Jinsi ya kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa


image


Post hii itakufundisha taratibu za kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa.


Kuzika
Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa. Japo ni faradhi kifaya, kila Muislamu anawajibika kushiriki katika mazishi kufanya hivyo kuna malipo makubwa mbele ya Allah (s.w) na yanapatikana mafunzo makubwa -kwa mwenye kuzingatia kifo. Hadith ifuatayo inatukumbusha wajibu kwa
ndugu zetu Waislamu:

 


Ally (r.a) amesimulid kuwa Mtume wa Allah amesema Muislamu kwa Muislamu mwingine anawajibika katika halt ya ioawaida kumfanyla ndugtuye mambo sits:
(i)Atamsalimia atakapokutana nave.
(ii)Ataitikia unto wake atakapomkarlbisha
(iii)Atakapopiga chafya na kusema "Al-hamdulillah" atamuitikia (kwa kuserna Rahmaka llaaahu)
(iv)Atamuangalia atakapokuwa mgonjwa.
(v)Atafuata jeneza lake atakapokufa na
(vi)Atampendelea kitu anachokipendelea yeye.

 


Na Hadithi ifuatayo inatuonesha umuhimu wa kushiztki katika mazishi:
Abu Hurairah (r.a) amesimutia kuwa Mtume wa Allah amesema "Atakayefuatajeneza kzMuisiamu akiwa noun ani na matamjioya kupata malipo (ku Allah) na hubakia na jeneza hiyo mpaka atakapois~yniin maiti na kisha akarnalizia mazishi yoke, bila, shako ata udi na malipo Qirat (malipo makubwa), kilo ghat at sawn ra mlima wa Ilhud Na yule atakayeiswalia na akaondoka kabla ya mazishi bila shako atanadi na Qirat moja”. (Bukhari na Muslim).

 


Kinachosisitizwa katika Hadithi hii ni kwamba kushiriki katika mazishi ni jambo muhimu kwa Muislamu. Pia Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa mtu azikwe mapema iwezekanavyo kama Hadithi ifuatayo in a vyotu fa ham is ha:

 


Huswayu bin Wahwal (r.a) amesimulia kuwa Talha bin Bara’a (r.a) aliugua. Hivyo Mtume (s.a.w) alikuja kumwona akasema:“Hakika simwoni Talha ila kifo kimeshampitia.Kwa hiyo nipeni amri juu yake (yaani niruhusuni nimswalie na kumzika) na fanyeni haraka si vizuri (si sawa) maiti ya Mu is lamu kungojeleshwa juu ya migongo ya watu wa familia yake”. (Abu Daud).

 

Utaratibu wa kuzika ni kama ifuatavyo:
1. Wateremke watu kaburini wenye idadi ya witri watatu, watano.

 


2. Jeneza liwekwe upande itakapokuwa miguu ya maiti.

 


3. Maiti atolewe kwa kutanguliza kichwa.

 


4. Maiti atakapoingizwa ndani ya kaburi, wapokeaji watamuweka magotini na kufungua kamba au vitanzi vyote vitatu vya miguuni, tumboni na kichwani. Pia watafunua shavu la kulia ili liguse ardhini wakati maiti itakapolazwa.

 

5. Maiti atalazwa kwa ubavu wa kulia k at ik a mwanandani na kuelekezwa Qibla.
Wakati wa kumlaza ni sunnah kusema maneno yaliyoelezwa katika Hadith iliyosimuliwa na Ibn Umar (r.a) kuwa
Mtume (s.a.w) alipokuwa akizika alikuwa akisema: "Bismillahi wabillahi wa-’alaa millati Rasuulullahi" “Kwa jina la Allah na kwa uwezo wa Allah na kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume wa Allah”. (Ahmad, Tirmidh, Ibn Majah)

 


6. Maiti apindwe kidogo miguuni na kichwani kwa kiasi ambacho uso na miguu iwe imegusa kuta za mwanandani.Kifua, tumbo na sehemu nyingine za katikati zibinuliwe nyuma kidogo.

 


7. Maiti awekewe mawe nyuma ya kichwa na nyuma ya miguu ili isije binuka na kukaa visivyo. Kisha ni sunnah kusoma aya za Qur-an kama iliyoelekezwa katika Hadith ifu atayo:

 


Abdullah bin Umar (r.a) anasimulia kuwa amemskikia Mtume (s.a.w) akisema “wakati mmoja wenu atakapokufa, msimcheleweshe, bali mzikeni haraka haraka. Msomeeni aya 1-5 ya Sura ya pili au aya mbili za mwisho wa Suratul Baqara - 2:285-286)”. (Baihaqi).

 

8.Maiti afunike kwa ubao, na kama patakuwa na sehemu zilizo wazi kiasi cha kuruhusu udongo kumfikia maiti zisiribwe kwa majani.

 


9.Kabla kaburi haijafunikwa, vitupiwe viganja vitatu vya udongo na katika kila tupio ni Sunnah kusema:

 


10.Kaburi lijazwe mchanga mpaka lijae na kisha liinuliwe kidogo kiasi cha shubiri moja.lwekwe alama kichwani na miguuni au ipandwe miti mibichi katika pembe za kaburi
ibakie kuwa alama za kaburi hilo. Pia ni vizuri kumimina maji juu ya kaburi iii kuufanya udongo ushikamane na usipeperushwe na upepo. Ni haramu kulijengea kaburi kwa namna yoyote ile, kukaa juu yake, kuwasha taa juu yake na kulielekea wakati wa kuswali kwa ushahidi wa Hadith zifuatazo:

 


Jabir (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amekataza kuyajengea makabun au kuyajengea nyumba juu yake au kukaa juu yoke. (Muslim).

 


Abu Marsad al-ghafanyyi ameelezq ku9,a Mtume wa Allah amesema Msikae juu ya trtalcabttri na u~ala msiswali kwa kuyaelekea". (Muslim.).

 


Baada ya kuzika Mtume(s.a.w) alikuwa akisin'riama baina ya kaburi na kaburi na kusema: Muombeeni msamaha ndugu yenu na murnuombee awe na kauli thubiti, kwani sass anaulizwa.

 


Yaliyo muhimu kuyafanya baada ya mazishi ni kuwashika wafiwa mikono na kuwausia kusubiri kwani kutokewa na msiba ni jambo la kawaida la maumbile na pia ni mtihani kwetu na watakaofaulu mtihani huu ni wale watakao subiri ambao wanapopata msiba husema: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye tutarejea ”. (2:155-156).

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    2 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    3 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    4 Jifunze Fiqh    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika
Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu. Soma Zaidi...

image Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kujitwaharisha Najisi hafifu na najisi ndogo
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi hafifu na najisi ndogo. Soma Zaidi...

image Kujitwaharisha kutokana na najisi
Post hii itakufundisha namna ya kutwaharisha Najisi. Soma Zaidi...

image Je ni nani mwenye haki ya kutaliki
Hapabutajifunza endapp mwanamke anahitaji kuachwa ni nini anatakiwa afanye. Soma Zaidi...

image Ni nini maana ya uchumi katika uislamu
Katikabuislamu dhana ya uchumi imetofautiana na dhana ya kidunia hivi leo ambapo kamari na riba ni moja ya vitu muhimu katika uchumi. Soma Zaidi...

image Mambo yanayoharibu Udhu (yanayobatilisha udhu)
Post hii inakwenda kukufundisha mambo ambayo hubatilisha udhu yaani mam,boa mbayo yanaharibu udhu. Soma Zaidi...

image Mambo anayofanyiwa mtu anayekaribia kufa
Haya ni maandalizi anayofanyiwa mtu aliye katika kilevi cha kifo yaani sakaratul maut Soma Zaidi...

image Dhana ya kumiliki raslimali katika uislamu
Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu. Soma Zaidi...

image Sifa za kuwa maamuma kwenye swala na namna ya kumfuata imamu
Post hii inakwenda kukuelezea sifa za kuwa maamuma na taratibu za kumfuata imamu. Soma Zaidi...