Sera ya uchumi katika uislamu

Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu.

4. Sera ya uchumi katika Uislamu

 


Kwanza, katika Uislamu utekelezaji wa mambo yote hutegemea zaidi ucha-Mungu wa mtu binafsi na kuogopa kwake kusimamishwa mbele ya Allah na kuhisabiwa, kuliko usimamizi wa vyombo vya dola kama sheria, mahakama, na askari polisi. Hii ni kwa sababu hisabu siku ya kiyama itakuwa kwa kila mtu binafsi. Hapana shaka vyombo vya dola vipo katika Uislamu na vinafanya kazi lakini msisitizo wa utekelezaji wa mambo yote upo katika uadilifu na taqwa kuliko katika kuogopa polisi na ma ha k ama.

 


Pili, uhuru wa watu binafsi kufanya wanalolitaka ndio sera inayofuatwa katika Uislamu. Yaani katika masuala ya uchumi Uislamu umempa uhuru kila mtu afanye lile analoliona linafaa. Na serikali ya Kiislamu haitaingilia uhuru wake huo isipokuwa tu pale ambapo haki haitatendeka iwapo uhuru huo hautaingiliwa. Mtume (s.a.w) amelielezea kwa ufasaha sana suala hili pale alipoyapigia mfano maisha ya watu katika jam ii na wasafiri waliomo chomboni baharini:

 


“Hebu tuchukue mfano wa meli inayosafiri baharini ikiwa imejaza abiria ambao wamekaa katika sehemu zote za chini na juu. Sasa iwapo abiria mmoja aliyekaa katika sakafu hiyo ataamua kujipatia maji kirahisi kwa kutoboa pale alipoketi na iwapo abiria wengine watamzuia kufanya hivyo (na ni wajibu wa abiria wote walio juu na chini kumzuia) watamnusuru yeye na wao wenyewe na kufa maji. Iwapo watamwacha atoboe basi watazama wote waliochini na juu ya meli.” (Bukhari).

 


Mfano huu unatuonesha kuwa japo Uislamu unampa kila mtu uhuru wa kufanya alitakalo lakini uhuru huo una mipaka. Iwapo mtu atafanya jambo lisilo la haki basi serikali ya Kiislamu lazima iingilie kati kwa maslahi ya jamii nzima.

 


Tatu, wajibu mkubwa wa serikali ya Kiislamu ni kusimamia haki na kuzuia dhulma katika maisha ya jamii.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1324

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 web hosting    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Hijjah

Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtazamo wa uislamu juu ya ndoa ya mke zaidi ya mmoja

Je jamii inachukuliaje swala la kuoa mke zaidi ya mmoja.

Soma Zaidi...
Hutuba ya Ndoa - Khutbat nikah

Hii ni hutuba ya ndoa kwa ufupi, Imekusanya mambo ya msingi yanayohitajika katika hutuba ya ndoa

Soma Zaidi...
Hadathi ya kati na kati

Posti hiibinakwenda kukufundisha kuhusu hadathi ya kati na kati.

Soma Zaidi...
Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu

Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu.

Soma Zaidi...