Vyakula vya kuoambana na mafua

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua

.VYAKULA VYA KUPAMBANA NA MAFUAMafua ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya mafua na pia inasadikika kuwa zipo takribani aina 200 za virusi hawa wa mafua wakiwemo rhinoviruses, parainfluenza viruses, enteroinfluenza viruses na vingine vingi. Virusi hivi hupatikana kwa kukutana na hewa yenye virusi hawa, pindi unapovuta hewa yenye mchanganyiko wa virusi hawa. Sababu zingine zinazosadikika kusababisha mafua ni panoja na sigara, moshi, mavumbi, baridi kuwa kali au kuchafuka kwa hewa.Udonjwa wa mafua unadalili tofauti tofauti na huenda zikafanana na ugonjwa wa malaria. Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kukosa hamu ya kula, kuhisi uchovu, kutokwa na makamasi mengi, koo kukereketa, maumivu ya kichwa na kupiga chafya mara kwa mara. Japo dalili za mafua hutofautiona kwa mtu na mtu kulingana na uwezo wa mwili wake kupambana na magonjwa ila hizi dalili tulizozitaja huwa maarufu kwa watu wengi.Mgonjwa wa mafua huenda akawa amechoka sana kiasi kwamba analala kitandani kwa homa kali aliyo nayo. Mafua huwaathiri zaidi watoto na wazee kwani miili yao haina kinga za kutosha kupambana na maradhi. Kwa wale wenye HIV+ ugonjwa wa mafua pia hueza ukawaletea athari kubwa sana ikiwemo homa kali na uchovu.Mtu ana weza kujikinga na mafua kwa kuosha mikono kabla na baada ya kula, kuziba mdomo anapopiga chafya. Kula vyakula vyenye vitamin A na C kwa wingi, kunywa maji mengi na kupunguza mawazo yaani "stress" kwa lunga ya kigeni hapa kinacho maanishwa ni kuwa na furaha. Jambo la msingi limgine ni kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mare humuepusha mtu na mafua kwa kiasi kikubwa.Miongoni mwa vyakula anavyotakiwa ale mwenye mafua ni kama mboga za majani zenye vitanimi kwa wingi, kwa mfano spinach, na mchicha. Pia kula matunda yenye vitamin C kwa wingi kama mapapai, na machungwa. Vyakula hivi husaidia katika kuupa mwili uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi na mashambulizi mengine. Maji ya kutosha humsaidia mtu mwili wake kuweza kufanya kazi ya kudhibiti maambukizi kwa urahisi. Hali kadhalika kufaya mazoezi husaidia mwili kufanya kazi vizuri. Pia anashauriwa mgomjwa wa mafua awe chai.Wapo baadhi ya wataalamu wa tiba mbadala wanazungumzia matumizi ya kitunguu maji kuhusu kutibu mafua. Wanatumia harufu ya kitunguu maji kutibu mafua. Mgonjwa atachukuwa kitunguu kasha ataondowa majani, au maganda ya juu kisha atakuwa anavuta haruvu ya kitungu. Atafanya hivyo kwa mara kadhaa hasa anapokwenda kulala.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 2074

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Zijue kazi za madini ya chuma mwilini

Posti hii inahusu zaidi kazi za madini ya chuma mwilini,Ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini na pia utokana na vyakula mbalimbali ambavyo upatikana kwenye wanyama na mimea. Zifuatazo ni kazi za madini ya chuma.

Soma Zaidi...
Rangi za majimaji yanayotoka kwenye uke na maana yake kiafya

Je unajuwa kuwa majimaji yanayotoka ukeni yanatueleza mengi kuhusu afya yako, rangi za majimaji ya ukeni na damu ya hedhi

Soma Zaidi...
Asili ya vyakula vya madini ya zinki

Post hii inahusu zaidi asili ya madini ya zinki, hii inaonesha sehemu gani tunaaweza kupata madini ya zinki.

Soma Zaidi...
Faida za mchai chai

Posti hii inahusu zaidi faida za mchai chai, ni mmea ambao upandwa na watu kama maua, dawa au kikolezo cha chai na Kuna wengine kabisa wanatumia kama sehemu Mojawapo ya dawa kwa hiyo tutaona faida za mmea huu wa mchai chai.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za viazi vitamu

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula viazi vitamin

Soma Zaidi...
Faida za limao au ndimu

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ndimu au limao

Soma Zaidi...
Dalili za upungufu wa vitamini C

Utajuaje kama una upungufu wa vitamini C. Zijuwe dalili za upungufu wa vitamini C hapa

Soma Zaidi...
Ni katika kiungo kipi cha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula virutubisho hufonzwa?

Post hii itakupa elimu kuhusu mfumo wa mmrng'enyobwa chakula unavyo fanyankazi

Soma Zaidi...