Muendelezo.....
VIATU VYA AJABU VYAONDOKA NA MKONO WANGU
Aliponieleza sifa za viatu anavyotaka nikamsogelea kwa ukaribu na kumkazia macho kama nataka kumpiga vile kisha nikamuuliza “wewe ni nani, na ni nani amekutuma, vina nini hasa viatu hivi” alibakia kimya kwa muda kidogo kisha aksema “baba anakutafuta, anakuhitaji uende nyumbani”. nikamuahidi kuwa nitakwenda siku ya ijumaa. Basi akaniahidi kuwa atakuja na ndugu yake kesho kuja kunielekeza nyumbani kwao.
Kesho yake nikaandaa pale ndani chumba kingine kitupu. Nikaweka vyakula na vinywaji. Alipokuj tukaendelea kuburudika na wageni wangu watatu wenzie wamefunika sura zao. Mmoja kati yao alitoka nje, kisha baada ya muda akarudi. Basi kumbe alikwenda chukuwa dawa bila ya sisi kujuwa akiweka kwenye kinywaji na tukalewa, na kuja kuamka ni usiku na nilipowasha taa nikakuta pembeni yangu kuna kichwa cha yule binti wa siku zote aliyetaka viatu. Sikuweza kuwaona wenzie wawili.
Nilishituka sana kuona binti amekufia kwangu, nikafunga duka na kuchimba shimo uwani nikamfanyia maiti yake maandalizi yote na kumzika kwa siri. Usiku huohuo niliondoka na kurudi misri. Nikawa kila baada ya miezi 6 nalipa pesa ya ada ya kile chumba. Nilikaa misri kwa muda wa miaka mitatu hata nikajiridhisha kuwa huwenda mpaka sasa wakawa wamesahau kilichotokea. Nikaamuwa kurudi tena Yemeni ili nikamalize kazi yangu ya kuwatafuta wale watu. Pia kukutana na yule mzee aliyenitafutaga.
Nilifika Yemeniwakati wa usiku, nikaingia dukani kwangu na kuanza kusafisha, alama za michirizi ya damu zilikuwa zikionekana. Nilisafisha, sasa nilipokuwa naamsha viti ndipo nikaokota pete. Pete ilikuwa na picha ya kichwa cha mamba kwa juu. Picha ya kichwa cha kunguru na kambale kwa upande wa pembeni kulia na ushoto. Nikaamuwa kuiuza pete ile nipate pesa za kuanzia maisha. Nikaenda kwa sonara wa kwanza akasema hanunui pete ila maana ni ya thamani sana.
Nikaenda kwa sonara mwengine akaniambia nisubiri. Akaondoka kidogo na kwenda alikokwenda kisha akarudi. Akanieleza kuwa hawezi kununua. Kume aipotoka alikwenda kutoa taarifa kuwa pete iliyoibiwa imeonekana. Usiku askari wakanifamia na kunibambikia kesi ya wizi vinginevyo nitaje jinsi nilivyoipata pete ile. Mbele ya kadhi nilishindwa kueleza ukweli nikiamini kuwa nikieleza ukweli ndio nitauliwa. Nikamueleza niliiba kwa binti mmoja.
Baada ya hapo kadhi akanipa hukumu ya kukatwa mkono wangu. Nilishukuru kukatwa mkono ili kunusuru kichwa changu. Walinikata mkono, nilipata maumivu makali sana, damu ilitoka na nikapoteza fahamu. Nilipokuja kushituka nikajikuta nipo kwenye kitanda. Nilijiuguza pale kwa muda wa siku tatu. Siku ya nne akaja mzee mmoja mrefu mwenye sura ya heshima. Kwa kumuangalia utajuwa kuwa ni mchamungu, pia ni tajiri. Akaniambia “mwanangu, najua hii pete hukuiiba, naelewa fika hii pete haiwezi kuibiwa, hivyo basi nieleze historia yako na hadi likatokea hili la kutokea”. nikaanza kumueleza mpaka mwisho, kuanzia wageni wa baba, hata nikafika Yemeni na haliyotokea.
Nilipomaliza kusimulia yule mzee alikuwa akitokwa na machozi kisha akaema kwa hakika umesema vyema kwa hakika hukudanganya. Nilitambua historia yako hata kabla hujaitaja. Nilitaka kuthibitisha ukweli wa maneno yale, yaliyonenwa na wageni wale, yapata miaka 10 iliyopita. Mwananfu kuwa na amani hapa ulipofika ni kwenu, na jihisi upo kwa baba yako. Natambua yaliyomkuta baba yako, mwanangu na wewe. Nitakueleza kuanzia tafsiri ya waliyoyatenda wageni wale kwenu, na maswali mlioyashindwa kuyajuwa kuhusu wageni wale.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:16:40 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 86
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Kitabu cha Afya
Simulizi za Hadithi EP 8 Part 2: Siri ya kifo
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 12: Hadithi ya mfalme alikuwa kwenye kisima
Wapendwa tuendelee kuoata stori nzuri na za kusisimua kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 5: Simulizi ya samaki wa ajabu
Simulizii hii inapatikana kwenye hadhithi za HALIF LELA U LELA katika kitabu cha kwanza.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Rafiki wa ukweli
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 4: Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu.
Hadithi za HALIF LELA U LELA hii ni moja wapo imetoka katika kitabu cha kwanza imaelezea kisa cha mzee wa tatu.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 14: Jaribio la pili kwa Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 11: Vidole gumba vilikatwa
Kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA kina simulizi nyingi nzuri na za kusisimua, muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 5: Mshenga wa Aladini kwa mara ya pili mbele ya mfalme
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 10: Mapenzi kwenye mtihani
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 3: Kisa cha mke na kasuku
Simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizii hii inasimulia kisa cha mke na Kahuku wake.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 15: Aladini na kitabu
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 10 Part 4: Ndoa ya kwanza
Muendelezo..... Soma Zaidi...