Menu



Simulizi za Hadithi EP 10 Part 7: Taharuki

Muendelezo.....

TAHARUKI

Siku hiyo kamaralzamani Feki alikuwa ufukweni kukaguwa mendeleo, alikuwa yeye na mke mwenzie. Wakiwa wanakaguwa mara wakaona chombo kipya kinaingia. Wakasogea karibu. Ilikuwa ni kawaida ya kisiwa cha Serendib kuwa hakuuzwi bidhaa yeyote mpaka ikaguliwe. Katika ukaguzi ikafahamika kuwa mmilikiwa maboga hayupo kwenye dau. Baada ya kufuatilia kumbe alikimbiwa. Sasa bibi aliyejifanya Kamaralzaman akanunua maboga yale na kuwarudishia pesa ili wakampe mwenye maboga. Mzigo ukapelekwa kwa Binti mfalme wa Serendib kwa masharti kuwa asiyapasue mtu maboga kwani anataka kujifunsisha upishi wa maboga kutoka kwa mtoto wa Mfalme wa Nchi za China.

 

 

Basi baada ya kufanya kazi zao hapo wakarudi kwao na kuanza kuchambuwa maboga yao waanza upishi. Walikuwa wanatabia hii ya kupika wenyewe siku mojamoja. Watu walikuwa wakifurahi wakijuwa kuwa Kamaralzaman na me wake ndio wanapika. Ilikuwa haruhusiwa mtu kuingia jikoni wakati wawili hawa wanapika. Hii ilikuwa ni njia yao ya kufcha siri yao. Sasa wakiwa wameanza kuyachambuwa vyema maboga yao wakagundua kuna kitu. Walipopasua loo ni vipande vya dhahabu tupu walipolipasua lile kubwa bint mfalme wa nzi cha china alichikwa na butwaa kuona kamkufuu kake. Alifurahi sana akiamini kuwa sasa anakwenda kumuona mume wake. Akamueleza kila kitu kuhusu ule mkufu mke mwenzie.

 

 

Kwa haraka wakaagiza nahodha wa marekebu ile aitwe haraka. Alipokuja wakamwambia aende saa hivi akamchukuwe mwenye maboga bila hiyo mizigo yao na watu wote hawatatoka pale. Basi hakuwakuwa na budi ila ni kuanza safari ya kwenda kumchukuwa Kamarakzaman. Walipofuka kule walimbeba na kummalizia stori zote kwenye dau. Baada ya mwendo wa wiki mbili wakafika serendib. Kwa siri waliagizwa wamvalishe kitambaa sikijulikane. Moja kwa moja akachukuliwa na walinzi na kupelekwa kwa binti sultani. Hakujuwa kinachoendelea baada ya kuoga kuvaa nguo safi na kupata chakula kila mtu alikuwa akimuhedhimu akidhani ndio mume wa binti Sultani.

 

 

Alipomaliza kila kitu akachukuliwa kwa mabinti hawa wawili na kupewa habari nzima. Siku ilofata wakamuita mfalme na kumueleza kila kitu. Kwakweli walifurahi watu wote wa furaha kubwa sana. Pia walimsifu binti wa nchi za uchina kwa uvymilivu na ujasiri.basi ndoa ikafungwa tena hapa. Na Kamaralzaman akawa na wake wawili. Aliweza kupata watoto kutoka kwa wake zake wote. Watoto wake waliweza kurithi madaraka ya mababu zao. Baada ya miaka alirudi kwao Peshia na wake zake. Wajukuu zake alibakia kwa mababu zao waweze kuwaliwaza. Maisha ya Kamaralzaman na wawekake yalikuwa ni ya furaha sana. 

 

Mwisho wa hadithi zetu za HALIF LELA U LELA kitabu cha tatu,, tukutane kwenye simulizi nyingine nyingi, mbalimbali na zakufundisha na na kuburudisha...

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa image Tarehe 2024-09-10 15:13:37 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 405


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 14: Hadithi ya kifo cha kujionea
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Muendelezo wa safari ya Sinbad Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 17: Ufupisho wa ALIFU LELA U LELA KITABU CHA KWANZA
Huu ni ufupisho mfupi kuhusiana na kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 2: Aladini kwenye pango la utajiri
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 8 Part 3: Kijana mchonganishi
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 3: Aladini akiwa na binti wa mfalme
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 17: Hadithi ya Malipo ya wema ni wema
Mwendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 4: Ndoa ya kwanza
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 9: Familia mpya
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 5: Safari ya kwenda nyumbani
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hadithi ya Nurdini Mtoto wa Waziri
Hii ni hadithi ya kitabu cha tatu cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...