Hukumu ya Talaka kabla ya kufanya jimai

Talaka Kabla ya Jimai:Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa.

Hukumu ya Talaka kabla ya kufanya jimai

Talaka Kabla ya Jimai:
Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa. Mwanamume atatoa talaka na mkewe ataachika hapo hapo bila ya kukaa eda. Kama mwanamume ameshatoa mahari hatadai chochote kama yeye ndiye aliyeamua kumuacha mkewe bali atalazimika kumpa kiliwazo (kitoka nyumba). Ikiwa hajatoa mahari atalazimika kutoa nusu ya mahari. Kama mke ndiye aliyedai talaka atalazimika kumrudishia mumewe mahari aliyompa. Hukumu ya talaka ya ama hii inabainika katika aya zifuatazo:


Si dhambi kwenu kama mkiwapa wanawake talaka ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari (yao). Lakini wapeni cha kuwaliwaza (kitoka nyumba); mwenye wasaa kadiri awezavyo, na mwenye dhiki kadiri awezavyo. Matumizi hayo (wanayopewa) yawe kama inavyosema Sharia. Ndio wajibu kwa wafanyao mema. (2:236)


Na kama mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa na mmekwisha wawekea hayo mahari (basi (wapeni) nusu ya hayo mahari mliyoagana, isipokuwa wanawake wenyewe waache (wasitake kitu), au yule (mume) ambaye kifungo cha ndoa ki mikononi mwake aache (haki yake kwa kumpa mahari kamili). Na kuachiana ndiyo kunakomkurubisha mtu sana na kumcha Mungu. Wala msisahau kufanyiana ihsani baina yenu; hakika Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayoyafanya. (2:237)


Talaka ya Aliyerukwa na akili na aliyetenzwa nguvu
Talaka si jambo Ia kulifanyia maskhara Muislamu anatakiwa awe hadhiri wakati wa kutoa talaka. Ahakikishe kuwa wakati anaamua kutoa talaka akili yake iko katika hali ya utulivu. Talaka ya aliyerukwa na akili haiswihi kama tunavyojifunza katika Hadith:



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Kila talaka ni halali isipokuwa talaka ya punguani na mwenye kurukwa na akili". (Tirmidh).
Pia mtu akilazimishwa kutoa talaka pasina sababu za kisheria au mume na mke wakitalakishwa kwa nguvu huku bado wanapendana katika mipaka ya Allah (s.w), talaka hiyo haitaswihi kama tunavyojifunza katika Hadithi:



Aysha (r.a) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allah akisema: "Hakuna talaka wala hakuna kumwacha huru mtumwa kwa nguvu ". (Tirmidh).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1372

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana: