Jukumu la serikali katika kuzuia dhuluma
Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma.
Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Kwanza, serikali ya Kiislamu inao wajibu wa kuandaa mazingira mazuri ya kihuduma na kimawasiliano kuwawezesha raia kujiletea maendeleo na inao wajibu wa kuingilia kati ili kusimamia haki na kuzuia dhulma. Ni wakati gani kwa mfano ambapo serikali inaweza kuingilia kati. Allah ndiye aliyeziumba rasilimali zilizopo duniani na hivyo ni wajibu wa binaadamu kuzitumia rasilimali hizo kwa manufaa ya watu na kwa ufanisi. Hivyo serikali yaweza kuingilia kati iwapo rasilimali hizo zitatumiwa kuwadhulumu watu au hazitatumika kwa ufanisi.
Pili, baadhi ya kazi ni haramu katika Uislamu kwa sababu zimefungamana na mambo ya haramu, kama vile kamari, umalaya, uchawi, ulevi n.k. Ni wajibu wa serikali kuona kuwa mambo hayo hayapewi nafasi katika jamii.
Tatu, ni wajibu wa serikali pia kutoa fursa sawa kwa watu wote ya kuendeleza na kuvikuza vipaji vyao kwa kuwapa fursa sawa za elimu na mafunzo. Ni wajibu wa serikali kugharamia elimu kwa ajili ya manufaa ya watu wote. Elimu ni haki ya msingi kwa wanadamu wote.
Nne, ni wajibu pia wa serikali kuhakikisha kuwa hata katika zile kazi za halali kisheria zinafanywa kwa uadilifu pasi na dhulma yoyote. Yaani Serikali ihakikishe mathalani kuwa bidhaa zinazotolewa zimefikia ubora kwa wanaoizalisha, kuona kuwa uadilifu wa kitaalamu unadumishwa, kuona kuwa Wafanyakazi wanalipwa mishahara kwa haki.
Hata hivyo, Uislamu hauelemei upande mmoja tu wa kumtetea mfanyakazi peke yake wala kumtetea mwajiri peke yake. Wafanyakazi pia wakileta madai yasiyo ya haki ni juu ya serikali kuingilia kati.
Tano, ni wajibu wa serikali pia kuzuia mambo yanayoweza kudhuru watu, kwa mfano kama mtu akijenga kiwanda cha hatari katika makazi wanamoishi watu. Au hata mambo yanayoweza kuwatesa wanyama, kama kuwabebesha mizigo mizito sana hadi wanaanguka na kuvunjika miguu au kufa, au kuwafanyisha kazi kwa mateso makubwa na kutowapa chakula cha kutosha. Hali kadhalika serikali inaweza kwa mfano kuzuia magari au meli iliyopakia abiria au mizigo kuliko uwezo wake.
Sita, katika suala la usambazaji wa bidhaa, serikali inaweza kuingilia kati iwapo watu watahodhi vyakula na bidhaa nyingine muhimu kwa lengo la kupandisha bei.
Saba, ni wajibu wa serikali kujenga miundo mbinu (in-frastructures) na kuidhibiti, kwa mfano kujenga barabara, madaraja, reli, kusambaza maji ya bomba, kujenga mitambo ya umeme, simu n.k.
Wakati wa Ukhalifa wake, Ali (r.a) alimwambia Nahri, ambaye alikuwa mkuu wa jimbo la Misri; “Usifanye ukusanyaji wa kodi ya ardhi kuwa ndiyo kazi yako kubwa; kazi yako kubwa ni kuindeleza ardhi hiyo.”
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina ๐2 web hosting ๐3 Kitabu cha Afya ๐4 Kitau cha Fiqh ๐5 Madrasa kiganjani ๐6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Jinsi ya kusherehekea siku ya idi katika uislamu
Uislamu umeweka taratibu maalumu za kuzifata katika kusherehekea siku ya idi.
Soma Zaidi...hukumu ya ombaomba katika uchumi wa kiislamu
Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili.
Soma Zaidi...Maana ya swala
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno ยSwalaatย lina maana ya ยombi au ยdua.
Soma Zaidi...MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO
MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO.
Soma Zaidi...