja mpka mwisho......

HADITHI YA KHALIDI MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID.

Khalid na jalidi waliishi eneo moja huko kijijii kwao. Walikuwa na chuki zao za muda mrefu na hivyo ilipelekea uadui kati yao.Khalidi hakupendezwa na ile hali ya kuwa na uadui na watu. Khalidi alifahamika kwa ucha mungu pale kijijini na ukarimu alio nao. Wat walikuwa wakimpenda sana khalidina kumchukia Jalidi kwa tabia zake mbaya. Ijapokuwa Khalid alikuwa akimtendea wema Jalidi lakini hili halikumfanya jalidi kupunguza chuku zake kwa Khalidi. Hapo zamani khalidi na Jalidi walikuwa ni marafiki wapenzi sana wa tangu utotoni. Ijapokuwa tabia ya Jalidi haikuwa njema sana hata wazazi wa Khalidi wakawa wanamkataza kucheza na jalidi. Mambo hayakuwa hivyo urafiki wao haukuweza kuvunjika kwa maneno haya. Marafiki hawa wawili walippenda sana kuwinda kwa kutumia manati, mikuki na mishali. Walifahamika kwa uhodari wao pale kijijini walipokuwa wanaishi. Sikumoja walipokuwa wanawinda karibu na mto ghafla nyoka aina ya chatu alimkamata Jalidi na kuanza kumbingirisha ili amuingize kwenye maji. Jalidi alipiga kelele na hiku akijikwamua kwenye mbavu za joka hili lakini juhudi zake zilikwama. Khalidi alikuja akiwa na mkuki wake na kuanza kumsaidia rafiki yake. Khalidi hakuwa na nguvu sana ukilinganisha na Jalidi lakini alikuwa akitumia akili ya ke hasa. Khalidi alikumbuka kauli ya babu yake alipomwambiaga kuwa ukipambana na chatu lenga macho yake, ukiyakosa kamata mkia wake na ukiukosa mtie jeraha sehemu ypyote lakini bora umjetuhi kwa kuuvunja mgongo wake. Mawazo haya yakapelekea mapambano makali kati ya Khalidi na nyoka yule ili kumsaidia Khalidi. Wakati huo Jalidi alikuwa ameshaanzwa kuviringishwa na lijoka hilo tayari kuanza kuvunja mbavu laini za Jalidi. Kwa upande wa Khalidi alikitafuta kichwa kwa hali na mali lakini hakukiona akakumbuka kauli ya baba yake alipomwambiaga “chatu mara nyingi anapokamata huficha kichwa chake ili kisijedhuriwa wakati wa mapambano”. basi akahamia kwenye mkia lakini mkia wa chatu ulikuwa ni vigumu kuumiliki alipoukamata alirushwa na mkia ule na alipata maumivu makali. Katika hali hiyo akakumbuka kuwa aliwahi kusikia kuwa chatu huulinda mkia wake kwa hali na mali. Katika hali hiyo Khalidi akahamia kwenye mgongo na kuamza kumjerui nyoka yule, juhudi za Khalidi hazikutoka patupu alifanikiwa kumtia majeraha kadha na hapo chtu akaanza kupoteza nguvu. Wakati anataka kuvunj mgongo wa chatu mkuki ulidunda pale ngonjo ni na ukamtoka mkononi. Mkuki ule ulikwenda mchoma Jalidi kwenye jicho na kumtoboa. Kwa pigo lile chatu alipata maumivu na kukimbia mbalia sana na kumuacha Jalidi akiugumia maumivu. Kuja kupata ahueni Jalidi alijikuta akiwa na chongo la upande wa kulia. Hali hii ilipelekea kutengeneza uadui na kuvunja urafiki. Jalidi aliamini Khalidi alifanya kususi kwani angeweza kumnusuru bila hata kumjeruhi lakini uzembe wake wa kutokukamata vizuri mkuki umepelekea maumivu kwa jalidi. Hivyo uadui huu ukajengeka kwenye nafsi ya Jalidi na kuanza kumfanyia vituki vipy kila siku. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu sana hata Khalidi akachoshwa na vituko vya Jalidi. Hali hii haikumpendeza khalidi hivyo akaamua kuhama kwenda mjini kwa kumkimbia jalidi na kwa kuepusha shari zaidi. Kule mjini Khalidi alifahamika sana wa uchamungu hata ikafikia watu wanampenda sana kwa uchamungu wake. Watu wakawa wanakuja kwake ili awaombee dua kwa Allah Muumba wa mbingu na ardhi. Basi Khali alihamia mjini na kwa pesa alizotoka nazo kijijini alinunua nyumba na kuanza kufanya biashara ndogondogo pale mjini. Watu walimpenda sana Khalidi pale mjini kwa ukarimu, ucheshi na uchamungu wake. Watu kutoka mjini pale walikuwa wakienda kwa Khalidi na kumuomba awaombee dua. Watu wa mjini waliamini dua ukiombewa na Khalidi itkuwa ni yenye kukubaliwa na Mwenyezi Mungu. Basi pale mjini Khalidi aliishi maisha mazuri sana akiwa na upendo kwa watu hata akasahau vttuko vya jalidi. Biashara zake zilipata nuru na kipato chake kikawa kinaongezeka siku hadi siku. Licha ya kuwa nyumba ya khalidi ilikuwa eneo zuri la kibiashara lakini nyumba yake ilikuwa ina kisima ambachoo katu hakikuwahi kukaukwa wala kuchimbwa upya kwa muda wa miaka 50. khalidi alitumia maji haya kwa matumizi ya nyumbani na akawa anatowa sadaka ya maji kwa wapita njia na watu wanaokujwa kununua biashara zake. Khalidi sasa amefika umri wa miaka 30 bila ya kuwa na mke. Sasa khalidi alikuwa akifikiria kupata jiko. Siku moja bila ya kutarajia aliuona uso wa Jlidi pale mjini akija kumsalimia. Khalidi alimpokea Jalidi kwa tabasamu na bashaha akidhani ugomvi wao umekwisha. Jalidi alikaa pale kwa muda wa siku mbili na akawa anachukiwa sana na mafanikio ya Khalidi pale mjini. Basi siku ya tatu walipokuwa wanazungumza huku wanatembea wakati wa jioni wakapita karibu na kisima kile. Jalidi akajifanya anataka aelezwe mengi kuhusu kile kisima ila haukuchukuwa muda akamsukumiza khalidi kwenye kisima. Bila ya kujuwa kinachoendelea kwenye kisima alirudi nyumbani kijijini akiamini ameshammaliza Khalidi.

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-09 14:38:39 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 142


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini na mtumwa
Muendelezo....... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 17: Hadithi ya Malipo ya wema ni wema
Mwendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP4  Part 5: Hadithi ya pili ya mtoto chongo wa mfalme
Hadithi za HALIF LELA U LELA huwa zina muendelezo na hadidhi hii ni muondelezo wa kisa cha pili cha mtoto chongo wa mfamle ambayo imetoka ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 9: Familia mpya
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 5: Simulizi ya samaki wa ajabu
Simulizii hii inapatikana kwenye hadhithi za HALIF LELA U LELA katika kitabu cha kwanza.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 15: Hadithi ya safari ya Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 14: Simulizi ya binti wa kwanza na mbwa
Tuendeleee kuburudika na simulizii zetu nzuri kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 21: Kinyozi mwenyewe
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 3: Aladini akiwa na binti wa mfalme
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 2: Sultani mtoa buradani kufariki
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 12: Sehemu ya tano ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza... Soma Zaidi...