Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu.
Milki ya Rasilimali
Ili kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo. Miongoni mwa rasilimali kuu (natural re-sources) ni zile zinazohusiana na ardhi, maji na wanyama. Kwa mujibu wa Uislamu rasilimali hizo ni neema za Allah (s.w).
“Na katika ardhi mna vipande vinavyoungana (na kuzaa kwake namna mbali mbali) na mna mabustani ya mizabibu, na mimea mingine, na mitende ichipuayo katika shina moja na isiyochipua katika shina moja. Vyote vinavyonyweshelezwa (vinamiminiw a) maji yale yale; na tunavifanya bora baadhi yake vyengine katika kula (katika utamu). Hakika katika haya zimo ishara kwa watu w anaotia mambo akilini”. (13:4)
(b) Rasilimali za maji na mvua
“… Na unaiona ardhi imetulia kimya lakini anapoyateremsha maji juu yake, inataharaki na kukuwa na kuotesha kila namna ya mimea mizuri.” (22:5)
“Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka maw inguni. Kisha akayapitisha (chini kwa chini) yakawa chemchem katika ardhi, tena akaotesha kwayo mimea ya rangi mbali mbali (na sura mbali mbali)…” (39:21).
(c)Rasilimali za bahari na samaki
“Mwenyezi Mungu ndiye aliyekutiishieni bahari ili humo zipite merikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake na mpate kushukuru ”. (45:12)
“Na yeye ndiye aliyeitiisha bahari ili humo mule daima kitoweo kipya (samaki) na mtoe humo mapambo mnayoyavaa. Na utaona merikebu zikipasua humo, ili mtafute fadhila zake (kwa kufanya biashara) na ili mpate kushukuru.” (16:14)
(d)Rasilimali za wanyama
“Na (pia) amewaumba wanyama. Katika hao mnapata (vifaa vitiavyo) joto na manufaa; na wengine mnawala(16:5).
Na mnaona raha mnapowarudisha jioni na mnapow apeleka malishoni asubuhi.(1 6:6)
Na (wanyama hao pia) hubeba mizigo yenu kupeleka katika m iji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka na taabu. Hakika Mola wenu ni Mpole sana (na) Mwenye rehema nyingi”.(16:7)
Na (amewaumba) farasi na nyumbu na punda ili muwapande na (wawe) mapambo. Na ataumba (vipando vyingine) msivyovijua ”. (16:8).
(e) Rasilimali za madini
Muhutasari wa aya hizo juu ya rasilimali unapatikana katika aya ifuatayo:
“Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi.” (2:29).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hadithi hii inakwenda kukufundisha historia fupi ya adhana pia utakwenda kujifunza jinsi ya kuadhini na kuqimu.
Soma Zaidi...Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu.
Soma Zaidi...Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.
Soma Zaidi...