Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA...
SIRI YA KIFO YAFICHUKA
Kijana akaanza kueleza kuwa huyu binti ni mkewangukabisa na ni mtoto wa mjpomba wangu, na huyo mjomba ni huyu mzee. Mimi na mkewangu tuliiishi vyema sana. Mkewangu alinipenda sana na miaka yote tulioishi sikuweza kumuona na tabia mbaya hata siku moja. Niliweza kuzaa nay watoto watatu. Siku moja alikuwa anaumwa, maradhi haya yali dumu kwa muda uliokaribia mwezi mmoja kisha akapata nafuu kidogo. Haikuchukuwa muda mrfu akaumwa tena baada ya siku kadhaa akapata nafuu tena.
Siku moja alinipa matumaini kuwa kuwa amepata nafuu sana. Sasa akaniambia kuwa ana hamu na tunda epo na hatokwnda kuoga mpaka ale tunda hilo. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mke wangu. Nilikwenda kumtafutia tunda epo popote pale. Nilihangaika sana kwenye mabostani mengi ya mjini. Lakini bila mafanikio. Siku hiyo nilirudi mtupu kwa mke wangu. Loo siku hiyo mke wangu hakwenda kuoga. Basi siku ilofata nikatoka tena kwenda kutafuta tunda epo. Wakati nilipokuwa nimekata tamaa kabisa ya tunda ndipo nikakutana na mze mmoja akanileza kuwa kuna mji matunda hayo yanapatikana. Basi nikafunga safari kulekea huko.
Safari ilinichukuwa siku tatu hata kufika na kurudi na nilinunua matunda matatu kwa gharama ya vipande 15 vya dhahabi. Cha ajabu niliporudi mke wangu hakuwa tena na hamu ya tunda epo. Lakini alichukuwa matunda yale na kuyaweka kwenye kabati. Siku tatu zikapita bil mke wangu kugusa yale matunda. Basi siku ya nne nilipokuwa mtaani nilikutana na kijana mmoja mtanashati sana akiwa na tunda la epo. Kijana yule nikamuuliza wapi amepata ili nikanunue mengine. Kijana akanieleza kuwa “nimepewa na mpenzi wangu kama zawadi, mumewe alikwenda mbali safari ya siku tatu kununua maepo matatu kwa thamani ya vipande 15 vya dhahabu. Na mkewe ambaye nimpenzi wangu wa siri akanipatia kama zawadi.
Niliposikia maneno haya nilistaajabu sana na kuvurugwa moyo wangu. Nilitoka mbio hadi kwa mke wangu. Nilipoangalia kabatini nilikuta tunda moja halipo na yamebakia mawili. Nilistaajabu na kuyasadikisha maneno ya yule kijana. Nilimkamata mkewangu na kmchoma kisu cha tumbo kisha nikamchinja na kumkatakata vipande na kuvifunga kama ulivyoona kwenye boksi. Baadaye nilianza kujuta sana na kulia sana.
Kitu cha ajabu siku ya tatu niimkuta mwanagu analia sana. Nilikuwa na uhakika kuwa hatambui kuwa kama mama yake nimemchinja. Basi nikamuuliza mwanangu kipi kinakuliza?. akanieleza kuwa “naogopa mama akirudi atanipiga, matunda yake matatu nimechukuwa mmoja, nikaenda nalo kucheza. Mkaka mmoja akaninyang’anya na kunipiga, nikamwambia kuwa ni la mama ameletewa na baba kutoka mbali safari ya siku tatu na amenunua kwa thamani ya vipande vitatu vya dhahabu. Yule mkaka akakimbia nalo” basi hapo hapo nikamwambia mwanangu anyamaze.
Dah nikagundua kuwa yule kijana alikuwa ni muongona ndiye chanzo cha kifo cha mke wangu. Niliia sana sanaaaa. Baba mkwe wangu ambaye ni mjomba wangu huyu hapa akaja. Nikamueleza kila kitu naye alilia sana. Hivyo khalifa mimi ndiye niliyemuuwa huyu binti, tafadhal niadhibu mimi niweze kulipa deni la nafsi ya mke wangu. Baada ya kusikia habari hii khalifa akamueleza waziri Mansur. “Nenda ukanitafutie huyu kijana, ninakupa siku tatu tu, na endapo hutamleta nitakuchinja kama alivyochinjwa huyu binti”.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:54:08 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 209
Sponsored links
👉1
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2
Simulizi za Hadithi Audio
👉3
Kitabu cha Afya
👉4
kitabu cha Simulizi
👉5
Madrasa kiganjani
👉6
Kitau cha Fiqh
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 10: Hadithi ya Ndoto ya binti mgonjwa wa mfalme
Skmulizi hii ipo ndani ya kitabu cha kwanza kwenye hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 10: Jumba la Aladini
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 20: Kinyozi maishani mwangu
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 13: Wageni wa Baraka kujongea
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part24 : Kaka wa tatu wa kinyozi
Muendelezo Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 2: Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake
Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na husikiliwa na kusomwa na wakubwa kwa wadogo pia hadithi hizi zimeenea duniani Kate zikisikilizwa na maelfu ya watu mbalimbali. Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini akiwa hatiani
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 7: Sehemu ya nne ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 3: Uokozi kwenye kisiwa
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 22: Kaka wa kwanza wa kinyozi
Muendelezo.... Soma Zaidi...