picha

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 14: Hadithi ya kifo cha kujionea

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Muendelezo wa safari ya Sinbad

SAFARI YA SITA YA SINBAD.

 

Walipokusanyika watu wote akaanza kusimulia kuhusu safari yake ya sita. Nilipookoka na safari ya tano sikutamani tena kusafiri kwa njia ile. Hali hii haikudumu kwa muda mpaka nilipoamua kufanya safari ya mwisho kwani nilikuwa uymri umeshakwenda sana. Nikaamini kuwa faida nitakayoipata safari hii sitafanya safari nyingine yeyote ya majini. Basi nilianza kujiandaa kwa ajili ya safari hii. Hata hivyo maandalizi yalichukuwa muda kwani umri ulikuwa umeshakuwa mkubwa. Baada ya maandalizi safari ikaanza.

 

Safari hii ilikuwa mbaya sana, maana hata hatukuweza kupata siku mzima iliyo salama. Mara tuu baada ya kuanza safari kwa muda wa masaa kama nane kwa makadirio upepo uliharibika na kuwa mkali sana. Jahazi lilikuwa likipelekwa tusukokujuwa kwa muda wa siku tano. Siku ya sita upepo ulitulia katika sehemu ambayo hata hatuijui kabisa. Nahodha baada ya kuangalia zaidi eneo hili alilitukusanya karibu na akatuambia kuwa hapa tulipo tupo katika mkondo hatari sana baharini na hakuna jahazi lililokuja mkondo huu na kupona. Ghafla maji yaendayo kwa kasi yakatuchukuwa na kutupeleka kwenye ufukwe wa kisiwa tusichokijua. Tulipofika pale nahodha akatuambia tuchuke sisi na mizigo yetu kisha akagawa chakula tulicho nacho sawa kwa sawa kwa kila mtu. Kisha akatuambia kuwa hapa tulipo hakuna upepo unaotoka kuelekea kokote. Maji yote yanavutwa kuelekea hapa. Na eneo hili kama mnavyoona lina mlima huu ambapo hata ukipanda sauti haitafika popote wala kusikiwa na mtu.

 

Kisha akatuambia kuwa hakuna yeyote atakuja kutuakoaa hapa hivyo maisha ya mtu kuishi yatategemea kuisha kwa chakula chake. Wakati anazungumza maneno yale mimi nilikuwa nawaza yalonikuta kule kwenye mapango. Basi hali ikawa hivyo kwa hakika hakuna pa kutokea. Nilizunguka kuangalia eneo li;le nikagunguwa kuwa kuna mto ambao umetokea mlimani kisha ukakunja bila ya kuingua baharini ukarudi upande wa bondeni kudogo pembeni mwa ufukwe na ukapotelea kwenye pango ililo jembaba.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Mankaa image Tarehe: 2024-09-10 10:15:00 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Views 778

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 2:  Simulizi ya tabibu wa mfalme

Simulizi ni nzuri sana maana zinafundisha na hazibagui mkubwa wala mdogo... tusikilize na kusoma kisa cha tabibu wa mfalme....kutoka katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA...

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 2: Kisa cha kinyozi msiri..

Karibuni tuendelee kusimuliana stori za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza, stori nzuri sana na za kuvutia zimeandaliwa kwaajili ya kujifunza na kujiburudisha pia.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 2: Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake

Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na husikiliwa na kusomwa na wakubwa kwa wadogo pia hadithi hizi zimeenea duniani Kate zikisikilizwa na maelfu ya watu mbalimbali.

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo....

Soma Zaidi...