image

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini akiwa hatiani

Muendelezo....

NURDINI HATIANI

 

 

 

Mama aliendelea kugomba sana kisha akamfungia binti ndani na kuweka walinznwa kiume, kisha akawaambia “haruhusiwi kuingia wala kutoka yeyote humu ndnai, hata mbwa Nurdini” neno mbwa lilimtoka tu mama Nurdini kisha akajilaumu kwa kumfana nisha mwanaye na Mbwa. Kwani si katika vitendo vya waungwana kuwafananisha watu na wanyama kwa ubaya. Nurdini aliamua kukibia na kuelekea shambani. Mama nurdini aliendelea kumsubiri mumewe ampe habari nzima. Lakini katika nafsi ya mama Nurdini alikusudia kuja kumhauri mumewe amuozeshe Nurdini kumuozesha yule Mtumwa.

 

 

 

Mpaka inafika jioni Nurdini hajarudi nyumbani. Wakati huo ndio mzee Farid anaingia nyumbani. Siku zote waziri Farid alizoea kupokelewa mizigo yake na mkewe ama mtoto wake. Lakini leo hakuna yeyote aliyekuja kumpokea. Jambo hili lilimtia wasiswasi sana. Akaelekea ndani Loo akamkuta mke wake macho mekundu kwa huzuni. Baada ya salamu na kula chakula mke akamueleza mumewe kila kilichotokea. Alikasirika sana na kuhamaki, kuona jambo hili lilitokeaje. Mzee aliona sasa nimeshaharibikiwa. Alitangaza kuwa nitamchinja Nurdini muda wowote nitakapomona.

 

 

 

Kupitia mashushushu wake Nurdini aliupata ujumbe huu. Siku hiyo alirudi saa nane za usiku. Akanyata na kwenda kula chakula. Mzee faridi alihofia sana mali zake na maisha ya familia yake. Mkewake wakati wa usiku alitumia fuesa hiyo kumshauri mumewe amuozeshe Nurdini yule mtumwa. Hapo mzee akamwambia “mke wangu sihofii kumpatia mtumwa huyu mwanangu, ninahofia vipi waziri Masoud atafanya baada ya kuzipata habari hizi. Kwani jambo hili litaweza kupelekea uhasama kati yake na mfalme, na kuweza kupoteza maisha yake, ya familia yake na upotevu wa mali. Mambo haya aliyawaza sana mzee faridi, jash lilimtiririka kila anapowaza hali hii.

 

 

 

Siku tatu zilipita bila ya baba wala mama kumuona mtoto wao kipenzi. Mama alipatwa na hofu. Akaanza kufuatilia wapi mtoto wake anakula na kulala. Aligundua kuwa saa nane za usiku anakuja kula, na ifikapo saa kumi na moja anaondoka. Mama alihuzunika sana. Alimueleza mume wake hali ya mtoto wao. Alitaka kujuwa namna ya kumsaidia. Kwa upande wa binti yeye alikuwa akiendelea kulia kila siku. Akiamini nea katu hatoweza kumuona Nurdini tena. Aliamini kuwa sasa nitakwenda kuuzwa kwingine, na nisimuone tena Nurdini.

 

 

 

Mama naye alitumia fursa ya usiku kwa mara nyingine kuendelea kumshauri mume wake awaozeshe Nurdini na yule mtumwa. Mama alipoona baba nurdini hataki kuelewa somo, akajifanya kumjia juu “ama ndio ulikuwa unamtaka wewe yule mtumwa, maana nilikuwa sikuelewi, mtumwa gani anayewekewa wafanyakazi, pia kama mtumwa alikuwa ni kwa ajili ya mfalme, kwa nini usingempeleka siku ilelile ama siku ya pili yake, kama hutamuozesha Nurdini huyo mtumwa basi muondoe hapa kwangu, maana sitaweza kuwa na mke mwenzangu aliyekutana na mwanangu.” baada ya kuyasema maneno haya mama nurdini akaanza kulia tena kulia sana.

 

 

 

Kwa hakika wanawake wanajuwa madhaifu ya wanaume yapo wapi. Kwa kweli mzee Faridi aliguswa kweli. Alianza sasa kumbembeleza mkewe huku akijitetea wee kuwa yule mtumwa hakuwa na habai nae hizo. Mama nurdini alipoona kuwa sasa somo limempata akakandamiza tena “basi muezeshe mwanangu” saswa nimekubali, ila tuwe tayari na mashambulizi kutoka kwa Masoud. Siku hhiyo baba na mama wakaenda kumvamia Nurdini. Walimkuta jikoniakipakuwa chakula. Baba alijifanya anataka kumchinja, hapo mama akajifanya anakwenda kuamulia. Mwishowe mama akajifanya anapatanisha. Na Nurdini akapigwa ndoa siku ilofata. Mambo haya yote yalifanyika kwa siri sana, bila ya wengine kutambuwa.

 

 

 

Basi Nurdini aliishi na mke wake kwa amani sana katika masiku yale. Wote walitegemea kula kwa baba na mama. Nurdini katu hakujifunzaga kufanya kazi za kuzalisha kipato. Siku zote alitegemea kwa baba kwa kila kitu. Nurdini alikuwa na marafiki wengi lakini ukweli ni kuwa wote walikuwa wakimnyonya Nurdini na kwa pamoja walikuwa wakiwanyonya wazazi wa Nurdini.

 

 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 15:00:16 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 83


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Bostani la kifalme baghadad
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Mtumwa wa mfalme na mawaziri
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha tatu..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 2 Part 4: Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu.
Hadithi za HALIF LELA U LELA hii ni moja wapo imetoka katika kitabu cha kwanza imaelezea kisa cha mzee wa tatu.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 14: Simulizi ya binti wa kwanza na mbwa
Tuendeleee kuburudika na simulizii zetu nzuri kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 16: Kitabu cha ajabu
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 2: Sehemu ya safari ya kwanza ya sinbad
Muendelezo wa stori ya safari ya Sinbad ambayo ipo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 18: Binti wa pili mwimba mashahiri mwenye makovu
Mwendelezo wa hadithi kutoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hatma ya Nurdini
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 9: Hadithi ya binti wa mfalme kufichwa.
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 7: Sehemu ya nne ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part24 : Kaka wa tatu wa kinyozi
Muendelezo Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 12: Dirisha moja kwanini????
Muendelezo.... Soma Zaidi...