picha

je ni vipi vyakula vyenye protini kwa wingi?

Makala hii iatakuletea aina kuu tano za vywkula vyenye protini nyingi zaidi. Kama ulikuwa unajiuliza kuwa ni vyakula ipi hasa vinaweza kukupatia protini kwa wingi ni vipi, makala hii ndio majibu yako kwa swali hilo.

VYAKULA VYENYE PROTINI

Tunaweza kupata protini kwenye mimea jamii ya mikunde kama kunde na maharagwe. Pia kiasi kikubwa cha protini tunaweza kukipata kwa kula mayai, nyama, samaki, dagaa na maziwa. Pia tunaweza kupata protini kwa kula nafaka kama mchele na nafaka zingine. Ulaji wa mboga za majani unaweza pia kutupatia protini kwa kiasi kidogo. Wadudu kama kukbikukbi, senene na wengineo pia wanaweza kutupatia protini.


 

Kwa kifupi vyakula vinavyotupatia protini ni pamoja na :-

1. Samaki; samaki ni chanzo kizuri cha protini. Samaki wenye mafuta kama salmon ni vyanzo vyema zaidi vya protini. Ulaji wa samaki umekuwa ni chanzo kizuri cha protini hasa kwa wakazi wa maeneo ya baharini na maeneo ya pwani ama mitoni, mabwawa na maziwa. Tunaposema samaki hapa wanaingia mpaka dagaa, kaa, kaji, kamongo, perege, mikunga, papa na samaki wengine. Pia ulaji wa samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo, kukinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali, chanzo cha madini ya chumvi na fati


 

2. Mayai; mayai ni katika vyanzo vikubwa vya protini. Karibia watu wengi hujipatia protini kwa kula mayai. Unaweza kula yai likiwa limekaangwa, chemshwa ana la kuchoma. Pia unaweza kula yai bichi kama wafanyavyo baadhi ya watu. Ulaji wowote kati ya niliotaja unaweza kukupatia protini. Ila hakikisha kama umelikaanga ama kulichoma halikauki sana likawa kama chapati iliyokauka, upishi huu unaweza kuathiri virutubisho.


 

3. Maziwa; maziwa ni katika vyanzo vikuu vya protini kwa binadamu na wanyama. Maziwa ya mama ni chanzo kipekee kilicho salama zaidi kwa mtoto mchanga kuliko hata ya ng’ombe. Tofauti na kutupatia protini maziwa pia ni chanzo cha vitamini na fati. Maziwa ni katika vyakula vilivyokusanya viinilishe vyote muhimu. Ni vyema kuyachemshha maziwa kabla ya kuyanywa ili kuepuka baaadhi ya matatizo ya kiafya.


 

4. .Nyama; tunaweza kupata protini kwa kiasi kikubwa kwa kula nyama. Nyama ni katika vyanzo vizuri vya protini. Inaweza kuwa nyama nyekundu ama nyama nyeupe. Nyama nyeupe tunaweza kuzipata kwa kula kuku, baadhi ya samaki, kaa. Nyama nyekundu tunaweza kupata kwa kula mbuzi, kondoo na karibia wanyama wengi. Nyama pia ni chanzo kizuri cha fati mwilini. Ulaji wa nyama unaweza kuleta athari za protini kwa muda mchache sana.


 

5. Mimea aina ya kunde na nafaka; mimea jamii ya kunde hii ni mimea ambayo inatambaa kama kunnde na maharagwe na mimea jamii hii. Mimea hii inatambulika kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Watu wenye kipato cha chini mimea hii ni chanzo chao cha msingi cha kupata protini. Maharagwe yapo katika aina nyingi yapo ya soya na aina mbalimbali. Ulaji wa aina zote hizi unaweza kutupatia protini.


 

6. Mboga za majani. Kwa kiwango kilicho kidogo tunaweza kupata protini kwa kula mboga za majani. Mboga za majani oekee hazitoshelezi kutupatia kiwango cha protini kinachohitajika. Kwa wale ambao hawali chama (vegetarian) wapo ambao hawali nyama lakini wanakula mayai na maziwa hawa wanaweza kujipati protini kwenye mayai na maziwa. Lakini kwa wale ambao hawali nyama, maziwa wala mayai watahitajika kupata vyamzo vingine mbadala vya protini yaani watumie protini za kutengeneza japo miongoni mwazo zipia mbazo zinatengenezwa kwa wanyama.


 

7. Vyanzo vingune: tofauti na vyanzo vya protini nilivyotaja hapo juu lakini pia kuna vyanzo vingine kama ulaji wa senene na kumbikumbi na wanaofanana. Kuna baadhi ya jamii zinakula senene hasa jamii zinazopatikana maeneo ya kagera. Kwao senen ni chanzo kizuri sana cha protini. Kumbikumbi nao hupatikana maeneo mengi na jamii nyingi zinatumia chakula hiki.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2021-05-31 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 1842

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 web hosting    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Faida za kula mayai

Posti hii inahusu zaidi faida anazozipata mtu anayekula mayai hasa wakati wa kifua kinywa, tunajua wazi kuwa mayai yana kiwango kikubwa cha protini pamoja na hayo kuna faida nyingi za kutumia mayai hasa wakati wa asubuhi kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Vyakula hatari kwa mwenye kisukari

Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula hatari kwa mwenye kisukari

Soma Zaidi...
Faida za kula Tango

Matunda ya zamani na ya asili, zijuwe faida za kiafya za tango

Soma Zaidi...
Faida za kula Faida za kula Boga

Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako

Soma Zaidi...
Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake

Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake

Soma Zaidi...
Kitabu cha Afya 02

Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili.

Soma Zaidi...
Faida za kitunguu maji/ onion

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu umuhimu wa kitunguu maji mwilini

Soma Zaidi...
Vyakula vya vitamin A

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin A

Soma Zaidi...
Faida kuu 10 za kula matunda na mboga mwilini - kwa nini ni muhumu kula matunda?

Makala hii inakwenda kukutajia sababau kuu 10 ambazo zinaonyesha umuhimu wa kula matunda kiafya. kwa nini kiafya unashauriwa ule matunda na mboga mara kwa mara?

Soma Zaidi...