Simulizi za Hadithi EP 5 Part 11: Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza....
NDANI YA PANGO LA MAKABURI
Mmoja wapo akatowa kamba na kulifunga jeneza vizuri na kuanza kulishusha chini ya mapango kwa kamba ile.hatimaye n ikahisi jeneza limefika chini kutokana na kugonga chini. Nikalifungua jeneza lile na kutowa mikate yangu nane na maji yangu. Nikaangalia huku na huku hakuna pa kutokea. Nikaangalia juu ni mbali sana na tundu ni dogo na hata sauti haifiki. Nilizunguka mchana mzima sikupata pa kutokea. Sikuya kwanza, pili, tatu mpaka siku ya nne sikupata pa kutokea. Nilikata tamaa nikajua sasa huu ndio mwisho wa Sinbad.
Nikaanza kula mikate yangu kwa kuilinda ili isiishe kwa araka. Sasa imefika siku ya sita nikiwa na mikate miwili mkononi. Ilipofika siku ya saba mida ya mchana nikasikia migongano. Nikasogea karibu kwenye lile tundu loo!! ni jeneza linakuja. Nilikuwa nikihisabu siku kwa kuangalia mwanga kwenye tundu lile dogo la kuingizia majeneza. Jeneza lile lilipofika chini nikaona mwanamke aliye hai amezikwa na mumewe. Mwanamke yule nikamsaidia kutoka pale nikiwa na imani kuwa ana mikate yake saba ambapo huenda akanisaidia pindi ya kwangu ikiisha. Nikamsaidia kutoka pale na kujanae pembeni kabisa ya lile pango ambapo harufu za wafu hazifiki kwa kasi.
Siku ile usiku nilipolala ghafla nikasikia sauti ya mnyama anayechimba, nikasogea vizuri ila kwa kuwa ni kiza nisione vyema. Nikamwacha akaenda kule kwenye wafu na kuanza kula mizogo. Aple nilipo nikajisemea kuwa sasa huenda hii ndio nusura. Mnyama yule akala mizoga na muda wake ulipofika akatoka. Mimi nikawa namfatilia kwa nyuma usiku ule, tukapita njia nyembamba sana hatimaye akatokea baharini. Basi nikarudi tena kule pangoni kwenda kumchukuwa yule mwenzangu na kuchukuwa mali ambazo watu wamekuwa wakizikwa nazo kama mikufu ya dhahabu na thamani nyinginezo.
Nilibeba mzigo mkubwa sana wa mali za dhahabu na thamani nyingine nzuri. Tukatka mimi na mwenzangu yule na kwa bahati tukakutana na jahazi linaloelekea baghadad. Tulipanda mimi na mwenzangu yule. Tulipofika baghadad niliwahadithia kila kilichotokea na walishangaa sana kuniona nipo hai. Yule mwanamke nilompata kule nilisubiri eda yake ilipoisha kulingana na tamaduni za waislamu nikamwoamimi. Kwa hakika safari hii nimepata faida sana na mafunzo mengi.
Sin bad alipomaliza hadithi hii ya safari yake ya nne akamwambia Sinbad mbeba mizigo kuwa awahikesho ajesikia yalompata kwenye safari ya tano. Safari hii ya tano kuna matukio kadhaa yalinikuta hivyo uwahi mapema. Kisha akampatia pesa kwa ajili ya matumizi ya siku ile na ijayo. Watu wote wakatawanyika.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 18: Binti wa pili mwimba mashahiri mwenye makovu
Mwendelezo wa hadithi kutoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA......
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 2 Part 3: Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi.
Simulizi za HALIF LELA U LELA ni nziri sana tuwe pamoja kusikiliza kisa cha mzee wa pili na mbwa wawili weusi...
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho
Ni mojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....
Soma Zaidi...