Muendelezo
HADITHI YA KAKA WA TATU WA KINYOZI
Kaka yangu wa tatu alikuwa ni kipofu. Alipata upofu badala ya kupata ajali katika shughuli zake za kutafuta mali. Baada ya kupata upofu alikuwa akijipatia pesa kwa kuombaomba kutoka kwa watu. Kaka hakuwa na mke wala watotot. Ilitokea siku moja katika kuombaomba kwake alifika kwenye nyumba moja. Akagonga mwenyenyumba alipouliza kaka hakujibu kitu. Lengo lake ilikuwa mpaka ajemwenyeyumba ili atakapomuona ataweza kumsaidia. Kwa mara ya pili mwenyenyumba akauliza “wewe nani na unataka nini?”/ kaka hakujibu kitu hata akauliza kwa mara ya tatu bila ya majibu tena.
Mwenyenyumba alikasirika na akatoka kuja mlangoni. Alipofika mlangoni akamkuta kaka. Kaka akamweleza kuwa anahitaji msaada japo wa chakula ama pesa. Kwa hasira mwenyenyumba akamwambia nifate. Kaka akamfuata kwa kumshika kipande cha kanzu yake. Wakiwa wanapanda ngazi za gorofa kaka aligundua kuwa walikufika hadi gorofa la nne. Juu kileleni mwenyenyumba akamwambia kaka “umesema unahitaji nini” kaka akajibu “msaada, wa kifedha ama chakula”. mwenyenyumbq akajibu “ruka chini hapo msaada upo huko mbele” kaka akagunduwa kuwa endapo ataongeza hatua mbili mbele ataangukia chini. “kama hutaki kunisaidia si ungenieleza tu toka mwanzo” “nilipouliza nani aliyekuwepo mlangoni na nini unataka haukunijibu” yalikuwa ni maneno ya kaka na mwenyenyumba.
Kaka akagunduwa kuwa endapo ataendelea kupoteza muda anaweza kuuwawa ama kupata madhara zaidi. Kaka akashuka kwa haraka huku anahisabu vingazi alipokazibia chini kwa bahati mbaya alianguka na kuumia vibaya. Kaka akaelekea asikokujuwa akiwa anaugumia maumivu ya mguu. Katika kutembea huku na kule alikutana na vipofu wengine wawili. Kwa kuwa nao walikuwa hawakujui wendako wakaungana na kutengeneza mstari mmoja wa vipofu. Wakiwa wanatembetembea wakafika kwenye kajumba kamoja wakakaa. Wakiwa wamepumzika ghafla wakasikia sauti za watu zinawakaribia.
Kaka akashauri wenzie wazunguke nyuma ya nyumba wajifiche wasije onekana. Wakazunguka nyuma kimyamkimya, na baada ya muda wale watu wakaingia kwenye kijumba kile na kuakuzungumza. Katika mazungumzo ya watu wale kaka aligunduwa kuwa walikuwa ni wezi na pale walikuja kuficha pesa walizoiba. Walipatana warudi pale baada ya wiki moja huku wakisubiria mtaani kutulitulia. Waliziweka pesa zao kwenye moja ya sanduku la mbao lililopo pale ndani. Kisha wakaondoka zao.
Kaka na wenzie walikaa kule nyuma ya kijumba kile, kisha walipojiridhisha kuwa wale watu hawapo tena walirudi walipokuwa mwanzo. Wakajadiliana na kukubaliana kuwa wazitfute zile pesa na wagawane. Wakaingia ndani na kuzitafuta. Baada ya muda wakafanikiwa kuzipata. Loo ilikuwa ni viande 3000 vya dhahabu na 200 vya silva. Wakakubaliana kugawana kiasi kile cha pesa. Wakati wapo katika harakati za kugawana kaka aligunduwa kuwa kuna mgeni kati yao. Kaka akawaambia wenzake “mbona kuna mtu mwingine kati yetu”. Wakaanza kuchunguza wakamgundua mtu wa nne.
Wakamkamata na kuanza kumshambulia kwa kumpiga. Kaka akachukuwa zile pesa na kuzificha tena. Kakana wenzake wakamburuza yule mwingine hadi mbali kidogo na lile eneo a kuanza kumshambulia tena. Haukupita muda watu wakaanza kujaa. Yule mtu mwingine akajichokowa kwenye macho na kuwa kama kipofu. Kisha akaanza kuguta kelele “jamani naombeni msaada, hawa wenzangu wananionea na kunidhulumu, naombeni msaada”. watu wakaona wawapeleke wote kwa kadhi apate kutoa hukumu kati yao.
Kadhi alipouliza hasa kilichotokea yue mtu akasema “kadhi niadhibu kwanza kisha nitakueleza kila kitu” basi kadha akaamrisha apingwe viboko 25. kisha akaanza kueleza “sisi unaotuona hapa wote si vipofu. Tumeigiza kuwa vipofu ili tupate kuwaibia watu na kuapata msaada wa bure kifedaha. Na kwa kutumia njia hii tumenufaika vyema” kisha akafumbuwa macho yake Loo!! hakuwa kipofu hata kidogo kisha akaendelea kusema “leo tulipata pesa vipande 300 vya dhahabu na 200 vya silva. Lakini tulipokuwa tunagawana wenzangu wakanidhulumu wakati mimi ndiye niliyepata pesa hiyo. Ninakuomba uwaadhibu vikali ili wafunguwe macho yao, na waseme ukweli”.
Basi kaka na wenzake wakaanza kuadthibiwa kwa mijeledi . walichapwa viboko 25, waliposhindwa kufungua macho yao wakaongezwa viboko 25 hata wakashindwa kukaa wala kuzungumza. Kisha wakamuelekea yule mtu wakambana vyema aeleze ukweli vinginevyo ataadhibiwa tena. Ndipo akaanza kutaja kuwa pesa zimefichwa sehem flani, na kama kadhi ataahidi kuwa naye atapewa shea atawaonyesha mahali pesa ilipofichwa. Pia aliongezea kwa kusema “hawa hawatafumbua macho kwa hofu, hivyo kuthibitisha utapeli wetu na wao na kutaka kunidhulumu kwao nitakwenda kuonyesha mahali esa ilipo”.
Kadhi akachaguwa kundi la askari limfate. Akaenda nao mpaka kwenye kale kajumba na kuzitowa zile pesa. Kadhi akampatia yule mtu fungu lake na zilizobakia zikawekwa kwenye hazina ya nchi. Kaka na wenzake wakafukuzwa mjini na hawakutakiwa kuonekana tena. Mimi nilipopata habari hizi nikaenda kumchukuwa kaka kwa siri. Mpaka kufikia hapa kinyozi akamaliza stori ya kaka wake wa tatu. Kisha akaendelea kuhadithia kilichompata kaka wa nne kama ifuatavyo:-
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:24:10 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 124
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Madrasa kiganjani
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 4: Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu.
Hadithi za HALIF LELA U LELA hii ni moja wapo imetoka katika kitabu cha kwanza imaelezea kisa cha mzee wa tatu.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hatma ya Nurdini
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 12: Dirisha moja kwanini????
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 9: Hadithi ya binti wa ndotoni.
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 1: Aladini na taa ya mshumaa wa ajabu
Hii ni simulizi iliyopo ndani ya kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 11: Kisa cha Kalid na Jalid
Tuendelee kusikiliza na kusoma visa, hadithi, na simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza tuwe pamoja mpka mwisho...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 11: Ndani mwa junba la Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 8: Aliyekatwa kidole gumba
Kojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 4: Mshenga wa Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 9: Hadithi ya binti wa mfalme kufichwa.
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 13: Jaribio kwa Aladini kwa mara ya kwanza
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 3: Kisa cha mke na kasuku
Simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizii hii inasimulia kisa cha mke na Kahuku wake.... Soma Zaidi...