Navigation Menu



Sifa za stara na mavasi katika uislamu

2.

Sifa za stara na mavasi katika uislamu

2. Sitara



Sitara ni sharti la pili ya kusimamisha swala. Ili Muislamu swala yake isimame analazimika kusitiri uchi wake kulingana na mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu (s.w). Sio kujisitiri kwa kufuata matashi ya jamii ya Kitwaghuti.



Sitara ya Mwanamume



Utupu wa mwanamume ni sehemu yote iliyo kati ya kitovu na magoti. Hivyo, Muislamu mwanamume akiwa na nguo ya kutosha kufunika kitovu na magoti na sehemu yote iliyo baina ya hivyo anaweza kuswali.



Lakini kwa ukamilifu mtu anapoweza kuwa katika hali ya kawaida avae kama kawaida ya kuvaa. Tukumbuke kuwa Allah (s.w) anatutaka tujipambe wakati wa kwenda kwenye swala. Anatuagiza:



“Enyi wanaadamu, chukueni, mapambo yenu katika kila swala... ” (7:31)
Kujipamba hapa ni pamoja na kuvaa vizuri na kujipaka manukato ambayo kwa wanaume ni Sunnah.Wanawake wanaruhusiwa kupaka manukato yasiyo na harufu kali.



Sitara ya Mwanamke



Kutokana na umbile lake, aurah (uchi) ya mwanamke ni mwili mzima isipokuwa uso na viganja vya mikono. Muislamu mwanamke swala yake haitaswihi iwapo sehemu nyingine yoyote ya mwili itakuwa wazi bila kufunikwa wakati wa swala. Kuhusu vazi la mwanamke wa Kiislamu, tunafahamishwa kwa uwazi katika aya ifuatayo;



Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika (na ni uso na vitanga vya mikono). Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasioneshe mapambo yao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume zao.... au wanawake wenzao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume (watumwa zao), au wafuasi wanaume w asio na matamanio (kw a w anaw ake) au w atoto ambao haw ajajua mambo yanayohusu uke. Wala wasipige miguu yao ili yajulikane yaliyofichwa katika mapambo yao. Na tubieni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Wa is lamu ili mpate kufaulu. (24:31)



Neno “ziinah” lililotumika katika aya hii lina maana mbili; Uzuri wa kuumbika kiwiliwili (na) uzuri wa kujipamba kama vile pete, vidani na nguo.
Aya hii inatupa fundisho kuwa, sitara ya mwanamke ni mwili mzima, kwa vile kila sehemu ya mwili wa mwanamke ni pambo lenye kuwavutia wanaume jambo ambalo huweza kuleta vishawishi na kuruka mipaka ya utu. Hivyo Allah (s.w) ametoa tahadhari kuwa wanawake wasidhihirishe miili yao na mapambo yao na wala wasionyeshe dalili ya kuwa na mapambo waliyoyavaa kwa mitingisho ya mwili isipokuwa kwa wale wasioweza kuwatamani wakiwa ni miongoni mwa Maharimu zao, wanawake wenzao na watoto.
Pia pamoja na kujifunika mwili mzima wanawake wanaamrishwa wateremshe shungi zao ili pamoja na kufunika nywele zifunike pia shingo na kifua.
Aisha (a.s) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Swala ya mwanamke baleghe haikubaliki bila ya shungi.



Katika Hadith tunafahamishwa kuwa, pamoja na kutekeleza sharti la kufunika mwili mzima na kuteremsha shungi, sharti la pili la vazi la mwanamke wa Kiislamu ni kuwa vazi hilo lisibane mwili kiasi cha kuonyesha ramani ya mwili. Sharti la tatu la vazi la Kiislamu ni kuwa liwe zito kiasi cha kutoweza kuonyesha rangi ya ngozi au umbo la mwili. Kama tuonavyo umezuka mtindo wa wanawake kuvaa nguo zinazofunika mwili bila ya kuficha. Juu ya mtindo huu Mtume (s.a.w) amesema:
Katika vizazi vijavyo vya umma w angu w atakuwepo w anawake ambao watavaa lakini watabaki uchi. Hao hawataingia Peponi wala kupata harufu yake.


Pia Hadithi ifuatayo inafafanua zaidi:
Aisha (r.a) amesimulia kuwa siku moja Asma ’a bint Abubakar alikuja kwa Mjumbe wa Allah wakati akiwa amevalia nguo nyepesi, Mtume (s.a.w) alimwendea na kumwambia: “Ewe Asmaa msichana anapofikia balegh (anapovunja ungo) si sawa sehemu yoyote ya mwili wake kuachwa wazi isipokuwa hii na hii. Alionyesha uso na viganja. (Abu Daud).



Sharti la nne. Pia vazi la mwanamke lisiwe lenye kuvutia sana kiasi cha kuwa sababu ya kuvuta macho ya watu. Wake wa Mtume (s.a.w) na wanawake wa Kiislamu wanaamrishwa katika Qur-an:



Ewe Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa kiislamu, wajiteremshie vizuri shungi (nguo) zao. Kufanya hivyo kutawapelekea wajulikane upesi (kuwa ni watu wa heshima), wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu(33:59)
Katika aya hii imebainishwa kwa uwazi kuwa lengo kubwa la kujisitiri ni kuchunga heshima ya mwanamke wa Kiislamu na kuwatakasa na mambo maovu.


Masharti mengine ya mavazi ya Kiislamu ni kwamba vazi la mwanamke Muislamu lisiwe sawa na lile vazi linalojulikana kuwa ni la wanaume:


Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Abbas (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake na wanawake wanaojifananisha na wanaume.


Pia vazi lisiwe la fahari, majivuno na kibri. Hii yote ni kumtakasa mwanaadamu na uchafu wa nafsi na kumvisha joho la usafi na utu.
Hivyo ni dhahiri kwamba Muislamu akitekeleza kwa ukamilifu sharti hili la sitara kwa kuzingatia masharti haya ya kujisitiri na akawa anafanya hivyo kwa swala zote tano za siku, na akawa anavaa nguo nzuri katika swala, atakuwa msafi wa mwili na mwenye kuheshimika katika jamii.



Swala hutoa fundisho na mazoezi makubwa mno ya kujisitiri na kujiheshimu hasa kwa wanawake.Kwa mfano mwanamke Muislamu anayejisitiri vilivyo kwenye swala, humzoesha kubakia katika hali ya sitara anapokuwa nje ya swala katika maisha yake ya kila siku. Kwani Mungu yule yule aliyemuamrisha kujisitiri wakati wa swala ndio huyo huyo aliyemuamrisha kujisitiri anapokuwa mbele ya wasio maharimu wake.



Je, si jambo la kushangaza kumuona mwanamke anayejisitiri vizuri wakati wa swala, na kutembea uchi barabarani mara tu baada ya swala? Je, anaweza kusema swala yake imemsaidia kumtakasa na mambo maovu na machafu? Swala inayomtakasa mja na mambo maovu na machafu ni ile inayomfanya mja afuate kwa kila hali mwenendo wa maisha anaouridhia Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha yake.



Pamoja na kutekeleza masharti ya mavazi, mavazi hayo pia hayana budi kuwa twahara.




                   


Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 2632


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Hili ndio lengo la kufunga.
Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga. Soma Zaidi...

Mgawanyo wa mirathi kutoka kwenye Quran
Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo. Soma Zaidi...

Tathmini ya swala zetu, kwa nini swala zetu hazijibiwi?
Soma Zaidi...

Sunnah za siku ya idi na utaratibu wa kusherehekea
Hapa utajifunza utaratibu wa kusherekea ifil fitir. Pia utajifunza sunnah zinazoambatsns na idil fitir Soma Zaidi...

Usimamizi wa Haki na haki za binadamu Katika Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa jirani
Soma Zaidi...

Haki za raia katika dola ya kiislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nyakati za swala za dharura swala ya mgonjwa na mafiri
Soma Zaidi...

Swala ya tarawehe jinsi ya kuiswali
Post hii itakwenda kukufundisha kuhusi swala ya tarawehe, faida zake na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

darsa nzuri zenye kuelimisha hasa katika ndoa ya kiislam.
Assalaam alykum warahmatullah wabarakatuh. Soma Zaidi...